Rais Samia, ingilia kati tulipwe fedha za mradi wa Ufugaji samaki kupitia Vizimba-Mwanza

Rashidi Jololo

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2022
Posts
1,704
Reaction score
2,858
Mheshimiwa Rais kuna UPIGAJI MKUBWA unaenda kufanyika hapa, tunakuomba uwe mkali kama Hayati Magufuli ili fedha hizi tulipwe sasa. Walikudanganya kwamba tungelipwa kufikia Septemba 15, hadi leo hii ni SARAKASI tu zinaendelea.

Mheshimiwa Rais tunakuomba ufike Mwanza na kutoa maelekezo, fedha tulizoahidiwa kukopeshwa zilipwe sasa ili nasi tuweze kulipia vizimba vyetu tulivyoagiza. TUSILAZIMISHWE kununua vizimba vyao hawa wababaishaji visivyo na ubora tunaohuitaji, yasije kutokea kama yale ya wakulima kupewa mbegu FAKE na zikashindwa kuota.

Baadhi yetu tuliweka ODA ya vizimba vya kisasa kabisa kutoka kwa wauzaji wa nje ya nchi, hadi sasa tumekwama kuvilipia. Badala yake tunasikia WAPIGA DILI hawa wanatengenezesha vizimba vyao ili tuuziwe hivyo kwa BEI YA JUU (sawa na bajeti yetu ya kuagiza nje ya nchi)- rejea picha za vizimba vya kisasa hapo chini.

Cage System Fish Farming.jpg
 
View attachment 2364067
Mradi wenyewe ndio huu wakuu. Kuna MCHWA wanapigana vikumbo kutaka kutafuna hizo fedha zilizotolewa na Wafadhili (IFAD), kwaajili ya kuendeleza sekta ya uvuvi nchini kwa miaka 5.

Mikopo Vizimba.PNG
 
Nashindwa kuelewa kuhusu hii nchi ni sisi wananchi tunavitabia vya ulalamishi na lawama sana

au ni watumishi wetu wanashida ya vimkono mrefu kila sehemu mmh..?
 
Kaka inasikitisha sana, kuna watu wamekaa ofisini tu wanataka kutajirikia kwenye huu mradi kwa migongo ya wengine.
 
Nashindwa kuelewa kuhusu hii nchi ni sisi wananchi tunavitabia vya ulalamishi na lawama sana

au ni watumishi wetu wanashida ya vimkono mrefu kila sehemu mmh..?
Watu wanapigwa wewe unaita ulalamishi, acha watu waongee wasiposema haya mambo hayataisha na hawatapata haki zao, tena naomba mtumie wabunge wenu na wanasheria ikiwezekana kumaliza hii kitu
 
Wabunge hawasaidii chochote, ni sehemu ya wanufaika wa huu utapeli. Umesahau kwamba walihadaa watu kwamba Rais amemwaga mabilioni kwa vijana ili kufuga samaki, wakati hizo pesa 66,244,723.00 USD zilitolewa na IFAD?
 
Attachments

Rais Samia fukuza Waziri wa Mifugo na Uvuvi pamoja na Mkurugenzi wa TADB, hao ndio vinara wa upigaji kwenye mradi huu. Wanatengeneza mazingira ya kuleta hasara kwenye mradi, wanataka hasara hiyo ibebwe na nani?
Muda wa kufanya tathimini ya awamu ya kwanza ni mwezi Juni 2023, na tangu tumeahidiwa kulipwa hizo pesa hadi sasa ni sarakasi tu zinaendelea.
 
Mama fukuza kazi Waziri wa Mifugo na Uvuvi, wamejipanga kuharibu mradi wa ufugaji samaki kwa kutumia vizimba. Mradi huu unaenda kuwa kama ule wa mtoto wa Mseven kule Uganda. Usije kusema hatukukwambia mapema Mama. @UvuviNa @tadbtz
 
Akichukua kalamu kukata jina la waziri wa Uvuvi basi asisahau jina la waziri wa maji.
Haiwezekani maeneo ya Goba ambayo yalikuwa hayajapata maji wakati wa Magufuli yaendelee na kero za kila siku kuwapokea watu wa maji wanakuja kuhakiki majina na fomu zetu maji hawaleti tunaingia mwaka wa pili sasa.
Kama Dar wanatufanyia hivi vipi huko mikoani?
 
Mama usiwe mzito fanya namna, bado hatujalipwa hizo pesa hadi sasa. Muda unazidi kwenda, hali bado mbaya sana Mama jaribu kuwa msikivu kama hayati
 
Wizara ya mifugo na uvuvi kuna madudu gani? Kwanini mradi huu unapigwa danadana tu hadi mwaka unakaribia kumalizika? Tuambieni ukweli kama pesa zimeliwa na serikali ya CCM.
 
Habari mkuu,hebu elezea kinaga ubaga tuelewe,ilikuaje na umefikia wapi?mmeshalipwa?mmeshaanza kuvuna?
 
Back
Top Bottom