Rufiji dam
JF-Expert Member
- Feb 20, 2020
- 4,107
- 9,671
Mama Samia kama unajua ama haujui kuna jambo baya linafanyika kupitia utawala wako. Nimetembea ofisi za binafsi hasa mabenki kutokana na nature ya shughuli zangu za binafsi nimekutana na jambo la hofu sana.
Kuna barua zinazambazwa kuomba mchango wa kufanikisha sherehe za mwaka mmoja toka uchukue uongozi, je hizi barua unazijua na huu mpango wa kuomba fedha je unabaraka zako?
Tuache kucheza na maisha ya watu. Mama unachangiwa fedha za sherehe yako ya mwaka mmoja kuongoza nchi? Kuna ulazima gani wa kufanyiwa sherehe? Kuna jipya lipi uongozi wako umelifanya mpaka likawa la ajabu ndani ya mwaka mmoja hivyo tunapaswa kusherekea.
Mama sitisha mpango huu kama pesa umebariki ipatikane ni vyema ikatumika kununulia vitanda vya watoto njiti ama ukawapa bima ya afya watoto masikini. Ila ukibariki hili umebariki wizi. Chawa hana huruma.