Rais Samia kamaliza kabisa leo Mwanza, ameahidi kutoa kipaumbele kwa vijana

Philipo Mwakibinga

Senior Member
Joined
May 13, 2013
Posts
110
Reaction score
175
VIJANA TUKISHINDWA KUFANIKIWA KATIKA KIPINDI HIKI CHA MATENDO YA MAONO HAYA YA MH RAIS MAMA SAMIA, BASI TENA.

Na: Philipo Mwakibinga.

Leo nimepata bahati ya kuudhuria Kongamano la Mh Rais wa JMT na Vijana wa Tanzania kupitia Vijana wa Wakanda ya Ziwa lililofanyika katika uwanja wa Nyamagana katika Jiji la Mwanza. Niliyoyashuhudia na kuyasikia yamenifanya niione Tanzania ya aina yake na hapa nitaweka kumbukumbu sahihi.

Kongamano hili limekua la kihistoria katika Taifa letu. Sijui kwa Watanzania wenzetu wa miaka ya 60 na 70 kama wamewahikuwa na hili jambo lakini mimi wa miaka ya 80-90 nasema haijawahi kutokea. Kongamano lilifana na halikuchosha wala kukera, vijana bila kujali Itikadi zao na maeneo yao watokayo wote walikuwa ni Watanzania wenye Utanzania wao.

Rais Mama Samia anamaono ya mbali sana na Taifa hili jamani tuache masihara. Kwanza kaonesha kukerwa na maisha yetu ya kisiasa yasiyojali Nchi bali yamejikita kwenye malalamiko na tuhuma pasipokutoa masuluhisho.

Rais, ameonesha nia ya kweli na yadhati juu ya uwepo wa BARAZA LA VIJANA TANZANIA. Jambo ambalo limekua ni kiu ya Vijana kwa muda mrefu sana katika taifa letu. Rais kenda mbali na kuhoji juu ya mahali tunapokutana na kujadili mambo ya ki-nchi mbali na kwenye vyama vyetu vya saiasa. Pia katupa changamoto ya kutojitendea haki katika vyama vyetu hasa pale tunapotumia muda mwingi kutokuisaidia serikali badala yake tumekua watu wa lawama tu na tuhuma zisizomwisho.

Rais ameonesha maono ya namna vijana tunavyoweza kufanikiwa kimaisha kupitia fulsa mbalimbali zilizopo na zinazoendelea kuongezwa katika taifa letu. Mfano kilimo, kwamba siyo lazima wote tulime mwingine anaweza kuwa muuza pembejeo na meingine akawa mnunua mazao lakini sote tukawa Wakulima pamoja na yule aliyelima shambani. Huu ndiyo uongozi maana kiongozi anaonesha njia watu anaowaongoza.

Rais kaweka wazi kwa, vijana kuamini katika chama ambacho mtu atakaua na mapenzi nacho lakini isiwe ndiyo sababu ya kushindwa kujikita katika masuala ya msingi yenye manufaa kwa Taifa na maisha ya familia kwa ujumla. Ameonesha namna vijana wanavyojikita kwenye mabishano tu na itikadi zisizo na tija kwa Taifa. Rais kaenda mbali zaidi na kuwakumbusha UVCCM kutokana na ukongwe wao na ukubwa kuwa chachu na mfano ili wengine wafuate katika vyama vingine.

Rais kaonesha kwa dhati kuendelea kuwa na imani na vijana. Pamoja na changamoto zenyekukatisha tamaa kwabaadhi ya vijana wengine waliowahi kuaminiwa bado Mh Rais ameendelea kuahidi kuwaamini vijana kwenye nafasi mbalimbali katika Serikali na hasa kupitia Mikeka ya MaDC, na MaDed inayotarajiwa kuwa wazi siku chache zijazo.

Wamachinga kutodumaa. Hili nalolimekua jambo kubwa alilolisema Rais juu ya Machinga kuendelea kuwa watumwa wa wengine badalayake nao wawe wafanyabiashara wakubwa kwa kuchangamkia fulsa mbalimbali zinazotolewa na Serikali hii ya awamu ya 6. Katika hili Mh Rais kutokana mapenzi yake kwa wafanyabiashara wadogowadogo na hari yake ya kutopenda uonevu, unyanyasaji na ukandamizaji amewatumbua baadhi ya viongozi walioonekana kutendae ndivyosivyo baadhi ya Machinga katika mkoa wa Morogoro.

