Rais Samia: JWTZ halina mpango wa kuvamia nchi yoyote

Rais Samia: JWTZ halina mpango wa kuvamia nchi yoyote

Heparin

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2021
Posts
242
Reaction score
1,141
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akishiriki Kilele cha Miaka ya 60 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Uwanja wa Uhuru Dar es salaam, leo tarehe 1 Septemba 2024.


View: https://www.youtube.com/live/osYsFlm-yM4?si=1Cpa3zDEHIfIEkcn

"Jeshi letu limeunda na kuuenzi Muungano wetu na mapinduzi yetu matukufu ya Zanzibar, limelinda uhuru Katiba na mipaka ya nchi yetu, ardhini, angani na kwenye maji ikiwemo kuzima matishio makubwa dhidi ya uhuru na umoja wa nchi yetu.” – Rais Samia.

“Jeshi letu limeshiriki na kufanikisha harakati za ukombozi barani Afrika. Jeshi letu sio tu liliyapokea na kuyafundisha majeshi ya vyama vya ukombozi bali pia lilikuwa mstari wa mbele kwenye uwanja wa vita vya ukombozi katika nchi za Msumbiji, Angola, Zimbabwe, Namibia na Afrika Kusini.” - Rais Samia.

"Jeshi letu [JWTZ] limeendelea kuwa ni jeshi la ulinzi na sio jeshi la uvamizi, hatujavamia nchi yoyote na hatuna mpango huo.” – Rais Samia
 
Hotuba nyepesi kabisa. Kwenye sherehe za kijeshi amiri jeshi anatakiwa kutoa hotuba yenye kuchochea morali. Ni kama alikuwa anawahutubia wananchi wakati hotuba ilitakiwa kuwagusa hasa wanajeshi.
 
Siku za usoni jeshi liwe sehemu ya kutengeneza ajira nje ya mipaka nchi za jilani zinahitaji au zina uhitahi wa ulinzi kwenye sehemu nyingi kama migodini na kwenye maofisi ni fursa kwa majeshi yetu kutengeneza ajira
 
Back
Top Bottom