Kesho kunani
Member
- Sep 10, 2023
- 72
- 191
Samia kaniponza! Ilibaki kidogo niache unga.
Leo baada ya kutoka church niliamua kwenda sokoni kununua mahitaji ya home, nikiwa sokoni katika story za hapa na pale wamama wauza nyanya wakaanza kulalamika ugumu wa maisha na kumtupia lawama Samia.
" Yaani kila kitu anapeleka kwao Zanzibar,na kazi za maana zote anawapa wazanzibar.. huyu mwanamke hatujali kabisaaa.. na tusipokuwa makini atauza kila kitu.." aliongea mama aliyekuwa ananiuzia nyanya.
Licha ya kutokubaliana na Samia kwa Mambo mengi lakini kauli hii sikuiona Kama sahihi, hivyo Bila kusita nilianza kumtetea.
" Haipo hivyo Mama zangu.. unajua Samia anania nzuri ila......."
Paaaaaa... Kabla sijamaliza kuongea nilipigwa konde la ajabu Sana, mpaka Sasa sielewi Kama yule mama alinipiga na mkono wake au alitumia tofali.
Muda huu nipo home,japo masikio Hadi Sasa hayasikii vizuriii kutokana na lile konde.
Upande mmoja wa nafsi unaniambia nikakichafue, lakini kila nikikumbuka lile konde miguu inakosa nguvu kabisaaa.
Samia umeniponza, Kama upo humu na unasoma hili mtume chawa wako afanye muamala chap nikatulize haya maumivu la chaz.
Kesho kunani
Kwasasa Songea, Majengo Mnadani.