Rais Samia karibu Kusini mwa Tanzania

Rais Samia karibu Kusini mwa Tanzania

Imekuwa muda mrefu sana, Watanzania waishio kusini mwa Tanzania pia wanatamani uwatembelee hata kama utakwenda mikono mitupu. Hakuna makuu kule, 2025 si mbali.
Ili mumpeperushie nae moshi mweupe kama magu?

Huko haji ng"oo ni katelefoni atakuwa anakuja kumuwakilisha tuu
 
Watu wa kusini kama kusingekua na gas nadhani viongozi wa kitaifa mngekua mnaishia kuwaona kwenye tv miaka yao yote ya uongozi. Yaani hata kwenye uchaguzi wangekua wanawaomba kura kupitia tv.

Ila kwa sasa kwa kua mna gesi basi watajitahidi kuja angalau mara 2 kwa miaka 5 muwaone.

Ila lazima pia muelewe kwamba rais ama marais wote wanapenda kwenda kanda ya ziwa kwa sababu kule ndio kuna determine urais wa nchi hii. Wakimaliza kanda ya ziwa wanaenda kasikazini. Nyie wa kusini hata rais asipokuja kuomba kura hamuwezi jubadilisha matokeo.

Niwaombe ndugu zangu wa kusini mkae mtulie, tutawaletea kiwanda cha gesi, tutachimba na ikiisha tutaondoka na hamtatufanya kitu. Mtumie hii fursa ya kiwanda cha gesi kubadilika. Shauri yenu.
 
Watu wa kusini lazima muelewe kwamba rais ama marais wote wanapenda kwenda kanda ya ziwa kwa sababu kule ndio kuna determine urais wa nchi hii.
Duh..., hoja nyingine kiukweli ni hoja za ukweli mchungu!. Hili la Kanda fulani kuwa ni determinant kwa urais wa nchi hii, japo sio jambo zuri, ila ni kweli!.
Kwenye uzi huu, Nimekubali matokeo, UKAWA Kanda ya Ziwa wako vizuri, Mnyika, Salum ni Combination ya hatari, nilisema
Wanabodi,

Sasa ikitokea na Kanda ya Ziwa, CCM ikachokwa mpaka basi, naomba kukiri, kwa uchaguzi wa 2015, kazi itakuwa ni rahisi sana, ni kama kumsukuma tuu mlevi!.

Kanda ya Kaskazini, waliisha kata shauri siku nyingi, kuwa CCM Basi!, ila kura za Kanda ya Kasikazini sio decisive kwa sababu kanda hiyo sio determinant ya nani anakuwa rais wa nchi hii, lakini kwa upande wa Kanda ya Ziwa, kura za kanda ya Ziwa ndio zina determine, ni nani anakuwa rais wa Tanzania!, hivyo ni decisive votes!.
Pasco.
Pia hapa nilisema kitu.

P
 
Duh..., hoja nyingine kiukweli ni hoja za ukweli mchungu!. Hili la Kanda fulani kuwa ni determinant kwa urais wa nchi hii, japo sio jambo zuri, ila ni kweli!.
P
Hoja yake haina ukweli wowote ila marais wanapenda zaidi kutembelea maeneo ya kanda ya ziwa na kanda ya kasikazini kutokana na ukubwa wake na akimaliza maeneo hayo ndipo aende maeneo ya kusini hii pia inachagizwa na mandhari ya kusuni.

Kumbuka ngome ya upinzani haipo kusini hivyo kwa strategy za kisiasa naona wanajaribu kutafuta uungwaji mkono kaskazini na nyanda za ziwa.

NB: Kusini ina upinzani ila ukitoa Mbeya na Iringa mjini maeneo mengine hayana usumbufu sana kwa CCM.
 
Hoja yake haina ukweli wowote ila marais wanapenda zaidi kutembelea maeneo ya kanda ya ziwa na kanda ya kasikazini kutokana na ukubwa wake na akimaliza maeneo hayo ndipo aende maeneo ya kusini hii pia inachagizwa na mandhari ya kusuni...
Kwa ujumla kanda ya ziwa na kaskazini ndo iliko nchi na huu ndo ukweli!
 
Imekuwa muda mrefu sana, Watanzania waishio Kusini mwa Tanzania pia wanatamani uwatembelee hata kama utakwenda mikono mitupu.

Hakuna makuu kule, 2025 si mbali.
Mpaka mtengeneze barabara za Mtwara-Tandahimba-Newala-Masasi-Nachingwea-Liwale. Hapo anaweza kuwaza kuja, nakumbuka kama kitabu changu cha matukio kipo sahihi enzi za umakamu msafara wake ni kama vile ulipata ajali, kama nijasahau ni barabara ya Mtwara-Tandahimba.
 
