Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amesema viwanja vya kufurahisha watoto vilivyojengwa Kizimkazi, Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar, vinapaswa kuwa sehemu salama ya watoto kujifunza, kucheza na kufurahia, na si kuwa chanzo cha kuwaharibu.
Rais Samia ameyasema hayo leo, Agosti 12, 2026, wakati wa ufunguzi wa Viwanja vya Kufurahisha Watoto vya Kizimkazi, Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar.
"Ndugu viongozi na wananchi wenzangu michezo ina umuhimu katika malezi na makuzi ya watoto wetu".
Alieleza kuwa kupitia michezo, watoto hujifunza tabia njema, ubunifu, nidhamu, heshima, na ushirikiano, ambavyo ni vichocheo vya kujenga utu na uwezo wa kuchangamana na wengine.
Kiwanja hiki kisiwe chanzo cha kuharibu watoto