Remembrance
Member
- Jun 22, 2020
- 74
- 180
Suala sio kufuta jeshi la polisi, hapo ni suala la nidhamu na kuajiri askari wanaofaa. Ndio nimesema mfumo mzima wa traffic polisi la lazima ubadilike, vinginevyo ni kuhamisha rushwa kwenye kitengo kingine. Wewe unadhani Camera itamshika dereva mlevi au ambae anaendesha huku anatext na simu yake? Haiwezekani.Polisi hawafutwi. Wanapunguziwa majukumu. Badala ya kusimama na camera za mwendo kasi, camera zinakuwepo wakati wote hata usiku. Badala ya kuzungumza na wewe ili usilipe fain ya overspeed, fain inaingia moja kwa moja kwenye bili ya gari lako. Badala ya kusimamisha simamisha magari na kuomba kuangalia fain, akikusimamisha tayari anajua una fain. Mambo mazuri haya si ya kupinga.
Kama hakuna madaliko kwenye mfumo wa traffic, rushwa inahamia kwenye kitengo cha Camera.
Halafu Kuna suala la gharama, nadhani system ya Camera moja tu, hata kama inatoka China, sio chini $50,000 kama sio zaidi. Serikali inashindwa kuwalipa vizuri traffic polisi, ipo tayari kuingia gharama hii kwa ajili ya usalama barabarani? Mungu ibariki Tanzania.