Watu wa kusini kama kusingekua na gas nadhani viongozi wa kitaifa mngekua mnaishia kuwaona kwenye tv miaka yao yote ya uongozi. Yaani hata kwenye uchaguzi wangekua wanawaomba kura kupitia tv...
Sawa kama ni hivyo basi tuache muda uongee, kwani Tanzania sasa imekuwa ni Dodoma, Geita, Mwanza, Manyara, Kilimanjaro, Tanga , Dar na Zanzibari.
 
Hoja yake haina ukweli wowote ila marais wanapenda zaidi kutembelea maeneo ya kanda ya ziwa na kanda ya kasikazini kutokana na ukubwa wake na akimaliza maeneo hayo ndipo aende maeneo ya kusini hii pia inachagizwa na mandhari ya kusuni...
Wamewauzia mbolea kwa shilingi 98-100 K huu mwaka. Na bado Raisi wao wanamwona kwenye TV, na si kwamba hasafiri, lahasha anasafiri na mpaka ng'ambo kavuka kwao hajawahi enda, "I just image if even Hon Kassim couldn't be from Ruagwa , would he dare to visit?" actually not, Yupo makamu Dr Mpango, hata huyo basi ? .
 
Hoja yake haina ukweli wowote ila marais wanapenda zaidi kutembelea maeneo ya kanda ya ziwa na kanda ya kasikazini kutokana na ukubwa wake na akimaliza maeneo hayo ndipo aende maeneo ya kusini hii pia inachagizwa na mandhari ya kusuni. Kumbuka ngome ya upinzani haipo kusini hivyo kwa strategy za kisiasa naona wanajaribu kutafuta uungwaji mkono kaskazini na nyanda za ziwa.
NB: Kusini ina upinzani ila ukitoa Mbeya na Iringa mjini maeneo mengine hayana usumbufu sana kwa CCM.
Ikumbukwe kwamba huu sio muda wa kampeni wala uchaguzi, huu ni muda wa kuijega Tanzania. Sasa kwanini asiende, Kama yeye angeli dhamiria na kukosa muda basi ningetegemea kumuona hata Makamu wake.
 
Imekuwa muda mrefu sana, Watanzania waishio Kusini mwa Tanzania pia wanatamani uwatembelee hata kama utakwenda mikono mitupu.

Hakuna makuu kule, 2025 si mbali.
Huko Hakuna uwanja wa ndege. Atakujaje?
 
Imekuwa muda mrefu sana, Watanzania waishio Kusini mwa Tanzania pia wanatamani uwatembelee hata kama utakwenda mikono mitupu.

Hakuna makuu kule, 2025 si mbali.
Kusini walitengwa tangu Ukoloni baada ya kukataa mkoloni asiwatawale kidhalimu. Serikali zote zilizotokea Tanzania zinafuata historia ya misimamo mikali ya watu wa kusini.
Udhalimu ni adui mkubwa wa watu wa kusini.

Wangoni ni hatari Kwa wanyonyaji.
Wamatumbi ni hatari Kwa wanyonyaji.
Wamwera hawaeleweke sawasawa.
Wamakonde ni hatari sana Kwa wezi.
Wayao ni hatari Kwa matapeli na wezi.

Hawa watu wa kusini kwanza hawana tamaa ya fedha nyingi na mali nyingi. Wanajali kile kinachowahusu TU hata kama ni kidogo ni Cha kwao. Wana ardhi kubwa yenye utajiri mara nyingi kuliko ule wa Kanda nyingine lakini walimkimbiza mkoloni asiikalie hasa Mjerumani ni umahiri wake alinyoisha mkono akaacha mashamba ya mkonge,pamba chai ,gesi, madini ya rubi na mafuta kule Rwangwa. Walifanikiwa TU kuondoka na mabaki ya mjusi mkubwa kuliko wanyama wote waliopo Karne hii.

Kanda nyingine ni Kanda za kimaslahi na wabinafsi. Kanda za waroho wa madaraka. Kanda za watu wenye viashiria vya ukabila.Mtu anapewa ukuu wa mkoa miaka minne anakua Bilionea wa kutupa mapaka anasema IST ni gari ya kuhonga TU demu Kwa tendo Moja la zinaa.Kuna watu wa kusini wamelitumikia Taifa hili Kwa miaka 40 lakini hawana tamaa ya KUIBIA au kukwapua Mali za umma au kutumia madaraka yao kujilimbikizia Mali.
Kawawa.
Kingunge.
Jenista mhagama.
Mahiza.
Majaliwa
Bwege.
Nape.
Mama Salma
Chiligati.
n.k.
Wamekua waadilifu sana kwenye nchi hii ya Kijamaa. Hata vijiji vyao vimeoangwa Kijamaa.
Tusiwabeze watu wa kusini. Wanafaa kuwa viongozi wa nchi hii ya Kijamaa.

