Rais Samia: Tuko vizuri kisiasa lakini mwenzetu mmoja anaendelea kutafakari, Tunaendelea kupokea matakwa yake

Rais Samia: Tuko vizuri kisiasa lakini mwenzetu mmoja anaendelea kutafakari, Tunaendelea kupokea matakwa yake

Rais Samia katika kikao na vyama vya siasa leo Julai 30, 2026 amesema hali ya kisiasa nchini inaendelea kuwa nzuri, akibainisha kuwa licha ya hali hiyo, bado kuna upande mmoja ambao unaendelea kutafakari msimamo wake kuhusu masuala ya kisiasa

Kwa upande mwingine kisiasa kama mnavyoona tuko vizuri."

Tuko vizuri lakini mwenzetu mmoja bado anaendelea kutafakari."

Tunaendelea kupokea misukumo yake, condition zake, matakwa yake. Tunaendelea na ndio mambo yanavyoendeshwa kwenye nchi."


Soma Pia: Rais Samia: Wananchi hawaitaji vurugu. Kwenye Siasa za chuki na mivutano maendeleo hutoweka

 

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, leo Julai 30, 2026, amekutana na viongozi wa vyama vya siasa Ikulu jijini Dar es Salaam na kueleza kuwa hali ya kisiasa nchini inaendelea vizuri na kuimarika isipokuwa bado bado serikali inaendelea kupokea matakwa kwa mmoja wa wanasiasa aliyepo gerezani

Akigusia masuala ya kisiasa, Rais Samia amebainisha kuwa serikali inaendelea na mazungumzo pamoja na kupokea maoni na masharti kutoka kwa wadau mbalimbali ili kuendesha nchi kwa maridhiano, huku akipongeza hatua kubwa iliyopigwa pande za Zanzibar kupitia msaada wa marais wastaafu.

Aidha, amesisitiza kuwa baada ya kukamilisha utekelezaji wa makubaliano yaliyosainiwa kuhusu mwelekeo wa nchi, hatua inayofuata itakuwa ni kushughulikia kikamilifu mchakato wa Katiba Mpya.

"Kisiasa, kama mnavyoona, tuko vizuri. Tuko vizuri lakini mwenzetu mmoja bado anaendelea kutafakari. Tunaendelea kupokea misukumo yake, condition zake, matakwa yake... tunaendelea. Na ndio mambo yanavyoendeshwa kwenye nchi."
 
Leo majira ya mchana maamuzi ya maombi ya marejeo ( Revision) yaliyofunguliwa na DPP dhidi ya Tundu Antipas Lissu, katika mahakama ya rufaa yamesoma na Lissu ameshinda.

Sasa ni mawili; turudi mahakama kuu kuendelea na tulipoishia kwenye kesi ya uhaini, au waifute na kumwachia huru Tundu Antipas Lissu.

Kumbuka hata tukirudi na kuendelea na kesi hii ya uhaini mahakam kuu lakini ushahidi wake muhimu ulishakataliwa na mahakama.
 
Rais Samia katika kikao na vyama vya siasa leo Julai 30, 2026.

View attachment 3640175
well done Dr. Samia Suluhu Hassan,
unafanya kazi nzuri sana ya kuwatumikia wananchi na waTanzania wote.

Tupo nyuma yako na tutallinda taifa letu kwa wivu mkubwa, kwa nguvu na gharama yoyote ile.

huyo moja hata asikusumbue, ni kibaraka huyo ametumwa tunamjua vizuri sana 🐒
 
Leo majira ya mchana maamuzi ya maombi ya marejeo ( Revision) yaliyofunguliwa na DPP dhidi ya Tundu Antipas Lissu, katika mahakama ya rufaa yamesoma na Lissu ameshinda.

Sasa ni mawili; turudi mahakama kuu kuendelea na tulipoishia kwenye kesi ya uhaini, au waifute na kumwachia huru Tundu Antipas Lissu.

Kumbuka hata tukirudi na kuendelea na kesi hii ya uhaini mahakam kuu lakini ushahidi wake muhimu ulishakataliwa na mahakama.

Wanavuta muda tu. Sharti walilopewa ni simple. Waimalize kesi kiaiasa au kisheria.
 
Screenshot_20260730_194045_WhatsApp.jpg
 
Kweli huyu tobo kisu ni haambiliki ;

Wenzake wote wapo hapo kwa maslahi ya nchi Chama chake tu ndio kikwazo.

Wao ndio wenye umuhimu kuliko wengine, wasikilizwe wao tu kwenye kila jambo.

Wasitucheleweshe kwenye mambo mazuri ni kuwaacha wabakie hivyo walivyo na ukaidi wao.
 
Back
Top Bottom