Haya na Mengine Mengi ambayo yanagusa Watanzania wote husasani vijana wa mijini na vijijini, wasomi na wasiowasomi, wasanii na wasiowasanii yamewekwa wazi leo. Nidhahiri kuwa Tanzania inaenda kupiga hatua nyingine kubwa zaidi katika maendeleo ya kiuchumi, kisasa na kijamii.

Nitoe wito kwa vijana wote wa Tanzania kuwa, undani na ukweli kuwa maendeleo hayana chama kaonesha Mh Rais mama Samia, hivyo ni jambo la maana sana kuelewa falsafa yake na kuiunga mkono kwa dhati kwani Tanzania tunaenda kuwa Taifa kubwa zaidi ya wengine.

Nawasalimu kwa Jina la Jamuhuri ya Muungano.
Nawasalimu kwa Jina la JMT.
 
Naona mkuu unaufukuzia mkeka wa maDC na maDED bila kusahau mkeka wa maDAS ila sasa mikeka yako ikichanika usije kuwa mkosoaji tena[emoji41]
 
Wenye akili muueleweni vizuri mama. Alishindwa kuwataja jina tu uvccm, kua acheni ujinga wa kujifanya kuwa Tz Ni ya ccm tu
Acheni upumbavu wa kutisha watu na kuteka watu, acheni ujinga wa akina hapi kutisha wazee wastaafu nk. Wenye akili tumemuelewa Mh rais.
 
VIJANA TUKISHINDWA KUFANIKIWA KATIKA KIPINDI HIKI CHA MATENDO YA MAONO HAYA YA MH RAIS MAMA SAMIA, BASI TENA.

Na: Philipo Mwakibinga.

Leo nimepata bahati ya kuudhuria Kongamano la Mh Rais wa JMT na Vijana wa Tanzania kupitia Vijana wa Wakanda ya Ziwa lililofanyika katika uwanja wa Nyamagana katika Jiji la Mwanza. Niliyoyashuhudia na kuyasikia yamenifanya niione Tanzania ya aina yake na hapa nitaweka kumbukumbu sahihi.

Kongamano hili limekua la kihistoria katika Taifa letu. Sijui kwa Watanzania wenzetu wa miaka ya 60 na 70 kama wamewahikuwa na hili jambo lakini mimi wa miaka ya 80-90 nasema haijawahi kutokea. Kongamano lilifana na halikuchosha wala kukera, vijana bila kujali Itikadi zao na maeneo yao watokayo wote walikuwa ni Watanzania wenye Utanzania wao.

Rais Mama Samia anamaono ya mbali sana na Taifa hili jamani tuache masihara. Kwanza kaonesha kukerwa na maisha yetu ya kisiasa yasiyojali Nchi bali yamejikita kwenye malalamiko na tuhuma pasipokutoa masuluhisho.

Rais, ameonesha nia ya kweli na yadhati juu ya uwepo wa BARAZA LA VIJANA TANZANIA. Jambo ambalo limekua ni kiu ya Vijana kwa muda mrefu sana katika taifa letu. Rais kenda mbali na kuhoji juu ya mahali tunapokutana na kujadili mambo ya ki-nchi mbali na kwenye vyama vyetu vya saiasa. Pia katupa changamoto ya kutojitendea haki katika vyama vyetu hasa pale tunapotumia muda mwingi kutokuisaidia serikali badala yake tumekua watu wa lawama tu na tuhuma zisizomwisho.

Rais ameonesha maono ya namna vijana tunavyoweza kufanikiwa kimaisha kupitia fulsa mbalimbali zilizopo na zinazoendelea kuongezwa katika taifa letu. Mfano kilimo, kwamba siyo lazima wote tulime mwingine anaweza kuwa muuza pembejeo na meingine akawa mnunua mazao lakini sote tukawa Wakulima pamoja na yule aliyelima shambani. Huu ndiyo uongozi maana kiongozi anaonesha njia watu anaowaongoza.

Rais kaweka wazi kwa, vijana kuamini katika chama ambacho mtu atakaua na mapenzi nacho lakini isiwe ndiyo sababu ya kushindwa kujikita katika masuala ya msingi yenye manufaa kwa Taifa na maisha ya familia kwa ujumla. Ameonesha namna vijana wanavyojikita kwenye mabishano tu na itikadi zisizo na tija kwa Taifa. Rais kaenda mbali zaidi na kuwakumbusha UVCCM kutokana na ukongwe wao na ukubwa kuwa chachu na mfano ili wengine wafuate katika vyama vingine.