Watu wa kusini wanaogopwa Kwa misimamo yao imara isiyotetereka.
Msimamo wa Mbunge mmoja wa kusini ni wabunge wote wa CCM Tanganyika. Msimamo wa Nape hauyumbi ndani na nje ya Chama.
Nape anafaa Kwa baadae. Ni mtu jasiri na mkweli hata kwenye utawala dhalimu anasema ukweli.

Kusini hoyeee.
Angalieni Shangazi zenu wasije wakapigwa tukabaki na Shangazi Wawili TU ,Maria na Fatma.

Tutafute Katiba mpya ili tuondokane na haya maujinga ya kupata viongozi kikanda na kikabila na kidini. Ni upumbavu mkubwa.

Tunataka tuwashindanishe watu Kwa hoja na maono chini ya Katiba Mpya inayotoa uhuru,haki,usawa, uzalendo ,utu na uadilifu .
Tunataka kuona watu waadilifu wakikalia ofisi za umma bila kunyimwa haki ya kuonyesha uwezo wao zaidi ya kubebwa na kutishana.

Kama sio katiba Bora ya Marekani Obama pamoja na uwezo wake asingekua Rais wa Taifa kubwa Duniani.

Tunataka Katiba Bora .

Tunataka tumsikie Nape Moses Nnauye Kwa hoja na ujasiri wake tuoni kama ni Chama kinambeba au yeye ndio anakibeba.

Tunataka tumsikie Mwigulu Kwa hoja sio kubebwa Bali aonyeshe uwezo wake Kwa kushindana Kwa haki na uhuru kwenye majukwaa na midahalo ya wazi ndani ya Chama na nje ya Chama.

Tunataka tumsikie Ndugai kwa hoja za kukataa mikopo mikopo na kujitegemea sio kufungwa mdomo kama farasi ili abebe Chama na watawala wasio na sifa.

Tunataka kumsikia Msomi Mahiri na Wakili Tundu Antipas Lisu Kwa hoja sio kumtisha.

Tunataka tumsikie Freeman Mbowe na maono yake Kwa Taifa hili Kwa Nini anakubali mateso Nini anakiwaza Kwa Taifa hili ,Kwa Nini anakua Mzalendo kiasi hicho je anaweza kushindana na uzalendo wa Polepole au Ndugai au Gwajima?

Tunataka tumsikie Zito Kwa hoja.

Tunataka tumsikie RC Anton mtaka Kwa hoja sio Kwa kabila lake.

Tunataka tumsikie Januari Kwa hoja zake sio kubebwa Wala kutengeneza mtandao .
Tunataka Katiba itakayomfanya Ridhiwani asikike Kwa hoja zake zenye maono mema na makubwa Kwa Taifa hili sio kubebwa Bali ajibebe ili tumshindanishe na Lema.

Tunataka tusikie hoja za Wanawake wasomi kama Maria Sarungi, Fatma Karume , Halima Mdee, ESTA Bulaya na wengine wakiwa huru ndani ya vyama vyao na nchi Kwa ujumla wakipigwa chini na wananchi kwenye kura Kwa hoja ndani na nje ya vyama vyao.

Tunataka Katiba itakayomfanya mtawala kuwa huru katika maamuzi bila kuogopa kakundi ka watu ndani ya vyama
Tunataka tumsikie Rais wetu Mama Samia akiwa huru ndani na nje ya Chama chake. Lakini akiweka mbele maslahi ya Nchi kuliko maslahi ya Chama kilichoundwa mwaka 1977. Nchi na watu waliumbwa na Mwenyezi Mungu. Kujali Chama kuliko Taifa ni dhambi kubwa sana.

Tunataka tuone katiba itakayotupatia majaji wenye sifa ndani ya nchi mpaka kwenye jumuiya ya madola. Wale Kodi yetu kihalali Kwa kutenda haki Kwa maana halisi ya ujaji na miiko yake sio Jaji wa kupangiwa hukumu na watu Kwa maslahi ya waovu.
 
Watu wa kusini kama kusingekua na gas nadhani viongozi wa kitaifa mngekua mnaishia kuwaona kwenye tv miaka yao yote ya uongozi. Yaani hata kwenye uchaguzi wangekua wanawaomba kura kupitia tv.

Ila kwa sasa kwa kua mna gesi basi watajitahidi kuja angalau mara 2 kwa miaka 5 muwaone.

Ila lazima pia muelewe kwamba rais ama marais wote wanapenda kwenda kanda ya ziwa kwa sababu kule ndio kuna determine urais wa nchi hii. Wakimaliza kanda ya ziwa wanaenda kasikazini. Nyie wa kusini hata rais asipokuja kuomba kura hamuwezi jubadilisha matokeo.

Niwaombe ndugu zangu wa kusini mkae mtulie, tutawaletea kiwanda cha gesi, tutachimba na ikiisha tutaondoka na hamtatufanya kitu. Mtumie hii fursa ya kiwanda cha gesi kubadilika. Shauri yenu.
Gas ilishavunwa yote
 
Back
Top Bottom