Rais Samia kabambikiwa sakata la Mwanza?

Hivi inakuwaje Rais wa nchi afanye kazi na RPC badala ya IGP ?
Hapa inakua hivi, Rais anampa maagizo IGP, IGP naye anampa maagizo RPC..kwasababu RPC ndiye muwakilishi wa IGP kwenye mkoa husika. Kwahiyo 'origin' ya amri ni kutoka kwa Mh. Rais, IGP ni mtu wa katikati tu.
 
That’s a million dollar question Mkuu, Tusitegemee jibu kutoka Serikali hii haramu.
Labda nijaribu kutoa ufafanuzi. Hapa ni kwamba Rais anampa maagizo IGP, IGP naye anampa maagizo RPC kwasababu RPC ndiye muwakilishi wa IGP kwenye mkoa husika. Kwahiyo 'origin' ya amri ni kutoka kwa Mh. Rais.
 
Soma kauli mbili za RPC Mwanza ambazo ZINAPINGANA
Kauli ya kwamba ni amri kutoka Rais
Kauli ya pili ni Chadema haikuomba kibali.
Bila ya shaka huyo RPC kama ilivyokuwa kawaida ya polisiccm anasema uongo katika kauli moja au zote mbili na Katiba ya nchi haisemi chama cha upinzani chochote nchini hakiwezi kufanya shughuli zake bila kibali cha polisiccm huo ni udikteta uliokuwa created na maccm.

Labda nijaribu kutoa ufafanuzi. Hapa ni kwamba Rais anampa maagizo IGP, IGP naye anampa maagizo RPC kwasababu RPC ndiye muwakilishi wa IGP kwenye mkoa husika. Kwahiyo 'origin' ya amri ni kutoka kwa Mh. Rais.
 
Mkuu, huko kwenye udikteta mimi sipo [emoji3]

Kimsingi mimi niliji-confine kwenye kung'amua swali kwamba "ni kwanini Rais afanye kazi na RPC badala ya IGP?".
 
FYI RPC hawezi kusema ni maagizo kapewa na Rais kama maagizo alipewa na IGP.

Mkuu, huko kwenye udikteta mimi sipo [emoji3]

Kimsingi mimi niliji-confine kwenye kung'amua swali kwamba "ni kwanini Rais afanye kazi na RPC badala ya IGP?".
 
Kuna vita kali kati ya Timu Bwagamoyo na timu chato kila moja ikitaka kumdhibiti samia bila kujali maslahi ya Nchi yetu.

Remote control ya bwagamoyo
Mhusika yupo yupo tu
Wanamchezea faulu ye mwenyewe kutwa kuzunguluka
Ni swala la muda akiamka atakuta walafi wamegawana
 
Reactions: BAK
RPC-Mwanza, SACP Ramadhan Ngh'anzi anasema John Heche na Peer Msigwa kuwa walipaswa kutoa taarifa kwake kuwa wanaingia Mwanza na watafanya shughuli zao hapo. RPC hajui lolote kuhusu "uhuru wa mtu kwenda atakako" (ib.17) katiba ya JMT, sheria ya 1984, Na. 15?
 
Kama hili linaukweli,amelichuma kwa mikono yake.
Alipoingia madarakani watu tulishaumu avunje baraza la waziri na kufumua mtandao was mtangulizi wake hakuelewa.
Sasa ataelewa lakini kishachelewa
 
"Huyu naye ameokotwa wapi? -- Nyerere (rip).
 
Muraaaa kodi muraaaaa
 
Kama hili linaukweli,amelichuma kwa mikono yake.
Alipoingia madarakani watu tulishaumu avunje baraza la waziri na kufumua mtandao was mtangulizi wake hakuelewa.
Sasa ataelewa lakini kishachelewa
Chelewa ufike. Kama angali ana nia njema na afike sasa. Tutakuwapo kumwuunga mkono.
 
Kwa yanayoendelea ndani ya taifa,hivi sasa na weza kusema zile mia za kwanza zilikuwa ni hadaa, iliyokuwa na malengo yenye manufaa kwa wachache kama ilivyo ada kwa wanasiasa.
 
Reactions: BAK
Huyo RPC Ni mpumbavu,kongamano la Dar mbona mama hakuzuia aje azuie la mwanza? Hao wanajituma wenyewe Kisha wanamsingizia mama.yaani mama kamtoa mdude,aje azuie kongamano.mnapokuwa na polisi wa aina hii ndiyo madhara yake.
 
FYI RPC hawezi kusema ni maagizo kapewa na Rais kama maagizo alipewa na IGP.
Hawezi??!

Mkuu, common sense ina-suggest kwamba ni busara kutoku-arrive kwenye conclusion mapema namna hiyo.

Mimi na wewe tunafanya 'hypothesis formulation' tu, ukianza kusema HAWEZI ni sawa na kutaka kusema na wewe ulikuwepo wakati wanapeana maagizo.

Unasahau kwamba kuna kipindi Muroto alikua anavaa 'jungle uniform' halafu chini anavaa viatu vya kawaida vya kipolisi (police shoes) badala ya chini kuvaa yale mabuti (sijui yanaitwaje kitaalamu), IGP akampiga biti, hapa kuna mawili, inawezekana Muroto alikua hajui kupangilia sare za jeshi la polisi au huenda zilikuwa ni ghiliba za nyani mzee.

Sasa tuje kwenye the present scenario, Yamkini baada ya IGP kumwambia RPC kwamba order imetoka kwa Rais, inawezekana RPC hakujua kwamba hakupaswa kumtaja Rais au alipewa maelekezo na IGP kwamba amtaje Rais. Usiseme HAWEZI.

J2 njema mkuu.
 
Zipo dalili pevu za njama na hujuma za kufarakanisha utawala huu na wananchi katika sekta nyingi: uchumi, siasa, usalama, na Haki za Binadamu. Adui wa kwanza wa utawala huu si wapinzani, si awamu iliyopita, NI serikali yenyewe inayoelekea kufarakana na kujianika.
Mama asirithi marafiki wala maadui. Atengeneze marafiki na maadui wake.

Hili ni kubwa sana,na wakina Mwigulu ndo wanatumia karata hizi kumchonganisha mama na wananchi.

Mama shkamoo, mama Samia yakatae haya.
 
Tuna wapinzani wa hovyo sana.

Yaani wanapambania mikutano ya kisiasa Karne hii ya 21??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…