Rais Samia, kiprotokali ni sahihi kumtaja Rais wa Zanzibar kabla ya Waziri Mkuu wa Tanzania?

Rais Samia, kiprotokali ni sahihi kumtaja Rais wa Zanzibar kabla ya Waziri Mkuu wa Tanzania?

Ijulikane kuwa waziri mkuu wa Tanganyika na si vingenevyo. Mwawaziri wakuu wawili ndani ya jamhuri ya muungano ni utata.
 
Akitambua uwepo wa viongozi na waalikwa katika Mkutano wa wa 15 wa Baraza la Taifa la Biashara, Rais Samia kaanza kwa kutambua uwepo wa Makamu wa Rais kisha Rais wa Zanzibar na baada ya hapo ndio akamataja Waziri Mkuu wa Tanzania, Bwana Kassimu Majaliwa na kisha akaendelea kutaja wageni wengine waliokuwa wamehudhuria katika tukio hilo.

Swali langu ni je, kati ya Raisi wa Zanibar na Waziri Mkuu wa Tanzania, ni nani mwenye cheo kikubwa?

Zanzibar si ni sehemu ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, sasa iweje Rais wa Zanzibar ambae ni sehemu tu ya Muungano awe juu ya Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania?
Rais wa Zanzibar akikanyaga ardhi ya bara anakuwa na hadhi ya waziri.

Na Waziri mkuu ni boss wa Mawaziri.

Chukua hiyo.
 
Akitambua uwepo wa viongozi na waalikwa katika Mkutano wa wa 15 wa Baraza la Taifa la Biashara, Rais Samia kaanza kwa kutambua uwepo wa Makamu wa Rais kisha Rais wa Zanzibar na baada ya hapo ndio akamataja Waziri Mkuu wa Tanzania, Bwana Kassimu Majaliwa na kisha akaendelea kutaja wageni wengine waliokuwa wamehudhuria katika tukio hilo.

Swali langu ni je, kati ya Raisi wa Zanibar na Waziri Mkuu wa Tanzania, ni nani mwenye cheo kikubwa?

Zanzibar si ni sehemu ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, sasa iweje Rais wa Zanzibar ambae ni sehemu tu ya Muungano awe juu ya Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania?
Kwani katiba iliyozeeka si inasema serikali 2? Basi Boss ni majaliwa. Kama Mpango ni Rais wa Tanganyika na Mwinyi Rais wa Zanzibar basi yuko sahihi kiprotokali.
 
Mpango kasoma HGE sijui analytical skills kapata wapi mana hajasoma advanced maths. Na mi navyojua kama hijasoma maths akili huna

lkn CV yake inasema alikuwa Top economist wa World Bank, hivyo inapingana na ulichokisema …
 
Zamani vilaza si walikiwa wanavhukuliwa tubmana wasomi walikuwa wachache.

senior economist wa World Bank utachukuliwa tu kivipi? Nani anafanya vetting ili uajiriwe World Bank kama economist?
 
Mbona hata mwigulu nchemba ni first economist japo hana akili kabisa

well, i dont know about that, sijawahi kusikia kwamba Mwigulu aliwahi kuwa Top Economist wa World Bank au any international organization/Company …
 
Akitambua uwepo wa viongozi na waalikwa katika Mkutano wa wa 15 wa Baraza la Taifa la Biashara, Rais Samia kaanza kwa kutambua uwepo wa Makamu wa Rais kisha Rais wa Zanzibar na baada ya hapo ndio akamataja Waziri Mkuu wa Tanzania, Bwana Kassimu Majaliwa na kisha akaendelea kutaja wageni wengine waliokuwa wamehudhuria katika tukio hilo.

Swali langu ni je, kati ya Raisi wa Zanibar na Waziri Mkuu wa Tanzania, ni nani mwenye cheo kikubwa?

Zanzibar si ni sehemu ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, sasa iweje Rais wa Zanzibar ambae ni sehemu tu ya Muungano awe juu ya Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania?
Yupo sahihi. Zanzibar ni nchi kamili isiyokuwa na dola kamili tu. Majaliwa ni Mkuu wa Nchi ya Tanganyika ambayo ipo kivulini na isiyokuwa na dola kama ilivyo kwa Zanzibar. Hivyo, Rais wa Zanzibar ni Mkubwa kuliko Mkuu wa nchi iliyokivulini. Mamlaka ya Waziri Mkuu wa Tanzania yanaishia pare Feri na Kigamboni. Kule Zanzibar hana mamlaka yoyote. Akiende Zanzaibar labda aende kibinafsi tu au ziara za ujirani mwema kama vile ameenda nchi jirani.
 
