Rais Samia: Huenda kesi zimepungua Polisi kwasababu wananchi wamekata tamaa kupata haki zao

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema huenda makosa yamepungua Polisi Watanzania hawaendi Vituoni kuripoti kwasababu wamekata tamaa kutokana na kutopata Haki zao.

Ameeleza hayo leo Jijini Dar es Salaam katika ufunguzi wa Kikao Kazi cha Maafisa Wakuu Waandamizi wa Jeshi la Polisi na Makamanda wa Polisi wa Mikoa/Vikosi.

Amesema sababu nyingine ambayo inaweza kupelekea Kesi kupungua ni umbali wa Vituo vya Polisi ambao hupelekea watu kumalizana pasipo kufika Vituoni, na wakati mwingine husababisha wachukue #Sheria mikononi.
 
Kwa hiyo Raisi ana ushauri upi ili kesi zifurike polisi na mahakamani Hadi mafaili ya kesi yajae kila Kona Hadi corridor za vituo vya polisi na ofisi za mahakama?
 
Mimi nilijua baada ya kutoka Zambia, kaunganisha DRC!!
 
Wewe mama mbona uko hivyo. tatizo unalijua , it was your turn to come out with a solution kuwa kuanzia leo hakuna kumpeleka mtu mahabusu /mahakamani bila kuwa na ushahidi/upelelezi kukamilika, hakuna kuwaweka watu ndani zaidi ya saa 48 kama sheria inavyosema.

Sasa ngonjela za nini? Polisi hawa Lisu ame wa describe vizuri kuwa thinking capacity yao ni ndogo, wanavaa magwanda kuchukua rushwa.
 
Ukienda polisi kuripoti siku hizi lazima uwe na pesa mfukoni, kama hauna hautasikilizwa, na mbaya wako akifika polisi na pesa mfukoni yeye ataachiwa halafu wewe mshtaki ubaki ndani uje kutolewa na ndugu au rafiki zako, polisi wetu kumuita mtu gaidi siku hizi ni suala la sekunde tu.
 
Ilinikuta iyo acha tu
 
Sasa nchi yetu inakuwa nzuri zaidi, kama watu hawaendi tena polisi, wanamazana tuu huko mitaani.
Hii ni hatua njema, kama vile Hamza alivyomalizana na Polisi Juzi 😉 😉 😉 😉 🤣 🤣 🤣
 
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema huenda makosa yamepungua Polisi Watanzania hawaendi Vituoni kuripoti kwasababu wamekata tamaa kutokana na kutopata Haki zao.

Ameeleza hayo leo Jijini Dar es Salaam katika ufunguzi wa Kikao Kazi cha Maafisa Wakuu Waandamizi wa Jeshi la Polisi na Makamanda wa Polisi wa Mikoa/Vikosi.

Amesema sababu nyingine ambayo inaweza kupelekea Kesi kupungua ni umbali wa Vituo vya Polisi ambao hupelekea watu kumalizana pasipo kufika Vituoni, na wakati mwingine husababisha wachukue #Sheria mikononi.
Makosa yanayofanywa na Polisi si kwamba hayajulikani na si kwamba hata rais hayajui, isipokuwa ni kwa sababu wanasiasa wameamua kuwatumia kwa maslahi binafsi hivyo wanawaacha makusudi wafanye wapendavyo.

Hata likifumuliwa kusukwa upya hakutakuwa na Polisi mpya asiye na tabia hizi za wote labda waagizwe kutoka nje ya Tanzania!
 
Kweli
 
Kesi zimepungua vipi wakati magereza yamejaa mahabusu wanaosubiri kesi zao japo kutajwa tu?
 
Back
Top Bottom