Rais Samia kabambikiwa sakata la Mwanza?

Siku ukitia akili kichwani utaelewa tu!!! Kwa sasa endelea KUDEMKA.

 
Mama amefeli sana ! masaa 48 tu kishafeli kwenye miamala na demokrasia , au kalogwa ?
Issue ya Mwanza wamekurupuka.
Hao chadema na kongamano wangebwabwaja nakumaliza,isitoshe hata watu wasingejitokeza wengi.
Sasa Rais amesomeka vibaya kwamba ameanza udikiteta kwa nguvu ya Polisi iliyotumika
 
Wewe kama umetumwa na wenzako ili utuamishe mawazo yetu! Waambie kwa sasa Cyo agenda hiyo. Kawaambie makato hayo ni madogo sana!! Waambie waongezee tuu , ila TZ hatuami.

Matajiri wanaoweka na kutoa pesa benki; wao hawajaguswa na kodi ya uzalendo. Ila masikini wa vishilingi mia mbili vya kina mama zetu ndo vinaenda kukombwa na kuwaambia kuweni wazalendo na nchi yenu.
 
Angalia ZWAZWA hili KAKURUPUKA hata hajui nini kinachoendelea hapa! 😂😂😂😂

 
Inasemekana mama kaamua liwalo na liwe kwa vile hana mpango wa kugombea 2025 , hana shida na kura zenu , kwanza hamkuwahi kumchagua kapata kindondokela tu
Unaposema "Inasemekana" una maanisha inasemekania wapi? Na inasemwa na nani? Au ndio mambo ya kuamini hear say?
 
Ila mama si alikuwa Burundi madaraka alikasimu kwa nani? mie naona kachomekewa tu na ndo maana kauli ya kutumwa na Rais inasisitizwa sana
 
Mimi katiba imenichanganya pale kwenye separation of power.
 
Asanteni sana jeshi la Polisi mnatusaidia sana kuisagia kunguni CCM na Serikali yake,kazi iendelee,mkikuta wapinzani nyie pigeni tu ikibidi ueni kabisaaaaa.
 

..kwanini asiseme ikiwa ni maagizo ya mkuu wa nchi?

..je, raisi akiruhusu mikutano ya hadhara mtashauri polisi / ma-rpc wasiseme?

..kilichonisikitisha mimi ni kitendo cha Raisi kuwapa Polisi maagizo ambayo ni kinyume na sheria na katiba.
 
Nakubaliana na wewe kuhusu tabia mbaya ila kunahitajika katiba inayowapa uwezo wananchi kuwadhibiti viongozi wenye hizo tabia mbaya.
Hii katiba iliyopo inawapa nguvu viongozi kutumia tabia zao mbaya kuwatesa wananchi.
 
Kama kabambikiwa ni nani mhusika!? Ni mtu mmoja au kikundi cha watu? Kama hakuzia hilo Kongamano la Katiba mpya je atasema hadharani kwamba yeye hahusiki na hilo zuio!?
Mama akikubali kuchezewa namna hiyo atakuwa kajimaliza mwenyewe. Huwezi kucheka na nyani shambani kwako kiasi hicho.
 
Reactions: BAK
Kuwa na KATIBA imara na yenye msimamo kama MSUMENO wa kula mbele na nyuma (kwa watawala na watawaliwa)

KATIBA itakayo elekeza cha kufanya na kuadhibu kila upande(watawala na watawaliwa)

KATIBA itamke wazi kuwa "Mtu yeyote (mtawala na mtawaliwa) atakaye tenda tofauti na MATAKWA YAKE adhabu yake ni KIFUNGO GEREZANI KWA MUDA UTAKAOWEKWA KWA MUJIBU WA KATIBA.
 


Nilikwambia siku ukitia akili kichwani utaelewa. Endelea KUDEMKA.

 
Kama kabambikiwa ni nani mhusika!? Ni mtu mmoja au kikundi cha watu? Kama hakuzia hilo Kongamano la Katiba mpya je atasema hadharani kwamba yeye hahusiki na hilo zuio!?
Remote control ya bwagamoyo
Mhusika yupo yupo tu
Wanamchezea faulu ye mwenyewe kutwa kuzunguluka
Ni swala la muda akiamka atakuta walafi wamegawana
 
Reactions: BAK
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…