Sifahamu kuhusu hilo lakini nawashangaa wanaouliza. Hivi wanafikiri Rais anajipangia yeye protocol? Hawaelewi kuwa kuna Ofisi nzima ya Rais ina wataalam wa kila aina?

Unajuwa mtu mweusi alijaaliwa akili nyingi sana lakini tatizo ni kajazwa ujinga mpaka akaamini kuwa yeye ni mjinga, matokeo? Hajuwi kuzitumia akili zake.
.
Ushasema hufahamu kuhusu hilo na bado unalizungumzia

Pole kwa kutojua kutumia akili zako
 
Waziri Mkuu kikatiba ni mkubwa kuliko rais wa Zanzibar.
Hizo zinafanyikan zinafanyikan makusudi kabisa ku mo overate Rais wa Visiwabvya Zanzibar ambavyo sawa na wilaya Moja huku Bara.

Mamlaka ya Waziri Mkuu, kwenye Baraza la MAWAZIRI ,
Ibara ya 50, kifungu kidogo Cha (I) na Cha (ii) kinaonesha vizuri sana, kwamba KUTAKUWA NA BARAZA LA MAWAZIRI,

Linaundwa na Rais wa URT nayae atakuwa Mwenyekiti, asipokuwepo Makamu wa Rais.

Ikitokea Rais na makamu kwa pamoja hawapo,waziri Mkuu ataongoza kikao Cha Baraza la MAWAZIRI.

Wajumbe wanaounda Baraza la MAWAZIRI.

Mosi Rais, Mbili Makamu, tatu Waziri Mkuu.
Nne MAWAZIRI wote kamili sio manaibu,ni wajumbe, na Rais wa Zanzibar ni mjumbe tu,akiwa anaingia baraza la mawaziri hadhi yake ni sawa na Innocent Bashungwa au Masauni.

Nyongeza ikitokea Rais hayupo nchini Rungu anashiklia Makamu wa Rais, asipokuwepo yeye pia, Rungu atashika waziri Mkuu, naye asipokuwepo atashika speaker wa Bunge, na ikitokea wote hao hawapo kwa pamoja nchi itakuwa chini ya jaji mkuu!

Hapo Rais wa Zanzibar hatajwi.

Kumruka waziri mkuu au waziri mkuu kutangulia kuingia kwenye sherehe za kitaifa katika accending order na descending order yaani order of seniority ni JANJAJANJA tu ya makusudi inayofanyika.

Lakini ni ukiukwaji wa katiba mchana kweupe.

Hayo yanatosha kuelewa hata kwa mwanafunzi wa elimu ya Uraia Civics kuelewa kuwa waziri mkuu ni Mtu Mkubwa sana katika nchi kimamlaka na protocal akiwa chini ya Makamu wa Rais.

Kwahiyo kumdogosha waziri mkuu ni mbwembwe na janjajanja flani ya makusudi.

😅🤔🙏
Inategemea unaongelea nchi gani. Kama unaongelea Tanganyika yenye jina ubatizo la Tanzania upo sahihi. Lakini kama unaongelea Jamhuri ya Muungano wa Tanzania basi Rais wa Zanzibar mkubwa maana ile ni nchi kamili iliyotetea uhai wake ndani ya muungano tofauti na Tanganyika iliyolalaa fofofo na kuporwa mamlaka yake. Kifalsafa Waziri Mkuu ni Mkuu wa Nchi ya Tanganyika.

Hii nchi ngumu sana! Tuendelee kufurahia maisha yetu.
 
