Rais Samia, Katibu Mkuu Kiongozi undeni upya vetting section

Rais Samia, Katibu Mkuu Kiongozi undeni upya vetting section

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2019
Posts
762
Reaction score
6,984
Niombe sana Mhe. Rais upitie upya mfumo wa serikali unaopelekea majalada yafike mezani kwako kwa utiaji sahihi. Yawezekana mfumo huu ulivurugwa au umevurugwa bila kuzingatia utaratibu uliowekwa kwenye Utumishi wa Umma.

Upo uwezekana wapo watu wachache wasio waadilifu wameingizwa jikoni lakini pia upo uwezekano Kuna hujuma inaendele.

Nayaona makosa ya wazi kabisa katika teuzi ulizofanya, kosa la wazi lakiufundi lilifanywa kumpata Mkurugenzi wa petrolium and gas. Kosa hili umelirekebisha.

Jana zimesambaa taarifa za ofisi yako kumteua raia wa Marekani, natamani taarifa hizi ziwe za uongo. Ikiwa ni za kweli basi nachagua kuiombea ofisi yako ifunuliwe na kuanza kusaka vijana waadilifu kwenye taasisi mbalimbali wenye upeo mpana waje wakae ofisini kwako. Yamkini wazee hawajitumi kujielimisha na Awana muda na global issues.

Ikulu ni ya Watanzania watafute Watanzania wabobezi wape maeneo haya nyeti ili waweze kukung'ata sikio kabla PDF haijatoka.

Nikutakie kazi njema
 
Wewe mara umtetee Kakoko, ambaye ni mpigaji mzoefu, sasa unaibuka na rumours za mitandaoni as if it's official appointment?

Mama yupo vzr ndo maana hata jina la VP halikuvuja popote..
 
Huyo mtu kateuliwa kuwa kitu gani, mbona hamsemi?

Raia wa Marekani kateuliwa kufanya kazi ikulu ya Tanzania, au kateuliwa kuwa consul wetu kwenye kijiji kimoja huko Marekani avutie watalii wengi waje hapa?

Lakini ninakubaliana nawe, serikali hii ya mama bado ina ushamba mwingi. Sijui ni kukosa uzoefu au ndiyo hivyo tena ni Jamhuri yetu mpya ya Ndizi!
 
Wewe hukuona uteuzi uliofanywa na Rais juzi? Uko dunia ya wapi?

Sio kila kitu unachoona wewe kila mtu kakiona!! Sawa wewe uliyeona mbona unashindwa kujibu swali jepesi kabisa!! Kateuliwa kuwa nani mpaka midomo yenu inataka kupasuka kwa kupiga mayowe!!! Mnashindwa kutaja kwasababu mmekurupuka kushutumu wakati hamna facts ndezi nyie!!
 
Yani jina la VP kutovuja nayo ni sifa!
Kuna tatizo gani watu wangejua mapema VP VP atakuwa fulani? Mbona nchi zilizoendelea watu wanafahamu mapema fulani na fulani watataeuliwa katika nafasi fulani??
Wakati mwingine watu muache kuwa washamba.
Wewe mara umtetee Kakoko, ambaye ni mpigaji mzoefu, sasa unaibuka na rumours za mitandaoni as if it's official appointment?

Mama yupo vzr ndo maana hata jina la VP halikuvuja popote..
 
Yani jina la VP kutovuja nayo ni sifa!
Kuna tatizo gani watu wangejua mapema VP VP atakuwa fulani? Mbona nchi zilizoendelea watu wanafahamu mapema fulani na fulani watataeuliwa katika nafasi fulani??
Wakati mwingine watu muache kuwa washamba.
Wewe ndo mshamba, tunaongelea TZ wewe una cite sijui nchi zilizoendelea.
Hizi strategies za kijinga kujaribu kujinasua na crimes one committed hazisaidii kitu. Let him pay the price, malipo hapa hapa duniani
 
Kama ana Asili ya Tanzania au wazazi wake wana uraia wa Tanzania hakuna tatizo angekuwa anatoka Kenya ,Rwanda au EA hapo ingekuwa Tatizo coz hawa ni washindani wetu lakini US sidhani kama wanaweza kumtumia huyu kwa njia yeyote ile kwani wakitaka taarifa au jambo lolote Tanzania wana njia zao za kupata huyu hana madhara yeyote ni namuona ni sawa na Rashid wa Kawe tu.
 
Hilo tatizo lilishamili sana miaka 5 iliyopita kwa teuzi za unqualified personnels kupewa madaraka makubwa kwenye ofisi za Umma na consequences zake tuliziona kiuchumi na kijamii.

Mama naona ameanza vizuri kwenye teuzi zake ingawa alitaka kupotoshwa kwa Mkurugenzi wa Bandari. Hopefully vetting inafanyika this time kabla ya teuzi.
 
Back
Top Bottom