Rais Samia kabambikiwa sakata la Mwanza?

Rais Samia kabambikiwa sakata la Mwanza?

Siku ukitia akili kichwani utaelewa tu!!! Kwa sasa endelea KUDEMKA.

mtu kasema amri imetoka wapi,,, nyie mnakuja mnasema labda karogwa au mara mnahoji mode of delivery ya hiyo amri,huoni hyo ni double standard!kwahiyo watu wengine mnawa-take at their own words kama mwendazake hawa wengine mnaona Wanatania,,come on mkuu 🤣🤣,
 
Mama amefeli sana ! masaa 48 tu kishafeli kwenye miamala na demokrasia , au kalogwa ?
Issue ya Mwanza wamekurupuka.
Hao chadema na kongamano wangebwabwaja nakumaliza,isitoshe hata watu wasingejitokeza wengi.
Sasa Rais amesomeka vibaya kwamba ameanza udikiteta kwa nguvu ya Polisi iliyotumika
 
Wewe kama umetumwa na wenzako ili utuamishe mawazo yetu! Waambie kwa sasa Cyo agenda hiyo. Kawaambie makato hayo ni madogo sana!! Waambie waongezee tuu , ila TZ hatuami.

Matajiri wanaoweka na kutoa pesa benki; wao hawajaguswa na kodi ya uzalendo. Ila masikini wa vishilingi mia mbili vya kina mama zetu ndo vinaenda kukombwa na kuwaambia kuweni wazalendo na nchi yenu.
 
Angalia ZWAZWA hili KAKURUPUKA hata hajui nini kinachoendelea hapa! 😂😂😂😂

Wewe kama umetumwa na wenzako ili utuamishe mawazo yetu! Waambie kwa sasa Cyo agenda hiyo. Kawaambie makato hayo ni madogo sana!! Waambie waongezee tuu , ila TZ hatuami. Matajiri wanaoweka na kutoa pesa benki; wao hawajaguswa na kodi ya uzalendo. Ila masikini wa vishilingi mia mbili vya kina mama zetu ndo vinaenda kukombwa na kuwaambia kuweni wazalendo na nchi yenu.
 
Inasemekana mama kaamua liwalo na liwe kwa vile hana mpango wa kugombea 2025 , hana shida na kura zenu , kwanza hamkuwahi kumchagua kapata kindondokela tu
Unaposema "Inasemekana" una maanisha inasemekania wapi? Na inasemwa na nani? Au ndio mambo ya kuamini hear say?
 
Ila mama si alikuwa Burundi madaraka alikasimu kwa nani? mie naona kachomekewa tu na ndo maana kauli ya kutumwa na Rais inasisitizwa sana
 
JE NI KWELI KAAGIZWA? NI LAZIMA ASEME?

Sakata la CHADEMA na Polisi huko Mwanza lina harufu ya hujuma zifuatazo:

1. Je ni kweli Mh. Rais kaagiza kongamano lizuiwe?

2. Kama kaagiza kwa nini amuagize RPC badala ya IGP?

3. Je ni kweli RPC kasema hadharani kuwa kaagizwa na Rais au kachomekewa maneno na waandishi?

4. Kama ni kweli RPC amesema kuwa katumwa na Rais, kulikuwa na ulazima wa yeye kusema hivyo hadharani? Uwajibikaji wa pamoja uko wapi?

NIONAVYO MIMI:

Uhuru ni kitu pekee kinachotakiwa kulindwa kwa gharama zozote. Kwa hiyo:

1. Wanaokusanyika kupinga katiba mpya wawe huru kama wanaokusanyika kuunga mkono.

2. Vyombo vya ulinzi vilinde katiba visilinde watu, vyama, wala Viongozi.

3. Kuzuia watu kukusanyika ni kuandaa watu kutokusanyika watakapotakiwa kukusanyika. Matumizi ya nguvu ni tabia ya tawala zisizokubalika (Illegitimate). Utawala wetu unakubalika kwa hiyo ujitenge na matumizi ya nguvu.

4. Zipo dalili pevu za njama na hujuma za kufarakanisha utawala huu na wananchi katika sekta nyingi: uchumi, siasa, usalama, na Haki za Binadamu. Adui wa kwanza wa utawala huu si wapinzani, si awamu iliyopita, NI serikali yenyewe inayoelekea kufarakana na kujianika.
Mama asirithi marafiki wala maadui. Atengeneze marafiki na maadui wake.

Lisemwalo LINAWEZA kuwapo. Ondoa miwani utaliona.

Askofu Bagonza
Mimi katiba imenichanganya pale kwenye separation of power.
 
Asanteni sana jeshi la Polisi mnatusaidia sana kuisagia kunguni CCM na Serikali yake,kazi iendelee,mkikuta wapinzani nyie pigeni tu ikibidi ueni kabisaaaaa.
 
Amri IPO kuna kila dalili.
Isipokuwa RPC hakupaswa kusema Rais kaamuru
Rais ni Amiri Jeshi Mkuu
Polisi wanaweza tumia nguvu kubwa kwakuwa RPC ameamriwa na Amiri.
RPC angetisha tu kwa njia zingine.
Hapo sasa uadui mkubwa wawananchi waliokuwa kwenye kongamano ni Rais

..kwanini asiseme ikiwa ni maagizo ya mkuu wa nchi?

