PostGE2025 Rais Samia: Hii ni ripoti ya Rais, aliyeunda Tume ni Rais, wasitokee watu wengine wakadai ownership

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Hiyo kauli hii ni "ripoti ya Rais" maana yake anakwenda kuifungia hiyo ripoti ofisini kwake, asiulizwe kilichomo wala hatua atakazochukua kulingana na mapendekezo ya hiyo ripoti.

Ndio maana waelewa walishasema toka mwanzo hiyo ripoti haina maana, ni mpango uliosukwa kumsafisha muhusika mkuu wa yale mauaji, na kuudanganya ulimeengu ripoti ilishaundwa na mapendekezo yako ofisini kwake.

Bahati nzuri ulimwengu nao haudanganyiki, unataka ripoti ya wachunguzi huru. Sio wachunguzi waliotumwa na Rais waende waangalie maeneo yapi kufanya kazi yao.

Wakina Jaji Chande walikuwa watumwa wa Samia, hawakuwa huru kufanya kazi yao, ndio maana baada ya kuona mambo magumu, wakatumwa na bosi wao waka "edit".

Kilichomo kwenye hiyo ripoti ya leo ni matokeo ya "editing", walienda kufuta maeneo yote yaliyomkera Samia, wakaandika mambo ya kumpendeza, ndio maana sasa anasema hiyo ripoti ni mali yake.

Nami nasema kweli hiyo ripoti ni mali yake, aipeleke Kizimkazi akaifungie chumbani kwake, wala hatuna shida na maigizo yake.
 
Politics is about the characteristic blend of conflict and co-operation that can be found so often in human interactions. Pure conflict is war. Pure co-operation is true love. Politics is a mixture of both.

Michael Laver
 
Do ki ta Samuya. 😭😭😭😭 Taifa la Tanzania tumeangukia kweli.
 
Sisi wananchi ndo maboss kama wanavyotuita.. tunasema report iwekwe kwa umma kama file za Epstain
 
Kila aliyehusika na massacre ya 2025 atachanganyikiwa kwa wakati wake!
 
Hivi kwenye huu mchakato wote kuanzia mashahidi mpaka mashuhuda hakuna sehemu walisema kuhusu kunyimwa HAKI? Maana mchakato mzima unaanza nasikia kuhusu Amani tu, Amani bila haki! Ajabu sana hii
 
Raisi Samia ameomba mtu yoyote hatakiwi kuomba Ripoti ya Tume ya Jaji chande kwasababu hiyo Ripoti imeandaliwa kwaajili yake na yeye ndio aliounda hiyo tume.
 
Basi sawa, hiyo ripoti ni yake.
Sasa tunahitaji Tume Huru ya Uchunguzi itakayotoa ripoti huru yenye ukweli wote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…