Wakuu Kazi Iendeleee.
Taarifa Zilizopo Ni Kwamba Rais Samia Ana Ziara Ya Kikazi Nchini Congo.
Ataanza Ziara Hyo Wakati atakapotoka Zambia Kwenye Inauguration ya HH.
Akifika Congo atapokekewa na Mwenyeji Wake Rais Felix Tshisekedi.
Hakika Ziara zimeanza na Zimetaradadi
Hii ziara inaweza kuwa ya kimkakati na ya muhimu pengine kuliko ziara zote zilizofanyika toka mama aingie ikulu. Ni jambo la wazi kuwa katika nchi zote za maziwa makuu, DRC imejaaliwa kuwa na idadi kubwa ya watu takriban watu 120,000,000.
Itakumbukwa kuwa Tanzania tumejaaliwa kuwa na bandari, ambapo miongoni mwa nchi zinazotumia bandari yetu ni DRC.
Tanzania imekuwa ujenzi mkubwa wa reli ya mwendokasi ambayo inategemewa kuwa msaada mkubwa wa usafirishaji wa watu na mizigo kuelekea nchi za Rwanda, Burundi na DRC. Kimkakati, kama ujenzi huo utakamilika, Tanzania itakuwa imalamba dume kwa sababu tutaweza kujiinua kiuchumi kupitia sekta ya usafirishaji pamoja na kufaidika na masoko ya bidhaa zetu kupitia wato miliuoni miamoja waliopo mashariki mwa Kongo.
Mnyonge mnyongeni lakini haki haki yake apewe. Ziara ya Rais wetu huko DRC haipaswi kubezwa kwa sababu kiuchumi inalipa tofauti na nchi kama Rwanda, Burundi na Uganda ambazo zinapitisha mizigo yao katika bandari yetu ya Dar Es Salaam lakini, mizigo yao kidogo kuliko ile DRC kutokana na idadi ya watu katika nchi hizo ni ndogo.
Hongera Mh. Raisi wetu kwa kupanga ziara ya kimkakati ya DRC ambayo ni muhimu sana kwa musakabali wa uchumi wa nchi yetu.