Rais Samia kanyaga twende

Wimbo

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2012
Posts
866
Reaction score
625
Mama wa Taifa Samia, mambo mengine ni ya kuziba sikio maadamu unajua ni wapi unataka twende.
Mzee wako Mwinyi alipotutoa katika kongwa la uchumi wa chungu kimoja akatuletea uchumi huria tulipiga kelele hakuna mfano, najiuliza leo tungelikuwa bado huko tungekuweje,?

Mkapa akapokea kijiti na kugundua kwamba mashirika mengi ya umma yalikuwa ni mzigo mzito mno kwa serikali akayabinafsisha, kelele zilizopigwa hazina mfano.

Kikwete akadaka kijiti akaelekeza nguvu kwenye miundombinu na kuifungua Nchi kwenye Dunia ya diplomasia na kila mtz aweze kuchangia katika kukwamua hali yake na hatimaye Nchi kwa ujumla watu bado walipiga kelele. akaingia Chuma, yeye hakutaka hata kusikiliza mtu, akafanya yale aliyoona yanatufaa na kweli mziki wake tuliuona na histolia yake japo hatujaiandika na bahati mbaya aliondoka bila kuandika kitabu chake lakini aliyoyasimamia yana kumbukumbu ya ya 100years + vizazi vijavyo vitamuandika sana.

Risk avers always inamfaya mtu anayetaka kujikomboa achelewe shauri ya woga, Risk taker mara nyingi anatoboa, Mama WA TAIFA SAMIA Usiogope kuchukua risk, the higher the Risk the higher the return. kama kuna anayetaka kukuzingua thibitisha yale maneno yako.

(Ukinizingua nitakuzingua)
 
Ujumbe ni wake, sisi inatuhusu nini hata paragraph zinakushinda
 
Bandari za za bara zote nimali ya watanganyika. Tunahitaji bandari zetu.
 
Mtu akupeleke utumwani Dubai halafu unamwambia kanyaga twende..

Huu ni mtindio wa ubongo.
 
Sawa akanyage twende ila asiuze bandari
 
Unamdanganya. Kuna watu wachache wanamdanganya kwa makusudi ili wanufaike wao. Msimuingize Rais kwenye wakati mgumu kwa kuendekeza njaa zenu.
Kuna mahali lazima kuangalia wananchi wanataka nini. Nchi hii tuwe wote na mapenzi ya kweli. Tukianza kudanganyana, tutaiharibu wenyewe. Maana uongo haujawahi kumsitiri mtu.
Tumuunge mkono. Lakini tusimdanganye maana itakuwa tunamkosea haki na heshima
 
Bandari za za bara zote nimali ya watanganyika. Tunahitaji bandari zetu.
Umechelewa jamvini karamu imeshaliwa.

Unafahamu kuwa ndani ya miezi mitatu ya ya DP World kuanza kwa utafiti wao tu banfmdari inashusha mizigo mingi na kwa haraka kuliko wakati wowote, hiyo ni bashraf tu, bado mziki kamili haujaanza.
 
Umechelewa jamvini karamu imeshaliwa.

Unafahamu kuwa ndani ya miezi mitatu ya ya DP World kuanza kwa utafiti wao tu banfmdari inashusha mizigo mingi na kwa haraka kuliko wakati wowote, hiyo ni bashraf tu, bado mziki kamili haujaanza.
Mkataba ni wamuda gani?.
 
Sawa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…