Rais Samia, ikikupendeza tunaomba uwateue hawa wapinzani katika Serikali yako

Rais Samia, ikikupendeza tunaomba uwateue hawa wapinzani katika Serikali yako

Mr Dudumizi

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2020
Posts
7,799
Reaction score
14,215
Mh Rais, ningependa kukusalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Ama baada ya salamu, Mh Rais ikikupendeza tunaomba umteue Mbowe kuwa mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, huku Zitto Kabwe ukimpa mkoa wa Kigoma.

Najua rais hapangiwi ila huu ni ushauri wangu tu kwako mama yetu, kwa lengo la kudumisha amani, umoja na upendo zaidi kwenye nchi yetu.
 
Sema awahonge vyeo, ila nitamdharau sana Mbowe kama atakubali hivyo vyeo vya kitapeli.
Lissu ameshatoa msimamo kuhusu ushirikishwaji wa Chadema kwenye uongozi. Kwa kifupi amesema utakuwa ni ujinga kukubali kupewa vyeo ambavyo wanakuwa kama wanasesere, wanategemea kuteuliwa (na kutumbuliwa na rais).

Amesema hii ni kama kubariki kushiriki kwenye uozo. Sidhani kama hata watu wanatakiwa kwenda mbali kujua madhara yake bali ni kuangalia kinachotokea Zanzibar sasa hivi au kilichotokea Kenya kipindi cha Odinga akiwa waziri mkuu. Anayetaka kusikiliza kwa kirefu link hii hapa chini.

 
Lissu ameshatoa msimamo kuhusu ushirikishwaji wa Chadema kwenye uongozi. Kwa kifupi amesema utakuwa ni ujinga kukubali kupewa vyeo ambavyo wanakuwa kama wanasesere, wanategemea kuteuliwa (na kutumbuliwa na rais). Amesema hii ni kama kubariki kushiriki kwenye uozo. Sidhani kama hata watu wanatakiwa kwenda mbali kujua madhara yake bali ni kuangalia kinachotokea Zanzibar sasa hivi au kilichotokea Kenya kipindi cha Odinga akiwa waziri mkuu. Anayetaka kusikiliza kwa kirefu link hii hapa chini


Kabisa, na watawala wa kiafrika ni wazuri kwenye kuhadaa viongozi wa upinzani wasaka maslahi binafsi.
 
Kabisa, na watawala wa kiafrika ni wazuri kwenye kuhadaa viongozi wa upinzani wasaka maslahi binafsi.
Ni kwa nini Hawa watu wa ccm wanawaza sana vyeo vya kuteuliwa? Ikiwa mbowe na Lissu walihitaji hivyo vyeo si wangeshavipata tokea awamu ya mkapa?
 
Hapo kuna mmoja ndiye ana deserve hicho chao maana tayari ni muumini
Mkuu hapa unamaanisha huyo wa juu au chini?

images (15).jpeg


images (17).jpeg


images (25).jpeg
 
Mh Rais, ningependa kukusalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Ama baada ya salamu, Mh Rais ikikupendeza tunaomba umteue Mbowe kuwa mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, huku Zito Kabwe ukimpa mkoa wa Kigoma.

Najua rais hapangiwi ila huu ni ushauri wangu tu kwako mama yetu, kwa lengo la kudumisha amani, umoja na upendo zaidi kwenye nchi yetu.
Na Lissu naye atakuwa nani...?
 
Kumpa mbowe ukuu wa mkoa hata uwaziri hii ni sawa na ‘demotion’ kwake, unune usi nune Mbowe ni ‘presidential candidate’
 
Mmmh kujiaibisha tu,si mjipiganie au mko after matumbo yenu,upinzani sjui nini shida,mnataka mpewe position na sympathy au?
 
Back
Top Bottom