Rais Samia: Ili kudhibiti rushwa barabarani, trafiki waondoke barabarani, kamera na taa ndio zifanye kazi

Rais Samia: Ili kudhibiti rushwa barabarani, trafiki waondoke barabarani, kamera na taa ndio zifanye kazi

Rais Samia ameagiza kuanza kuondolewa Kwa Matrafiki ambao walijigeuza Wala Rushwa Barabarani badala yake ametaka zifungwe Kamera na Taa Ili Kuongoza magari.

---
Rais Samia Suluhu Hassan amesema katika kukabiliana na rushwa nchini, trafiki barabarani wanapaswa kuondolewa badala yake taa na kamera zitatumika kuongoza barabarani.

Rais Samia ameyasema hayo leo, Ikulu jijini Dar es Salaam katika hafla ya kuapisha viongozi wateule wa ngazi mbalimbali za uongozi nchini

“Usalama barabarani, tunataka kuondoa trafiki barabarani kukomesha rushwa. Tuyaache mambo ya pita wewe nenda wewe”

My Take
Naunga mkono hoja ya Mh.Rais.

Trafiki waligeuza usalama Barabarani kuwa mradi wa kuvuna pesa za Rushwa Kwa maderva huku ajali na makosa mengine yakizidi kuongezeka.

Kenya wameweza na sisi tuanze maana tulichepewa sana.

Tukitoka hapo tufungue kamela kwenye Mahospitali na kuwavalisha kamela maafisa wa TRA.
Enzi ya Kikwete kuna madogo wa DIT wali come up na Application ya kuongoza Magari kwenye mataa kwa baadhi ya maeneo. Presention fresh, simulation kbs....lilipokuja suala la implementation kuna wakuda walikwamisha purposely nadhani ni wale wanufaika na rushwa. Heko kwa Mh. Rais hili lifike mwisho usikubali wachache watukwamishe kwa manufaa yao!!!
 
“Usalama barabarani, tunataka kuondoa trafiki barabarani kukomesha rushwa. Tuyaache mambo ya pita wewe nenda wewe”

Viongozi wetu mabingwa sana wa kuongea mbele ya kadamnasi...

Jambo lolote la maendeleo ili liweze kufanikiwa linapaswa litungiwe sera, halafu ufuatiliaji na uwajibikaji uanzie hapo...

Yes, zitafungwa kamera na taa, lakini mla rushwa atahamia kwenye vyqnzo vingine...
 
Makamanda Waende Lindo Banks Haitawezekana
 
Ukiwa mtu wa kutumia akili za kawaida ktk mambo makubwa haya ndio madhara yake.

Rushwa ya polisi usalama barabarani haina madhara makubwa kama rushwa ya vituo vya polisi,kule haki zinapokwa wazi wazi,lakini barabarani mlalamikaji ni mizimu.hakuna mlalamikaji wa moja kwa moja zaidi ya wanafiki na watu wasio watumiaji wa barabara.huyu rais pamoja na viongozu wengine ndio wanufaika NO 1 wa uwepo wa hao traffic police barabarani kwa kupitishwa barabarani bila kupanga foreni,sijui kafikiri camera zitazibaje gape hilo???

Anapoamua kuweka camera ktk junction zirenge kunasa matukio ya matumizi ya barabara sio kuondoa kuondoa traffic anaohisi wanakula sana rushwa labda kuliko yeye.

Na kama ameamua kuwaondoa traffic basi isiwe sababu wanachukua rushwa,bali sababu hawahitajiki barabarani,kitu ambacho sidhani kama kipo nchi yoyote tofauti na nchi hii ya katafunua.
 
Kwahiyo ile Hela ya "kubrashia Viatu" ya mtangulizi wake ameikiuka?
 
Polisi hawafutwi. Wanapunguziwa majukumu. Badala ya kusimama na camera za mwendo kasi, camera zinakuwepo wakati wote hata usiku. Badala ya kuzungumza na wewe ili usilipe fain ya overspeed, fain inaingia moja kwa moja kwenye bili ya gari lako. Badala ya kusimamisha simamisha magari na kuomba kuangalia fain, akikusimamisha tayari anajua una fain. Mambo mazuri haya si ya kupinga.
Hakuna jukumu lolote linalopungua hapo.

Unajua shida ya nchi hii ni unafiki tu unatusumbua,huyu rais mzima ana adress jambo hili kimajungi majungu badala ya kulihandle kiamiri jeshi.

