Rais Samia: Kodi ndio Damu ya Serikali

Kwa hii Serikali ya sasa, utekaji na mauaji ya wakosoaji, ndiyo damu ya Serikali.
 
Watanzania wanalipa kodi wakibananishwa, kwa sababu wanaona dhahiri serikali haipo kwaajili ya ustawi wao. Kodi yao inafisadiwa, na hakuna anayeadhibiwa. Kodi yao inatumika kuwalipa watekaji na wauaji, huku serikali ikidai haina hela za kuwaajiri madaktari, wauguzi na walimu. Kodi yao inatumika hovyo kununua magoli na kuwalipa wasanii machawa, huku walipa kodi wakiogelea kwenye umaskini na huduma duni.

Watanzania wataendelea kulipa kodi kwa kubananishwa, ni pale ambapo hakuna namna ya kukwepa, mpaka siku ambayo watawala watakapoelewa kuwa kodi ni pesa ya wananchi, siyo ya Rais Samia au waziri Mwigulu, na hivyo inatakiwa kuheshimiwa na kuthaminiwa; siyo kama ilivyo sasa ambapo kodi ya watanzania inaonekana ni pesa isiyo na mwenyewe!!
 
Uchawa uliopitiliza huleta kichaa unashangaa wafanyabiashara kutolipa kodi mbona hushangai Raisi kutolipa kodi kwenye mapato yake? Mnafiki mkubwa wewe

Yeye damu yake kwenye kodi iko wapi kama kodi ndio damu ya serikali?
Alipe kofi asihubiri kitu ambacho yeye hafanyi abahimiza watu kulipa kodi wakati yeye halipi kodi

Vipi chawa unasemaje kuhusu hilo la Raisi kutolipa kodi kwenye mapato yake halafu anasukumizia watanzania wengine kuwa wawe na moyo wa kulipa kodi
 
Serikali na kodi... Mfumo wa wazi wa wizi na unyonyoji!
 

Mmmmhhhh mbona kila siku wanasema hela ni yako ni ni wewe unatoa na kufanya sasa hii kodi yetu unaitakia kwa kazi gani????[emoji15][emoji15][emoji15][emoji15]
 

Sijui inaweza ikawaje iwapo wote tutaiga na kutekeleza mfano wa boss wetu pamoja na wabunge wetu wa kutolipa kodi
 
Wewe kiongozi mkuu hulipi kodi kila kitu bure halafu na una pato la kufuru,unahamasisha watu waliona na kipato Duni ndio walipe kodi.hii sijaielewa kabisaa
Yaani wanasiasa pamoja na mishahara mikubwa na marupurupu manono eti wao hawalipi kodi. Hata tozo za miamala ya simu nasikia haziwagusi baadhi yao kama si wote. Mimi Mwl wa 700K kwa mwezi najikuta takribani 200K imefyekwa na serikali ikiwa ni kodi na makato kibao. Nchi ngumu sana hii.
 
Lipeni kodi serikali ikanunue cruser na prado new model zilizotoka. Hiyo ndo kazi wanayoijua.
Yaani usikute washaweka oda kila mwaka watengewe vinu vinane kadhaa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…