Rais Samia karuhusu upandaji wa LUKU mwisho wa mwezi, kipindi wakiwa na Magufuli waliahidi kushusha bei ya umeme, Imekuwaje?

Rais Samia karuhusu upandaji wa LUKU mwisho wa mwezi, kipindi wakiwa na Magufuli waliahidi kushusha bei ya umeme, Imekuwaje?

Itoshe tu kusema. CCM ni. ile ille...Samia anadolishia tu watu kule kama watoto,eti ameleta kile na hiki basi,utadhani ametoa hela yake mfukoni: Ni uswahili na usanii wa Zenj tu.
inaonyesha dhahiri kwamba una chuki ndani ya moyo wako.

kwani Magufuli alikuwa hasemi 'nimeleta'?
 
Akili zako zinafanya uhisi kila mtu ni CCM, mm nakuambia ukweli, acha kudeka deka, vitu vingine solutions zake ni simple sio za kuita wanasiasa, unakuwa kama mtoto,

Yan mbaba na ndevu zako unashindwa mpanga mwenye nyumba wako suala la buku jero ya kodi ya jengo ?

Mnafeli bana,
Mtu km Wewe Ni kujichosha tu kujibizana na wewe.hujui chochote unajifanya kwamba Wewe Ni mwelevi lkn huna unachokijua,na Ni hasara Sana kuwa na watu wa aina yako kwenye ili Taifa
 
inaonyesha dhahiri kwamba una chuki ndani ya moyo wako.

kwani Magufuli alikuwa hasemi 'nimeleta'?
Magufuli alikuwa nani na wa chama gani...na unaelewa maana ya CCM ni ileile?!Nani alikwambia mimi ni muumini wa Magufuli...Kwangu CCM wote mpaka wewe ni K...
 
Magufuli alikuwa nani na wa chama gani...na unaelewa maana ya CCM ni ileile?!Nani alikwambia mimi ni muumini wa Magufuli...Kwangu CCM wote mpaka wewe ni K...
so what! ukishindwa hoja ndiyo uweke acronym ya tusi? inaonyesha jinsi IQ yako ilivyo na matatizo.
 
Mkuu, hio ni kodi ya nyumba, haihusihani na TANESCO,
kingine wabongo tuache kulia lia,
Mfuate mwenye nyumba wako, mwambie arudishe hio 18k unayolipa kwa mwaka, mana ni jukumu lake, mbona simple tu ?

Yan tunalia vitu vidogo vya kusolve wenyewe tu
Unahisi huu ni utaratibu sahihi? Kwanini mwenye nyumba asikatwe kwa namna nyingine bila kuhusishwa mpangaji? Unaona ipo sawa kabisa kumfuata mwenye nyumba ndio akurudishie hela yako? Halafu asiporudisha unamshtaki au? Na unamshtaki kwa kosa gani?
 
Unahisi huu ni utaratibu sahihi? Kwanini mwenye nyumba asikatwe kwa namna nyingine bila kuhusishwa mpangaji? Unaona ipo sawa kabisa kumfuata mwenye nyumba ndio akurudishie hela yako? Halafu asiporudisha unamshtaki au? Na unamshtaki kwa kosa gani?
Ndio ni sahihi, serikali inajua mwenye meter ni mwenye nyumba, kama utaenda kukodi meter ya mtu, bas elewa inadaiwa
 
Kuna tuliobadirishiwa mita.za luku hasa double phase na.kupewa mita.za.edmi ni kilio kwanimita.hizi zinakula umeme isivyo kawaida.

Najuta kwa nini nililubali kupewa smart meter ya edmi ambayo inakiwa ni box linakaa juu ya.nguzo na remote unapewa unakaa nayo ndani.

Kuna utapeli mkubwa alyetengeneza mita hizi kwenda hataka.isivyo maelezo na kumaliza umeme haraka.sana. chukueni taadhari.

Na tulidhani bwawa la.umeme likianza.unit ya.umeme itashuka.yola.ilipokuwa.shs.327 kwa.unit irudi.walau shs 200 lakini.serikali ya.ccm.haijaliwananchi
 
Miongoni mwa waliohudhuria kwenye mikutano ya Rais Samia huko Katavi na mimi nilikuwepo

Kwenda kwangu kwenye mikutano hiyo, siyo kwamba ndio namkubali Rais katika utendaji wake, hapana

Nimepatwa na shida sana kichwani kuamini kwamba, huyo ndiye aliyezunguka na JPM kuomba kura huku wakituahidi maisha chipa pindi mitambo ya umeme ya JKHNP itakapokamilika na kuanza kutumika

Cha kushangaza ni kwamba, baada tu ya kukamilika na kuanza kutumika tukaanza kushuhudia Luku inawekewa tozo za ajabu ajabu zisizoeleweka,

Mbali na hilo, kipindi cha nyuma, Aliyekuwa aliyekuwa waziri wa Nishati bwana Januar Makamba, alitoa tamko mapema kuhabarisha kwamba, umeme hautashuka bei kama ilivyowahi kusikika kipindi cha viongozi hao wawili walipokuwa wakieleza manufaa ya kuwa na mradi wa JKNHP, hii ni kwa sababu walizozijuwa wao kina Makamba

Kwa maana hiyo, yawezekana kabisa kwamba, wapo na wananchi maelfu kwa maelfu waliohudhuria mikutano hiyo kwenda kumshangaa Rais huku wakiwa na maswali kama niliyonayo mimi,

Maana inakuwa ngumu sana kuamini, mtu aliyezunguka nchi nzima kutueleza umeme utashuka bei mara tu baada ya kuanza uzalishaji wa umeme kwenye mradi wa JKNHP kule rufiji leo amegeuka hivihivi yaani, uungwana ni tabu sana

Leo kageukaje? Licha ya hivyo, bado ameruhusu Luku iwe inatozwa fedha kibao mwisho wa mwezi wakati huo huo akijua walipaji wakuu wa tozo hiyo ni walala hoi waliopangishwa najumba na kundi la wenye kipato cha juu?

Siku mlala hoi atakapohitaji kuondokana na ulala hoi, shariti ajikatae, aseme yeye si yeye, bila shaka ndipo ataanza kuzisogelea ndoto zake

Mungu bariki nchi yangu Tanzania, Utupatie na viongozi makomando huwenda tutapa ahuweni!

Ameen


Pia soma: Magufuli aliondoa 'Service Charge' Tanesco ya 7,000 lakini Serikali ya sasa inazirudisha tozo kidogokidogo kupitia mfumo wa Luku
Kwa kweli hili ni janga wametupuuza Hawa watawala wetu. Kumbe sisi hatuna umuhimu !
 
Back
Top Bottom