Rais Samia kinara wa kuzalisha ajira Tanzania

MANKA MUSA

JF-Expert Member
Joined
Jul 9, 2014
Posts
924
Reaction score
1,096
No Joke- Rais Samia Ametengeneza ajira nyingi zaidi ndani ya kipindi cha miezi 18 kuliko Marais wa Tatu waliopita Tanzania.

Amerejesha asilimia 90 ya kazi zilizopotea chini ya janga la Corona.

Amepandisha madaraja na mishahara kwa Watumishi wa Sekta ya Umma kwa asilimia 23 jambo ambalo halikufanyika kwa kipindi cha miaka 6.

Ajira ziko wapi…
Mradi wa Gesi Asilia.
Vijana ajira ni hizi hapa zikiwa fresh kabisa Juni 11, 2022 Tanzania ilitia saini makubaliano ya awali ya mkataba wa nchi hodhi (HGA) wa mradi wa kuchakata na kusindika gesi asilia kati ya nchi na wawekezaji.

Huu ni mkataba wa kihistoria kwa ukubwa wa thamani yake kuwahi kuingiwa na taifa hilo la Afrika Mashariki, ukigusa eneo hilo la nishati ya gesi, ambayo inazidi kuongezeka thamani kila uchao.

Mkataba huo una thamani ya shilingi za kitanzania zaidi ya trilioni 70, ambazo ni sawa na dola za Marekani bilioni 30, ambazo zinaweza kuleta mageuzi ya uchumi iwapo zitasimamiwa na kutumika ipasavyo. Swali ambalo wengi wanajiuliza makubaliano haya yatainufaishaje Tanzania, je utakuwa kaa la moto kama mingine mikubwa iliyowahi kuingiwa?

Sehemu kubwa ya gesi hiyo, takribani futi trilioni 49.5 za ujazo, zipo katika kina kirefu chini ya Bahari ya Hindi. Maana yake mitambo ya teknolojia ya juu itahitajika kuichimba.

Mkataba huu na kampuni za Shell ya Uingereza na Equinor ya Norway unakwenda kuiwezesha kuichimba na kuichakata gesi hiyo tayari kwa ajili ya kuuzwa ikiwa katika mfumo wa Liquidfied Natural Gas (LNG).

LNG ni gesi iliyochakatwa na kuwekwa katika mfumo wa kimiminika huku ikiwa imesindikwa kwa zaidi ya mara 600 kutoka katika ukubwa wake wa asili na kuwa katika hali ya ubaridi mkali wa nyuzi joto hasi 162 ili kurahisisha utunzaji na usafirishaji wake.

Utekelezaji wa mradi huu unatarajiwa kukamilika mwaka 2025 na kuanza shughuli kati ya mwaka 2029 na 2030 kwenye mtambo wa gesi ya kioevu utakaojengwa katika mji wa Lindi uliopo kusini mwa Tanzania zaidi ya kilomita 450 kutoka jiji la kibiashara la Dar es Salaam.

Ujenzi huo utaenda sambamba na ujenzi wa ukanda wa kiuchumi kwa ajili ya kusaidia huduma kwenye mradi.

Ukiacha miundo mbinu ya barabara, maji na majengo ya kisasa yakiwemo, huduma muhimu za kibinadamu zitazalisha ajira maelfu ya ajira kwa Watanzania.

'Faida za wazi za mradi, ni kutengeneza ajira nyingi na kuongeza mzunguko wa fedha nchi Vijana tuingieni kwenye mnyororo wa thamani tukuze uchumi wa nyumbani.

Mradi wa Maji miji 28.
ndio mradi mkubwa wa maji, kuwahi kutekelezwa nchini kati ya miradi mikubwa iliyowahi kutekelezwa ambapo hakuna mji hata mmoja utakaoachwa.

Ni Mradi utakaogharimu zaidi ya Sh1 trilioni, ambazo ni fedha za mikopo zilizotolewa na Serikali ya India, ikiwa ni matokeo ya uhusiano mzuri kati ya nchi hizo.

Mradi huu unategemewa kuzalisha ajira zaidi na kusisimua uchumi.

Ruzuku ya Bilioni 150 kwenye Pembejeo.

