Rais Samia kuanza safari ya kikazi nchini DR Congo

Rais Samia kuanza safari ya kikazi nchini DR Congo

Mimi ninavyojua wanawake wa kizanzibari kwa kuzulula hawajambo.
Uwe na heshima mkuu...

Ikiwa mama yako mzazi unamheshimu....basi hebu heshimu mama wa wenzako tena Amiri Jeshi Wa Majeshi ya Ulinzi.....

Siasa "koko" ziendane na UTU WETU WA KIAFRIKA......
 
Kwa kweli, hapa ndipo anapopamudu vilivyo. Sijui tuishije mpaka hiyo 2025! Hapa tumeula wa chuya.
 
Hii ziara inaweza kuwa ya kimkakati na ya muhimu pengine kuliko ziara zote zilizofanyika toka mama aingie ikulu. Ni jambo la wazi kuwa katika nchi zote za maziwa makuu, DRC imejaaliwa kuwa na idadi kubwa ya watu takriban watu 120,000,000.

Itakumbukwa kuwa Tanzania tumejaaliwa kuwa na bandari, ambapo miongoni mwa nchi zinazotumia bandari yetu ni DRC.

Tanzania imekuwa ujenzi mkubwa wa reli ya mwendokasi ambayo inategemewa kuwa msaada mkubwa wa usafirishaji wa watu na mizigo kuelekea nchi za Rwanda, Burundi na DRC. Kimkakati, kama ujenzi huo utakamilika, Tanzania itakuwa imalamba dume kwa sababu tutaweza kujiinua kiuchumi kupitia sekta ya usafirishaji pamoja na kufaidika na masoko ya bidhaa zetu kupitia wato miliuoni miamoja waliopo mashariki mwa Kongo.

Mnyonge mnyongeni lakini haki haki yake apewe. Ziara ya Rais wetu huko DRC haipaswi kubezwa kwa sababu kiuchumi inalipa tofauti na nchi kama Rwanda, Burundi na Uganda ambazo zinapitisha mizigo yao katika bandari yetu ya Dar Es Salaam lakini, mizigo yao kidogo kuliko ile DRC kutokana na idadi ya watu katika nchi hizo ni ndogo.

Hongera Mh. Raisi wetu kwa kupanga ziara ya kimkakati ya DRC ambayo ni muhimu sana kwa musakabali wa uchumi wa nchi yetu.

Acheni ujanja ujanja. Mmesharudi kwenye upigaji wenu.
 
DR Congo ni mshirika no 1vwa bandari na maendeleo ya uchumi hapa nchini twende takwimu utaona ni vyema sana tuimarishe mahusiano ili waongeze mizigo kupitia dar
 
Burundi ina mchango mdogo wa uchumi kwetu?

Kenya na Rwanda zina mchango mdogo kwa uchumi wetu?

Hivi yale magari 3000 yaliyopokelewa bandarini YANAPEKEKWA "huko Ulaya usemako"?

Ulaya waje kuwekeza kitu gani?!

Kwa hiyo "REGIONAL ECONOMY" kwako ni kupoteza muda? 😲😲

#NchiKwanza
#KaziIendelee
#SiempreJMT
Umenena Mkuu, shida ni kila kitu kupinga na kuonyesha ujuaji, Nchi hizi zina umuhimu mkubwa kiuchumi hasa katika matumizi ya Bandari zetu ambazo ndio backbone ya uchumi, wakumbuke kuwa tozo na kodi zinazotozwa kupitia bandari ndio zinamchango mkubwa katika kufikia target ya ukusanyaji wa mapato,pia tupo na ushindani mkubwa na bandari za mombasa,beira na durban,pia kimkakati Rais wa nchi anapokuwa karibu na kufanya ziara husika kwa nchi husika inabadilisha mambo mengi sana na kwakutatua kero hurudisha imani za wafanyabiashara wa pande hizo mbili.Hivyo ninassuport ziara hizi za kimkakati.
 
Uchaguzi Mkuu wa 2020 ulishatoa majibu ya haya maswali. Vinginevyo ni kusukuma muda na kusubiri majibu ya maswali hayo 2025.
Hakuna uchaguzi uliofanyika 2020.Kilichofanyika ulikuwa ni uchafuzi wa vyombo vya dola kuisadia CCM kubakia madarakani baada ya kugundua kuwa ni chama ambacho kilishakufa siku nyingi sana.

Walichofanya CCM ni kupora uchaguzi kwa kutumia mabavu ili waendelee kutawala.Kwa lugha nyepesi CCM waliiba kura mchana kweupe bila soni wala aibu machoni.CCM ni chama kinachotawala Tanzania bila kibali cha wananchi.

109_20210724_194836.jpg

109_20210724_194739.jpg
109_20210724_194857.jpg
 
Umenena Mkuu, shida ni kila kitu kupinga na kuonyesha ujuaji, Nchi hizi zina umuhimu mkubwa kiuchumi hasa katika matumizi ya Bandari zetu ambazo ndio backbone ya uchumi, wakumbuke kuwa tozo na kodi zinazotozwa kupitia bandari ndio zinamchango mkubwa katika kufikia target ya ukusanyaji wa mapato,pia tupo na ushindani mkubwa na bandari za mombasa,beira na durban,pia kimkakati Rais wa nchi anapokuwa karibu na kufanya ziara husika kwa nchi husika inabadilisha mambo mengi sana na kwakutatua kero hurudisha imani za wafanyabiashara wa pande hizo mbili.Hivyo ninassuport ziara hizi za kimkakati.
Huo ndio ukweli usiohitaji KUMULIKWA NA TOCHI.....

