Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,362
- 48,879
KWenye jambo hili la utekaji na mauaji halijaanza na ndugu Yetu Ali Kibao. Limekuwepo kwa muda sasa huku likilindwa na baadhi ya watu wente namlaka.
Kama kweli Rais unataka kuwapata wahusika kamili na kujua nafasi zao kwenye huu ushetani, ungetoa maelekezo wafuatao wakamatwe mara moja:
1) Waziri wa Mambo ya ndani, bwana Masauni. Huyu na IGP, ndio wakati wote wamekuwa wakikuficha kuwa hakuna utekaji wala mauaji. Na wewe ukawaamini, hata ukafikia kutoa kauli tata kuwa utekaji na mauaji yanayolalamikiwa na wananchi ni drama. Jiulize kwa nini wamekuwa wakiyaficha matendo haya ya kinyama na kudai kuwa hayapo wakati yapo?
2) IGP Wambura. Naye kama ilivyo kwa Waziri wa mambo ya ndani, kwa nini wamekuwa wakificha utekaji na mauaji, na kudai kuwa mambo hayo hayapo. Hii ina maana wamekuwa wakiyalinda matendo haya ya kishetani, bila shaka wakitaka yaendelee.
3) Spika wa Bunge Tulia. Huyu alifikia kufuta hoja iliyoletwa na mwakilishi wa wananchi, na kuzuia Bunge lisijadili utekaji na mauaji yanayofanywa kwa wadau wa siasa. Yeye akasema hakuna utekaji wala mauaji, bali ni hisia tu. Bila shaka anawajua aliokuwa anawalinda.
4) Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Kagera. Huyu alisema kuwa kama endapo kuna wakosoaji wa viongozi watapotea, jeshi la polisi lisiwatafute. Huyi, lazima atakuwa anajua hao wakosoaji huwa wanawapoteza namna gani, na wanawapotezea wapi. Atakuwa anajua, huwa anashirikiana na nani kuwapoteza hao wakosoaji.
5) Mkuu wa Task Force, bwana Mafwele. Baadhi ya waliowahi kutekwa na kunusurika kifo, wameeleza wazi kuwa walipotekwa walipelekwa kwenye mabanda ya mbao yaliyo nyuma ya ofisi za Task Force, ambako waliteswa sana kabla ya kusafirishwa. Na hivi karibuni, mabanda hayo wameyabomoa.
5) Mkuu wa Kituo cha Polisi Oysterbay. Huko ndiko Sativa alifichwa na kuteswa kabla ya kwenda kutupwa hifadhi ya wanyama ya Katavi. Bila shaka, huyu anajua ni watu gani huwa wanawapeleka watu waliotekwa kwenye kituo chake.
Hawa ni suspects wa wazi na muhimu kabisa ambako uchunguzi ungeanzia. Japo yawezekana hawahusiki moja kwa moja, lakini bila shaka wanawafahamu na wapo karibu na watekelezaji wa huu ushetani.