Serikali itaanza kutoa ruzuku ya mbolea za viwandani kwa wakulima wa mazao yote nchini ili kupunguza maumivu kwa wakulima yaliyotokana na kupanda kwa bei za mbolea, hususani katika msimu wa kilimo wa 2021/2022.

Katika kipindi cha kati ya mwaka 2020 na mwaka 2022, bei ya mbolea kama ya UREA kwa tani moja zilipanda kutoka Dola za Marekani 251 hadi Dola za Marekani 1,214.

Kutengwa kwa ruzuku kunaweza kusaidia kupunguza athari zitokanazo na mabadiliko ya bei za mbolea kwenye soko la dunia, hivyo kuwanufaisha wakulima.

Ruzuku za pembejeo ni sehemu tu ya misaada ya Serikali kwa wakulima hususani wadogo ambao ndiyo wanaunda sehemu kubwa ya uzalishaji wa mazao nchini.

Kwa sehemu kubwa ruzuku zimewezesha matumizi ya pembejeo za kilimo na hivyo kuongeza tija kwenye kilimo. Na kuongeza nafasi kubwa kwenye ajira nchini.

Serikali pia inaendelea na utekelezaji wa mradi wa SGR.

Utekelezaji wa bwawa la kufua Umeme la Mwalimu Nyerere.
 
Hii sifia sifia kwa Nchi masikini kama Tanzania na ina kila kitu cha Kufanya tuinuke kiuchumi ni Ujinga mkubwa sana na ndio mtaji wa Wanasiasa.
 
Sifa hazijengi nchi,.... ubongo, macho na masikio tunayo so hatuhitaji kuambiwa.
 
Unasema Samia kinara wa kuzalisha ajira halafu sababu unayoitoa ni kuwa amesaini mkataba wa kusindika ajira. Ilipaswa kusubiri mpk mradi huo uanze ndipo ulete mada hii
 
Tatizo mmezoea vya kunyonga vya kuchinja amviwezi. Vijana wengi wanashindwa kuingia kwenye fursa kutokana na tabia ya kuwa na mindset za kukatishana tamaa. Mradi wa maji huo, Mradi wa Gesi huo, Ruzuku ya mbolea hiyo.
Upande uliochagua una uhai mfupi zaidi jenga hoja kupitia taarifa tujadili kisomi kama kijana.
 
Hii sifia sifia kwa Nchi masikini kama Tanzania na ina kila kitu cha Kufanya tuinuke kiuchumi ni Ujinga mkubwa sana na ndio mtaji wa Wanasiasa.
Hii ni taarifa ya wazi kulingana na miradi hii miwili Tanzania haijawahi kusaini miradi mikubwa kama hii tangu tupate Uhuru.
 
No Joke- Rais Samia Ametengeneza ajira nyingi zaidi ndani ya kipindi cha miezi 18 kuliko Marais wa Tatu waliopita Tanzania.

Amerejesha asilimia 90 ya kazi zilizopotea chini ya janga la Corona.

Amepandisha madaraja na mishahara kwa Watumishi wa Sekta ya Umma kwa asilimia 23 jambo ambalo halikufanyika kwa kipindi cha miaka 6.

Ajira ziko wapi…
Mradi wa Gesi Asilia.
Vijana ajira ni hizi hapa zikiwa fresh kabisa Juni 11, 2022 Tanzania ilitia saini makubaliano ya awali ya mkataba wa nchi hodhi (HGA) wa mradi wa kuchakata na kusindika gesi asilia kati ya nchi na wawekezaji.

Huu ni mkataba wa kihistoria kwa ukubwa wa thamani yake kuwahi kuingiwa na taifa hilo la Afrika Mashariki, ukigusa eneo hilo la nishati ya gesi, ambayo inazidi kuongezeka thamani kila uchao.

Mkataba huo una thamani ya shilingi za kitanzania zaidi ya trilioni 70, ambazo ni sawa na dola za Marekani bilioni 30, ambazo zinaweza kuleta mageuzi ya uchumi iwapo zitasimamiwa na kutumika ipasavyo. Swali ambalo wengi wanajiuliza makubaliano haya yatainufaishaje Tanzania, je utakuwa kaa la moto kama mingine mikubwa iliyowahi kuingiwa?

