Rais Samia ingilia kati, TRA watatukwamisha

Maybe ni strategy ya kuleta hela mtaani, si watu wanalilia mzunguko wa pesa mtaani? Ngoja raia wafuje ili zije mtaani.
 
Waliambiwa wakajadiliane na walipa kodi.

Ninadhani ndio hizo kazi za nje.

Wanawabembeleza walipa kodi..mambo yatakaa vizuri muda sii mrefu. Usihofu.
Lack of professionalism. Tumieni nguvu basi kama mtapata kodi...kwa mantiki hii, TRA inahitaji kusukwa upya. Iwe na watu wanaojitambua na wanatambua wajibu wao. TRA sio jeshi. Ni taasisi yenye waajibu wa kukusanya kodi na kuwalinda walipa kodi ili kodi iwe endelevu. TRA ya sasa inataka kukusanya kodi bila kujua wana wajibu wa kuwalinda walipa kodi kwa kudai kodi halali.
 
Hakuna Urafiki wa watoza kodi na wafanyabiashara dunia nzima (nature of Tax incidence)
Mkuu naomba usiweke mawazo ya jumla. Wanaofanya kuwe na uadui kati ya watoza kodi na wafanyabiashara ni watoza kodi wenyewe. Yaani kuanzia kwenye kukadiriwa utahojiwa kama uko kwenye Kituo cha Polisi. Ukiwaomba mfike kwenye eneo la biashara yako hawataki ni full kukadiria wapendavyo. Njoo sasa wakati wa kulipa makadirio waliyofanya, utakuta hata mtoa controll number anakuuliza "mbona umekadiriwa kidogo hivyo, kwanini". Halafu hiyo controll number kuipata unaisotea ni balaa. Sasa hapo unategemea nini?
 
nitakuunga mkono ukinionesha uthibitisho wa kuwa wewe ni mlipa kodi ya moja kwa moja. Weka payments zako za kodi kwa quarter ya kwanza ya mwaka tuone ulivyocomply kabla ya kuja na kulalamika.
 
Hebu mnyonge mnyongeni haki yake mpeni, kweli unawezaje kukubali tu ubambikiwe.Mimi wjaribu maana natunza rekodi zangu zote za mauzo ,manunuzi na matumizi ya biashara.Hapa najua ndiyo dawa kutunza kumbukumbu tu maana hata bodi au mahakama ya rufaa ya kodi ntafika.
 
Bora wametoa hii TRA maana walitaka msingizia baba wa watu bure. Yaani kuna vitu vingine unaona ni wivu tu au utakuta huyu mkuu wao tra ni msimamizi mzuri katika makusanyo.
 
Form six mna akili ndogo sana. Kwani hilo tatizo analo zungumzia mtoa mada linamuongelea babu yako, au linazungumzia TRA? Unafahamu maana ya OP wewe?
Umejibu kwa ghalabu. Dalili ya kuonyesha nilichosema kimekuingia panapo stahili na umepata ujumbe sahihi.
 
Samia ana marafiki gani ishu ya kodi na makusanyo yake kazingua sana na itamzingua mwenyewe. Mtake msitake kazingua kodi ndio uhai na heshima ya serikali. Mkisifia sifia ila ukweli kuhusu kodi ni kituko.
Mkuu 'Galileo_Gaucho' ni vizuri wakati mwingine kumsoma mtu na kuelewa kilichoandikwa.

Sikueleza chochote hapo juu kuonyesha kuwa kodi sio muhimu kwa nchi yoyote duniani; na wala sijamsifia lolote juu ya marafiki zake wafanya biashara.
Kama lisemwalo ni kweli, basi sote, mimi nawe tusubiri kuyaona matokeo. Maana haya hayajifichi.
 
Sasa majungu yako wapi hapo! Mimi nimetoa tu maoni yangu na tena nimeshauri! Au umeona nimemtaja mtu, zaidi ya kuitaja hiyo Taasisi? Uwe una akili hata kidogo basi.
Unawalalamikia TRA kwamba wanafanya makadirio unapotaka kuanza biashara bila kufika site. Nimehoji wafike kwenye biashara ipi wakati ndio umewafuata ili wakukadirie? Hayo kama sio majungu ni nini kumbe?
 
Unawalalamikia TRA kwamba wanafanya makadirio unapotaka kuanza biashara bila kufika site. Nimehoji wafike kwenye biashara ipi wakati ndio umewafuata ili wakukadirie? Hayo kama sio majungu ni nini kumbe?
Usikute nabishana na mtu ambaye hajui hata TIN ni kitu gani. Katika hali ya kawaida unawezaje kulipia mapato pasipo na biashara?

Na unapoenda kulipia, ndiyo wanakukadiria kodi pasipo kufika kwenye eneo ilipo biashara! Sasa wewe unaongea kama umekunywa pombe za kienyeji! Unanichosha tu hapa. Eti majungu! Yaani niionee majungu TRA!
 
Umejibu kwa ghalabu. Dalili ya kuonyesha nilichosema kimekuingia panapo stahili na umepata ujumbe sahihi.
Nimekupa jibu lililo endana na ulicho kiandika. Mada ilihusu ina mahusiano na TRA! Hivyo sikuwa OP kama ulivyochulia wewe. Wewe ndiyo umekurupuka.
 

TRA wanatoa leseni za biashara..?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…