Akitambua uwepo wa viongozi na waalikwa katika Mkutano wa wa 15 wa Baraza la Taifa la Biashara, Raisi Samia kaanza kwa kutambua uwepo wa Makamu wa Raisi kisha Raisi wa Zanzibar na ndio akmataja Waziri Mkuu wa Tanzania, Bwana Kassimu Majaliwa.
Swali langu ni je, kati ya Raisi wa Zanibar na Waziri Mkuu wa Tanzania, ni nani mwenye cheo kikubwa?
Zanzibar si ni sehemu ya Tanzania, sasa iweje Raisi wa Zanzibar ambae ni sehemu tu ya Muungano awe juu ya Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania?
Waziri Mkuu kikatiba ni mkubwa kuliko rais wa Zanzibar.
Hizo zinafanyikan zinafanyikan makusudi kabisa ku mo overate Rais wa Visiwabvya Zanzibar ambavyo sawa na wilaya Moja huku Bara.
Mamlaka ya Waziri Mkuu, kwenye Baraza la MAWAZIRI ,
Ibara ya 50, kifungu kidogo Cha (I) na Cha (ii) kinaonesha vizuri sana, kwamba KUTAKUWA NA BARAZA LA MAWAZIRI,
Linaundwa na Rais wa URT nayae atakuwa Mwenyekiti, asipokuwepo Makamu wa Rais.
Ikitokea Rais na makamu kwa pamoja hawapo,waziri Mkuu ataongoza kikao Cha Baraza la MAWAZIRI.
Wajumbe wanaounda Baraza la MAWAZIRI.
Mosi Rais, Mbili Makamu, tatu Waziri Mkuu.
Nne MAWAZIRI wote kamili sio manaibu,ni wajumbe, na Rais wa Zanzibar ni mjumbe tu,akiwa anaingia baraza la mawaziri hadhi yake ni sawa na Innocent Bashungwa au Masauni.
Nyongeza ikitokea Rais hayupo nchini Rungu anashiklia Makamu wa Rais, asipokuwepo yeye pia, Rungu atashika waziri Mkuu, naye asipokuwepo atashika speaker wa Bunge, na ikitokea wote hao hawapo kwa pamoja nchi itakuwa chini ya jaji mkuu!
Hapo Rais wa Zanzibar hatajwi.
Kumruka waziri mkuu au waziri mkuu kutangulia kuingia kwenye sherehe za kitaifa katika accending order na descending order yaani order of seniority ni JANJAJANJA tu ya makusudi inayofanyika.
Lakini ni ukiukwaji wa katiba mchana kweupe.
Hayo yanatosha kuelewa hata kwa mwanafunzi wa elimu ya Uraia Civics kuelewa kuwa waziri mkuu ni Mtu Mkubwa sana katika nchi kimamlaka na protocal akiwa chini ya Makamu wa Rais.
Kwahiyo kumdogosha waziri mkuu ni mbwembwe na janjajanja flani ya makusudi.
😅🤔🙏