Sehemu kubwa ya gesi hiyo, takribani futi trilioni 49.5 za ujazo, zipo katika kina kirefu chini ya Bahari ya Hindi. Maana yake mitambo ya teknolojia ya juu itahitajika kuichimba.

Mkataba huu na kampuni za Shell ya Uingereza na Equinor ya Norway unakwenda kuiwezesha kuichimba na kuichakata gesi hiyo tayari kwa ajili ya kuuzwa ikiwa katika mfumo wa Liquidfied Natural Gas (LNG).

LNG ni gesi iliyochakatwa na kuwekwa katika mfumo wa kimiminika huku ikiwa imesindikwa kwa zaidi ya mara 600 kutoka katika ukubwa wake wa asili na kuwa katika hali ya ubaridi mkali wa nyuzi joto hasi 162 ili kurahisisha utunzaji na usafirishaji wake.

Utekelezaji wa mradi huu unatarajiwa kukamilika mwaka 2025 na kuanza shughuli kati ya mwaka 2029 na 2030 kwenye mtambo wa gesi ya kioevu utakaojengwa katika mji wa Lindi uliopo kusini mwa Tanzania zaidi ya kilomita 450 kutoka jiji la kibiashara la Dar es Salaam.

Ujenzi huo utaenda sambamba na ujenzi wa ukanda wa kiuchumi kwa ajili ya kusaidia huduma kwenye mradi.

Ukiacha miundo mbinu ya barabara, maji na majengo ya kisasa yakiwemo, huduma muhimu za kibinadamu zitazalisha ajira maelfu ya ajira kwa Watanzania.

'Faida za wazi za mradi, ni kutengeneza ajira nyingi na kuongeza mzunguko wa fedha nchi Vijana tuingieni kwenye mnyororo wa thamani tukuze uchumi wa nyumbani.

Mradi wa Maji miji 28.
ndio mradi mkubwa wa maji, kuwahi kutekelezwa nchini kati ya miradi mikubwa iliyowahi kutekelezwa ambapo hakuna mji hata mmoja utakaoachwa.

Ni Mradi utakaogharimu zaidi ya Sh1 trilioni, ambazo ni fedha za mikopo zilizotolewa na Serikali ya India, ikiwa ni matokeo ya uhusiano mzuri kati ya nchi hizo.

Mradi huu unategemewa kuzalisha ajira zaidi na kusisimua uchumi.

Ruzuku ya Bilioni 150 kwenye Pembejeo.

Serikali itaanza kutoa ruzuku ya mbolea za viwandani kwa wakulima wa mazao yote nchini ili kupunguza maumivu kwa wakulima yaliyotokana na kupanda kwa bei za mbolea, hususani katika msimu wa kilimo wa 2021/2022.

Katika kipindi cha kati ya mwaka 2020 na mwaka 2022, bei ya mbolea kama ya UREA kwa tani moja zilipanda kutoka Dola za Marekani 251 hadi Dola za Marekani 1,214.

Kutengwa kwa ruzuku kunaweza kusaidia kupunguza athari zitokanazo na mabadiliko ya bei za mbolea kwenye soko la dunia, hivyo kuwanufaisha wakulima.

Ruzuku za pembejeo ni sehemu tu ya misaada ya Serikali kwa wakulima hususani wadogo ambao ndiyo wanaunda sehemu kubwa ya uzalishaji wa mazao nchini.

Kwa sehemu kubwa ruzuku zimewezesha matumizi ya pembejeo za kilimo na hivyo kuongeza tija kwenye kilimo. Na kuongeza nafasi kubwa kwenye ajira nchini.

Serikali pia inaendelea na utekelezaji wa mradi wa SGR.

Utekelezaji wa bwawa la kufua Umeme la Mwalimu Nyerere.
Hizo hawatakuelewa hao pimbi ila ukiwaonesha za hivi ndio wataelewa 👇
 
Attachments

  • Screenshot_20220713-195102.png
    Screenshot_20220713-195102.png
    157.7 KB · Views: 6

Anafanya vizuri maombi yangu amtoe Majaliwa kwenye nafasi ya Waziri Mkuu. Asante.
 
Back
Top Bottom