Polisi anakula rushwa sababu anasimama ilipo haki na batili,yaani ndiye msimamizi wa ufuataji wa sheria,hela anapewa na wasiotaka kufata sheria,ulizeni polisi wanaofatilia madeni mkaone rushwa nyingine msiyoijua.fine inaandikwa na traffic ambaye ataporwa majukumu na hii camera ya samia,lakini anayeshinikiza ulipaji ni polisi 2 anayekuja kukagua baada ya miezi kadhaa,rushwa inakwepwaje hapo kwa polisi???

Tuache unafiki,huyu mama awalipe watu hela za maana kisha azingatie nidhamu na rushwa kutoka juu,aonekama kuna traffic atagusa hela.

Watu wanajikatia tu mihela huko juu,unakuja na ngonjera za elfu 2 za traffic,hata laana huogopi!!!ndio maana JPM aliwahi kusema hizi sio ruswa,watu hawaijui rushwa inayoumiza.
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Kuna watu naona wanayo in hiisonya TU.Mh Raisi hili ukilisimamia na kutengeka utakuwa umejenga Iman kubwa kwetu wananchi.
 
DAR ES SALAAM: RAIS Samia Suluhu Hassan amesema katika kukabiliana na rushwa nchini, trafiki barabarani wanapaswa kuondolewa badala yake taa na kamera zitatumika kuongoza barabarani.

Rais Samia ameyasema hayo leo, Ikulu jijini Dar es Salaam katika hafla ya kuapisha viongozi wateule wa ngazi mbalimbali za uongozi nchini

“Usalama barabarani, tunataka kuondoa trafiki barabarani kukomesha rushwa. Tuyaache mambo ya pita wewe nenda wewe”,” amesema Dk Samia.

#Japo hili lilichelewa lakini kwa sasa ni wakati muafaka.

IMG_20240405_003638_802.jpg
see
 
Iwekwe sheria ya kuua mpokea na mtoa rushwa.

Simpo.
 
Iwekwe sheria ya kuua mpokea na mtoa rushwa.

Simpo.
Kuua, kufisha, kwa sababu ya rushwa, ilihali maisha yetu ni kiduchu hapa duniani, sheria za kuua hufanywa na watu wasio na deep thoughts, kufisha ni kumuingilia muumba katika utashi wake juu ya kiumbe chake!.
 
Tutawaambia Wachina.
 
Za chini ya kapeti ni kwamba huu mradi umefufuliwa baada ya JPM kuukataa kipindi Kangi Lugola akiwa waziri wa mambo ya ndani kutokana na upigaji.
Rais Samia ameagiza kuanza kuondolewa Kwa Matrafiki ambao walijigeuza Wala Rushwa Barabarani badala yake ametaka zifungwe Kamera na Taa Ili Kuongoza magari.

---
Rais Samia Suluhu Hassan amesema katika kukabiliana na rushwa nchini, trafiki barabarani wanapaswa kuondolewa badala yake taa na kamera zitatumika kuongoza barabarani.

Rais Samia ameyasema hayo leo, Ikulu jijini Dar es Salaam katika hafla ya kuapisha viongozi wateule wa ngazi mbalimbali za uongozi nchini

“Usalama barabarani, tunataka kuondoa trafiki barabarani kukomesha rushwa. Tuyaache mambo ya pita wewe nenda wewe”

My Take
Naunga mkono hoja ya Mh.Rais.

Trafiki waligeuza usalama Barabarani kuwa mradi wa kuvuna pesa za Rushwa Kwa maderva huku ajali na makosa mengine yakizidi kuongezeka.

Kenya wameweza na sisi tuanze maana tulichepewa sana.

Tukitoka hapo tufungue kamela kwenye Mahospitali na kuwavalisha kamela maafisa wa TRA.
 
Acha ujinga, traffic wamezidi, acha tutumie hizo gharama, kama kazi hawawezi bila kula rushwa waende wakalime.
Punguza jazba dogo! Public Policy haziendi hivyo. Unataka kuleta ufanisi kwenye kitengo chochote, badilisha mfumo mzima, ongeza mafunzo/ marupurupu na supervision. Vinginevyo ni kama kuziba Ufa kwa kutumia chewing gum. Hakuna la maana hapo. Ulaji unahamishwa kwenye Camera.

Nyie ndio walewale, wape ATC ndege nyingi baadae wataingiza faida. Matokeo yake ni hasara kila siku. Unataka kuleta mabadiliko, sio bandika bandua. Fumua system nzima.
 
Back
Top Bottom