Rais Samia kapata wapi ujasiri wa kusafiri ilhali kuna majanga nchini?

Rais Samia kapata wapi ujasiri wa kusafiri ilhali kuna majanga nchini?

1. Mmiliki wa Jengo yupo wapi?
NANI NI MMILIKI WAJENGO.
2. Ramani za jengo ziko wapi??
Uokozi bila Ramani.

3. Ghorofa nne watu wanaokolewa siku nne na sio moja. TAIFA LIMEOZA.

4. Selikali ipo Radhi kununua Mabomu, magali ya Jeshi nk kuizuia CHADEMA na Inashindwa KUNUNUA VIFAA VYA UOKOAJI kwa Raia wake.

5. Niffer amejipeleka Kituoni, Yuko wapi mmliki wa Jengo.

6. Je ni nani aliyetoa vibali vya kujenga na kubomoa anakamatwa Niffer.
TANZANIA YANGU MASIKINI

ZIMA MOTO NA UOKOAJI NI SAWA NA HAKUNA KITU ZERO KABISA.
JESHI LIVUNJWE HARAKA

MAJENGO MENGI KARIAKOO YAMEOZA
 
Janga la maafa Kariakoo limekuja na mengi
Yapo mazuri
Yapo mabaya
Yapo ya kuhuzunisha sana
Yapo ya kusikitisha na kutia simanzi
Yapo ya kuumiza hisia na mioyo
Yapo ya kuchekesha katikati ya huzuni kubwa
Yapo ya kushangaza sana
Yapo ya kufikirisha na yapo yanayozua sintofahamu na mijadala mingi
Mimi nimeliona hili.. Ambalo ni kama kijembe ama dongo kwa mtu asiyetajwa waziwazi.. Ni jiwe gizani
Huko mitandaoni wamejitokeza wanawake wakijirekodi video fupifupi za kejeli kwa wanawake wenzao wanaojisifu kuwa wanawake wanaweza. Wanawake ni jeshi imara.. Wanawake wamefanya makubwa..nknk
Wanauliza mbona kwenye shughuli za uokozi pale Kariakoo hajaonekana mwanamke hata mmoja?
Kwamba wengi walijali miadi yao, starehe zao na mambo mengine yasiyo na maana
Wanaume wamesifiwa sana na katika moja ya post ameoneshwa Jk akiwa eneo la maafa kwenye ghorofa lililoporomoka 2013

Hili ni jiwe kizani na naamini limeshampata mlengwa ama mhusika mkuu.. Kama bado basi Kazi bado pevu

Good morning Tanganyika!
Yupo Brazili anavunja rekodi huko
 
Sisemi kwa ubaya lakini Rais wetu kwa hili kakosea sana!!kaonesha ni jinsi gani asivyojali hili taifa!! Kaonesha ni jinsi gani asivyo na huruma na raia wake?
Samahani mkuu 'kimsboy'. Hivi kweli wewe ulisubiri janga hili ndipo ujue kuwa rais wako" asvyo kuwa na huruma na raia wake"?

Lakini umetumia 'emotions' sana katika maelezo yako, kiasi kwamba inakuwa vigumu kuamini ulivyo guswa na mkasa huu. Kwa mfano: kuna uhakika wowote kwamba "kuna mamia ya watu waliopo chini ya kifusi"? Mimi nadhani haijalishi ni watu wangapi walioko huko, hata mmoja tu angejulikana kuwa bado yupo hai huko, huyo huyo ingefaa kupiganiwa usiku na mchana ili kuokoa maisha yake.

Halafu: weka hiyo misahafu ya dini chini; haitasaidia chochote wakati wa janga kama hili Huyo Rais unaye mlilia, atakapo rudi, msihi sana haya mahela mengi anayo tapanya kwa ununuzi wa uongozi, na ununuzi wa mapikipiki, n.k., mweleze ni wakati wa kuimarisha huduma muhimu kama hizi za uokoaji wakati wa majanga.
 
Sasa wewe kwanini usiende kusaidia kuwaokoa?

Unategemea mama Samia ndiyo akawaokoe?
Unazeeka vibaya. Kwani anasema akatoe vifusi? Issue ni kuwa unapata wapi ujasiri wa kusafiri wakati wanao wanalia chini ya vifusi? Unapata wapi apetite ya safari, wakati wahanga wanatuma massage za kukosa hewa, mauti iwakabili??
 
Sasa wewe kwanini usiende kusaidia kuwaokoa?

Unategemea mama Samia ndiyo akawaokoe?
Unazeeka vibaya. Kwani anasema akatoe vifusi? Issue ni kuwa unapata wapi ujasiri wa kusafiri wakati wanao wanalia chini ya vifusi? Unapata wapi apetite ya safari, wakati wahanga wanatuma massage za kukosa hewa, mauti iwakabili?? Majibu yako ni ya kichawi
 
Back
Top Bottom