..je, raisi akiruhusu mikutano ya hadhara mtashauri polisi / ma-rpc wasiseme?

..kilichonisikitisha mimi ni kitendo cha Raisi kuwapa Polisi maagizo ambayo ni kinyume na sheria na katiba.
 
Nchi huwezi kuiendesha kama unavyolea mtoto..

Wafrika wengi hatujitambui ukimpa uhuru atakushika hadi matakoni hiyo haitoshi atakupaka na mafuta kabisa huku akikutolea maneno ya kebehi, hao ndio wafrika.

Hatujui tunachokihitaji kama taifa, hata hiyo katiba wakipewa bado haitowafaa watanzania wengi.

Katiba na tabia za asili za watanzania ni vitu viwili tofauti kabisa. Hizi ni tabia za mtu mfano wizi, rushwa, tamaa na uchu wa madaraka, kiburi, kutojali muda n.k hapo hata kama unakatiba nzuri bado kutakuwa na matatizo mengi kwenye mfumo wa uongozi na kwa wananchi.

Matatizo yetu kama vile:-
Mfumo wa elimu mbovu
Viongozi hawana miiko ya maadili ya uongozi
Kufanya kazi kwa mazoea
Ubinafsi kupitia udini na ukabila
teknolojia duni
Ujinga
Umasikini wa kifkra( hili ni janga kwa taifa)
Maradhi.
Siasa mbovu.

Ushauri wangu
× Bado tuna katiba nzuri japo sio bora sana ya kusifia, tatizo lipo kwa tabia za watu ambao hawafit kwenye hii katiba, hivyo basi tubadili tabia na mienendo yetu kwa viongozi na wanachi kwa pamoja.
Nakubaliana na wewe kuhusu tabia mbaya ila kunahitajika katiba inayowapa uwezo wananchi kuwadhibiti viongozi wenye hizo tabia mbaya.
Hii katiba iliyopo inawapa nguvu viongozi kutumia tabia zao mbaya kuwatesa wananchi.
 
Kama kabambikiwa ni nani mhusika!? Ni mtu mmoja au kikundi cha watu? Kama hakuzia hilo Kongamano la Katiba mpya je atasema hadharani kwamba yeye hahusiki na hilo zuio!?
Mama akikubali kuchezewa namna hiyo atakuwa kajimaliza mwenyewe. Huwezi kucheka na nyani shambani kwako kiasi hicho.
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Nchi huwezi kuiendesha kama unavyolea mtoto..

Wafrika wengi hatujitambui ukimpa uhuru atakushika hadi matakoni hiyo haitoshi atakupaka na mafuta kabisa huku akikutolea maneno ya kebehi, hao ndio wafrika.

Hatujui tunachokihitaji kama taifa, hata hiyo katiba wakipewa bado haitowafaa watanzania wengi.

Katiba na tabia za asili za watanzania ni vitu viwili tofauti kabisa. Hizi ni tabia za mtu mfano wizi, rushwa, tamaa na uchu wa madaraka, kiburi, kutojali muda n.k hapo hata kama unakatiba nzuri bado kutakuwa na matatizo mengi kwenye mfumo wa uongozi na kwa wananchi.

Matatizo yetu kama vile:-
Mfumo wa elimu mbovu
Viongozi hawana miiko ya maadili ya uongozi
Kufanya kazi kwa mazoea
Ubinafsi kupitia udini na ukabila
teknolojia duni
Ujinga
Umasikini wa kifkra( hili ni janga kwa taifa)
Maradhi.
Siasa mbovu.

Ushauri wangu
× Bado tuna katiba nzuri japo sio bora sana ya kusifia, tatizo lipo kwa tabia za watu ambao hawafit kwenye hii katiba, hivyo basi tubadili tabia na mienendo yetu kwa viongozi na wanachi kwa pamoja.
Kuwa na KATIBA imara na yenye msimamo kama MSUMENO wa kula mbele na nyuma (kwa watawala na watawaliwa)

KATIBA itakayo elekeza cha kufanya na kuadhibu kila upande(watawala na watawaliwa)

KATIBA itamke wazi kuwa "Mtu yeyote (mtawala na mtawaliwa) atakaye tenda tofauti na MATAKWA YAKE adhabu yake ni KIFUNGO GEREZANI KWA MUDA UTAKAOWEKWA KWA MUJIBU WA KATIBA.
 
Nilikwambia siku ukitia akili kichwani utaelewa. Endelea KUDEMKA.

mtu kasema amri imetoka wapi,,, nyie mnakuja mnasema labda karogwa au mara mnahoji mode of delivery ya hiyo amri,huoni hyo ni double standard!kwahiyo watu wengine mnawa-take at their own words kama mwendazake hawa wengine mnaona Wanatania,,come on mkuu 🤣🤣,
 
Kama kabambikiwa ni nani mhusika!? Ni mtu mmoja au kikundi cha watu? Kama hakuzia hilo Kongamano la Katiba mpya je atasema hadharani kwamba yeye hahusiki na hilo zuio!?
Remote control ya bwagamoyo
Mhusika yupo yupo tu
Wanamchezea faulu ye mwenyewe kutwa kuzunguluka
Ni swala la muda akiamka atakuta walafi wamegawana
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Back
Top Bottom