Swadakta mkuu wangu 👍👊

#NchiKwanza
#KaziIendelee
 
Kukubali chanjo ya J & J kumetupa kiasi gani cha hela!!??
Huko ni kupiga magoti ama ni kupiga "makofi"!!??
Mkopo wa 2.7 tirioni,tumepewa kutokana na mahusiano mema ya " regional intergration" ama nini!!??
Tulikataa mkopo wa masharti nafuu na "riba free" ya "Covax", leo tumekubali mkopo wenye riba wa "2.7 tirioni" , hiyo ni akili ama matope!!???
Hili la propaganda za chanjo hata mimi limenichanganya, tungeendelea na msimamo wetu ingekuwa poa sana kwa maoni yangu. Pia hakuna kitu kinachonikera kama haya mamikopo wakati tuna rasilimali nyingi ambazo tukizisimamia vizuri tunatoboa.
 
Wewe sukule,yaani unakubali kumpa hela baba yako ambayo una uhakika wa asilimia 200 kuwa ataenda kuhonga mwanamke au kunywea pombe kisa ni baba yako nawe ni mtoto!!???
Hao wanao waletea hizo pesa kutoka huko nje mnadhani wanaokota!? Ni tozo za watu wao nanyi mnazipokea kama msaada au hata hao akina TOBO huko Ulaya mnadhani wanaishi kwa pesa zipi!? Ni hizo hizo kama TOZO hii mnayopinga kwa nguvu na mapovu ya ajabu. Au hao ni baba zenu au wajomba wenu au mama zenu!?
 
Hakuna uchaguzi uliofanyika 2020.Kilichofanyika ulikuwa ni uchafuzi wa vyombo vya dola kuisadia CCM kubakia madarakani baada ya kugundua kuwa ni chama ambacho kilishakufa siku nyingi sana.

Walichofanya CCM ni kupora uchaguzi kwa kutumia mabavu ili waendelee kutawala.Kwa lugha nyepesi CCM waliiba kura mchana kweupe bila soni wala aibu machoni.CCM ni chama kinachotawala Tanzania bila kibali cha wananchi.
View attachment 1907170View attachment 1907171
View attachment 1907169
View attachment 1907173View attachment 1907178
Nakumbuka kusikia argument na uzushi kama huu kutoka kwa TOBO. Nothing is new here, haya ni marudio ya maubishi yale yale ya siku zote na wengine ninyi ni kama LOUDSPEAKERS TU!
 
Nakumbuka kusikia argument na uzushi kama huu kutoka kwa TOBO. Nothing is new here, haya ni marudio ya maubishi yale yale ya siku zote na wengine ninyi ni kama LOUDSPEAKERS TU!
Kwa nini unadai kuwa ni uzushi wakati hapo tunaona kabisa polisi wakikamata kura fake na hata kumpiga waliomkamata nazo?
 
Kwa nini unadai kuwa ni uzushi wakati hapo tunaona kabisa polisi wakikamata kura fake na hata kumpiga waliomkamata nazo?
Pelekeni hiyo au hayo madai na huo ushahidi kwa PILATO ili mpate haki yenu. Hili la kuandika humu JF na kubishana na akina CHIEF MASALAKULANGWA na wengine haisaidii ninyi kupata haki zenu.
 
Wakuu Kazi Iendeleee.

Taarifa zilizopo ni kwamba Rais Samia ana ziara ya kikazi nchini Congo.

Ataanza ziara hiyo wakati atakapotoka Zambia kwenye inauguration ya Hakainde Hichilema.

Akifika Congo atapokekewa na Mwenyeji Wake Rais Felix Tshisekedi.

Hakika Ziara zimeanza na Zimetaradadi
Ofcoz, Rais kufanya ziara za kikazi ktk mataifa mengine ni muhimu sana...

Lakini lililo muhumu zaidi ni kuwa, lazima ziara hizo ziwe za kimkakati zaidi zikibebwa na falsafa ya intelejensia ya uchumi...

Mathalani Rais kuitembelea DRC ni muhimu sana kiuchumi kwa sababu nchi hiyo ni miongoni mwa wadau wakuu na muhimu sana wa bandari yetu ya DSM na inayotaka kuanza kujengwa, bandari ya Bagamoyo...

Kwa hiyo, aende huko haraka iwezekanavyo...
 
Ofcoz, Rais kufanya ziara za kikazi ktk mataifa mengine ni muhimu sana...

Lakini lililo muhumu zaidi ni kuwa, lazima ziara hizo ziwe za kimkakati zaidi zikibebwa na falsafa ya intelejensia ya uchumi...

Mathalani Rais kuitembelea DRC ni muhimu sana kiuchumi kwa sababu nchi hiyo ni miingoni mwa wadau wakuu na muhimu wa bandari yetu ya DSM na inayitaka kuanza kujengwa Bagamoyo...

Kwa hivyo, aende tu...
Ila kwa hili la Bandari ya Bagamoyo binafsi SIKUBALIANI na wewe au yeyote anaye lipigania. Endelezeni bandari zilizopo kwa manufaa ya nchi hii na SIYO kwa manufaa ya wapigaji wachache.
 
Back
Top Bottom