Rais kaonesha kwa dhati kuendelea kuwa na imani na vijana. Pamoja na changamoto zenyekukatisha tamaa kwabaadhi ya vijana wengine waliowahi kuaminiwa bado Mh Rais ameendelea kuahidi kuwaamini vijana kwenye nafasi mbalimbali katika Serikali na hasa kupitia Mikeka ya MaDC, na MaDed inayotarajiwa kuwa wazi siku chache zijazo.

Wamachinga kutodumaa. Hili nalolimekua jambo kubwa alilolisema Rais juu ya Machinga kuendelea kuwa watumwa wa wengine badalayake nao wawe wafanyabiashara wakubwa kwa kuchangamkia fulsa mbalimbali zinazotolewa na Serikali hii ya awamu ya 6. Katika hili Mh Rais kutokana mapenzi yake kwa wafanyabiashara wadogowadogo na hari yake ya kutopenda uonevu, unyanyasaji na ukandamizaji amewatumbua baadhi ya viongozi walioonekana kutendae ndivyosivyo baadhi ya Machinga katika mkoa wa Morogoro.

Haya na Mengine Mengi ambayo yanagusa Watanzania wote husasani vijana wa mijini na vijijini, wasomi na wasiowasomi, wasanii na wasiowasanii yamewekwa wazi leo. Nidhahiri kuwa Tanzania inaenda kupiga hatua nyingine kubwa zaidi katika maendeleo ya kiuchumi, kisasa na kijamii.

Nitoe wito kwa vijana wote wa Tanzania kuwa, undani na ukweli kuwa maendeleo hayana chama kaonesha Mh Rais mama Samia, hivyo ni jambo la maana sana kuelewa falsafa yake na kuiunga mkono kwa dhati kwani Tanzania tunaenda kuwa Taifa kubwa zaidi ya wengine.
Nawasalimu kwa Jina la Jamuhuri ya Muungano.
Nawasalimu kwa Jina la JMT...
Kuna tofauti Kubwa sana kati ya Rais Kusoma ( Theoretically ) alichoandikiwa na Wasaidizi wake waliokomaa kwa Uwongo wa Kufanana na Ukweli ( Propaganda ) na kuwa Mtendaji na Mtekelezaji Kivitendo ( Pragmatically ) katika yale aliyoyahutubia na Kuyasisitiza.

Siasa za Afrika zimejaa tu Uwongo, Unafiki na Kuwafanya unaowaongoza kuwa ni Mangumbaru ( Wajinga ) ambapo Mifano hii ipo mingi tu. Mwanasiasa pekee ninayemuamini na Kumkubali ni wa Kizungu tu pekee kwani wayafanyayo yanaonekana ' vividly ' nchini mwao ( Kwao )
 
Vijana sasa ni kazi kwenu kupambana na maisha ili kugombania fursa zitakazotokea na hata kuridhika na matokeo yatakayokuja. Msisite kuwapongeza wale wachache watakaobahatika kuzipata.

Kitakwimu ndani ya kundi lenu mpo wengi sana na kwa hakika nafasi za ajira zilizopo ni chache mno. Teuzi na ajira mpya zikianza kumwagika kwa upande wenu msianze tena kutoa vilio upya bali mtoe pingezi kwa wachache watakaozipata.

Ndani ya kundi lenu kuna "clusters" za umri tofauti ijapokuwa wote mnahesabika kama ni vijana. Miaka yote iliyopo kati ya 18 mpaka 35 ina jumuisha vijana tofauti wenye wasifu tofauti katika umri, jinsi, elimu, utaalamu, ujuzi, stadi & stadi za kazi pamoja na uzoefu wa kazi mbalimbali.

Lazima mtambue miongoni mwenu wapo wachache mno ambao ndiyo watakaokidhi vigezo vyote muhimu vya ajira serikalini. Tusije tena kuanza kuwasikia baadhi yenu wakianza tena malalamiko mapya kuhusu eti baadhi yenu kupendelewa kutokana na sababu za udini, jinsia, ukaribu na viongozi waandamizi, itikadi, elimu, u Tanganyika ama u Zanzibar, ukabila, ukanda na mengine kama hayo.
 
Tatizo kuna wazee wana roho mbaya sana!
yaaani hata hao vijana wachache walio pata nafasi ktk serikali bado wazee wazima wenye roho ya korosho wana waharibia vijana wasisonge mbele, badala ya kuwa rekebisha pale wanapo teleza basi wanapata sababu ya kuwaangamiza kabisa.
Tunamuomba Rais aielewe kuwa kuna viongozi wazee wana waharibia kazi vijana, badala ya kuwajenga wana waharibia kazi na kuonekana hawafai...kumbe sivyo.
baadhi ya viongozi wazee wana roho mbaya kama wanyama.
 
Back
Top Bottom