Rais Samia, jiepushe na kauli zinazokufungamanisha na uovu

Bila bila

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2016
Posts
22,168
Reaction score
39,118
Kuita mauaji ni Jambo la kawaida ni kauli inayopaswa kutoka Kwa Mtu asiyejali, sadist anayefuraia kifo cha mwenzake.

Nikushauri mamangu, wengine tulikuamini Sana na mpaka Leo huwa najiuliza Samia wa March 2021 alipotelea wapi?

Kuna watu wanakushauri uongee maneno makali eti kuonyesha huo ndo ukamanda. Lakini asili yako inakufanya ukosee Kila unapotaka kuonyesha udikiteta.

Kuna watu nchi hii wanaishi Kwa kueneza habari za kufurahisha watu. Wengine wamejenga na wanaendesha magari mazuri Kwa kazi hiyo hiyo ya kutoa sifa feki.

Ogopa kusifiwa na kuletewa habari ambayo hata Mtoto wa la 7B ataiona ina mushikeli. Intelijensia ya Polisi iko vizuri Sana, lakini Taarifa nyingi za matamko ya kipolisi dhidi ya Wapinzani wala siyo Taarifa za kiintelijensia.

Ni viongozi wa Polisi Kwa kuwa wasemaji wa chombo hicho wanakaa na kujitungia uzushi na wameanza kukuwin wanakulisha upepo uamini wanakupenda kumbe wanalinnda nafasi zào.

Chukulia Taarifa ya mkutano wa BAVICHA Taifa pale Mbeya kuzuiwa kutokana na Taarifa za kiintelijensia. Huu ulikuwa utunzi wa Kamishna Awadhi na ndo maana hata RPC wa Mbeya alibaki kushangaa ukali wa bosi wake kwenye Jambo linalohitaji mazungumzo.


Pia soma: Rais Samia: Nina taarifa ya kikao chao cha Arusha, wanapanga uhalifu, Serikali ya Tanzania haiondoshwi hivyo
 
Rais Samia shikilia msimamo wako usithubutu Kufuata Kila ushauri. Bora ulosee ila ujumbe ufike
 
 
Kuita mauaji ni Jambo la kawaida ni kauli inayopaswa kutoka Kwa Mtu asiyejali, sadist anayefuraia kifo cha mwenzake.
Unajua nimeitafakari title ya thread yako. Umesema ajiepushe na kauli ambazo zitamfungamanisha na uovu, ukiwa na maana ametoa kauli ambazo zinamfungamanisha na uovu. Sasa swali langu ni kwamba, kama yeye mwenyewe ametoa kauli zinazomfungamanisha na uovu, kwa nini wewe unaona hapaswi kufungamanishwa na uovu?

NI sawa na mimi nikiwa Mwislamu, nitoe kauli inayosifia utamu wa kiti moto, halafu wewe uniambie nijiepushe na kauli ambazo zitafanya nionekane kuwa sehemu ya watu wanaokula kiti moto. Kuna lojiki hapo?
 
Tatizo la Chadema hua ni namna mnavyolichukulia hatua jambo flani...

Mnatoa kauli kama mmekatwa vichwa, reaction zikianza mnaanza kelele...
 
Tumuepushie Rais wetu kupewa taarifa ya uongo na yeyot yule. Hakika wahusika wanajua taarifa wanazotoa ni za uongo ila labda wamezoea. CCM chonde chonde muokoeni Rais kupewa taarifa za uongo.
 
Bongo kila mtu anajua kila kitu. Huyu nae anamshauri raisi
 
Mtu muovu ni muovu tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…