Yupo sahihi. Zanzibar ni nchi kamili isiyokuwa na dola kamili tu. Majaliwa ni Mkuu wa Nchi ya Tanganyika ambayo ipo kivulini na isiyokuwa na dola kama ilivyo kwa Zanzibar. Hivyo, Rais wa Zanzibar ni Mkubwa kuliko Mkuu wa nchi iliyokivulini. Mamlaka ya Waziri Mkuu wa Tanzania yanaishia pare Feri na Kigamboni. Kule Zanzibar hana mamlaka yoyote. Akiende Zanzaibar labda aende kibinafsi tu au ziara za ujirani mwema kama vile ameenda nchi jirani.
Rais wa Zanzibar ni mjumbe wa kawaida kabisa kwenye Baraza la MAWAZIRI, ambacho ni chombo kikubwa Cha maamuzi ya mhimili Excutive.

Rais wa Zanzibar akiwa pale ni sawa na BASHE,BASHUNGWA,SIMBACHAWENE,JENESTER MHAGAMA,MWIGULU NCHEMBA.

But waziri mkuu ametamkwa na katiba aweza kuwa Mwenyekiti wa kikao Cha Baraza la MAWAZIRI endapo Rais na Makamu wa Rais hawapo wote kwa wakati mmoja.

BARAZA la MAWAZIRI ibara ya 50 kifungu kidogo Cha (I) ,(I I)

Rais wa ZANZIBAR ni mdogo kimamlaka kwenye Serikali.

Pia ikitokea Rais,makamu wa Rais kwa pamoja hawapo ndani ya mipaka ya TZ , Waziri Mkuu atakaimu na kuongoza serikali mpaka pale matairi ya ndege ya ya Rais au Makamu yanapogusa ardhi ya Tz, kukaimu kwake kunakoma.

Ikitokea pia Rais, Makamu waziri mkuu kwa pamoja hawapo, inashuka kwa speaker wa Bunge naye pia asipokuwepo inashuka kwa jaji mkuu!

Whre is president of Zanzibar???

Kwanini haitokei kukaimu au kuongoza Baraza la MAWAZIRI??

Hiyo ni ushuhuda tosha sana wa kuwa WAZIRI MKUU NI MKUBWA SANA KWENYE MUUNDO WA SERIKALI NA kwenye ku excute power, tofauti na RAIS ambaye anaongoza nchi inayofanana na wilaya ya Nachingwea,Kilwa.

🙏🙏
 
KATIBA SURA YA PILI(SERIKALI) wanaohusika na mamlaka ya serikali ya jamuhuri ya muungano:
-raisi wa jamuhuri
-makamu wa jamuhuri
-raisi wa Zanzibar
-waziri mkuu wetu.
NA HIYO NDIYO PROTOKALI MAANA YAKE.BUT ZANZIBAR TUMEWAMEZA.ukichek hata kiulinzi,mkuu wa jeshi Zanzibar ana cheo cha brigedia generali hivi na anaripoti kwa CDF bara,the same mkuu wa polisi Zanzibar ana cheo cha kamishna na anaripoti kwa IGP bara.ahsante
Zanzibar haina Jeshi. Masuala na Ulinzi na Usalama ni la Muungano. Hivyo Zanzibar haina Mkuu wa majeshi na Mkuu wa Polisi. Kiulizni zile ni kanda maalum yenye hadi ya Mkoa.
 
Zanzibar ni nchi kamili. Siyo Wilaya.
Ilikuwa nchi kabla ya kuanza kutawaliwa na bara, ,haina hata uwezo wa kuchukua mikopo au Treasury bonds kubwa bila kupitia mwavuli wa bara.

Ukubwa wa Zanzibar ni kama wilaya Moja ya Bara,
Ni chungu kumeza,lakini mezani tu hamna jinsi
 
Ilikuwa nchi kabla ya kuanza kutawaliwa na bara, ,haina hata uwezo wa kuchukua mikopo au Treasury bonds kubwa bila kupitia mwavuli wa bara.

Ukubwa wa Zanzibar ni kama wilaya Moja ya Bara,
Ni changu kumeza,lakini mezani tu hamna jinsi
Sahihi kabisa maana nchi isiyokuwa na dola haiweai kuwa na uwaklilishi nchi ya mipaka yake. Lakini ili kuwa nchi haipimwi kwa ukubwa wa eneo. hata Rwanda ni ndogo kuliko Wilaya ya Sikonge kule Tabora.
 
Huwa unaangalia maadhimisho ya sikuku ya Mapinduzi??? Yule anayepigiwa mizinga 21 ni rais wa nchi gani??
 
Back
Top Bottom