PreGE2025 Rais Samia kuboresha taarifa zake awamu ya pili inamaanisha yeye mwenyewe haamini kama atatoboa?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, amesema kuwa kutokujitokeza kujiandikisha au kuhuisha taarifa katika Daftari la Kudumu la Mpiga Kura ni sawa na mtu kukataa haki yake ya kikatiba kwa hiari, jambo ambalo siyo uzalendo.

Rais Samia ameyasema hayo leo Jumamosi Mei 17, 2025 mara baada ya kuhuisha taarifa zake kwenye daftari hilo katika Kata ya Chamwino, Jijini Dodoma, ambapo pia amezungumza na wananchi waliokusanyika kwenye kituo cha uandikishaji.

"Kutokujitokeza kujiandikisha ni kukataa mwenyewe haki yako ya kikatiba na unapokataa haki ya Kikatiba jiulize je wewe ni mzalendo? Mzalendo wa aina gani ambaye Katiba imekupa fursa nenda kajiandikishe, piga kura, weka kiongozi unayehisi atakuja kukuhudumia, wewe unaikataa, ukiikataa wenzio wataenda kuweka wanayemtaka na utakosa fursa ya kushawishi wengine kuweka yule mnayemtaka kwahiyo unakuwa wewe wa kubabaisha tu na kulalamika. Hii ni fursa kubwa inatokea kila baada ya miaka mitano, haiji kila siku kwahiyo ni vyema kila Mtanzania ajitokeze atumie fursa hii." Amesema Rais Samia.

Amesema kuwa ameamua kuungana na wananchi wa Chamwino katika mchakato huo kwa kuwa yeye ni mkazi wa eneo hilo, na mwaka huu atapiga kura katika kata hiyo. Aidha, ameongeza kuwa amerekebisha taarifa zake ili kuhakikisha kuwa yuko tayari kushiriki katika uchaguzi ujao.

Rais Samia amewakumbusha wananchi kuwa huu ni mzunguko wa pili wa uandikishaji na uhuishaji, na baada ya awamu hii hakutakuwa na nafasi nyingine ya kujiandikisha, hivyo ni muhimu kutumia fursa hii kikamilifu.

Ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi na pia kuwahamasisha wengine kushiriki katika zoezi hilo muhimu. “Tuonyeshe uzalendo, tujitokeze kwa wingi, na pia tuwe wavumilivu pale changamoto zinapojitokeza,” amesema Rais Samia.

Amebainisha kuwa Serikali imeweka mipango mizuri kuhakikisha kila anayefika kituoni anaandikishwa, na hivyo hakuna sababu ya mtu kubaki nyuma.

Zoezi la kujiandikisha na kuhuisha taarifa linaendelea katika maeneo mbalimbali nchini, likiwa ni hatua muhimu kuelekea uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu.

Kwa maana sahihi ni kwamba kuiba kura ndio sahihi.
 
Uzalendo ni kuipenda Nchi yako, hata ikikupasa kuweka maisha yako hatarini kuitetea kisiasa, kiuchumi, kiulinzi na kijamii. Na siyo kuipenda Serikali au chama Fulani au MTU Fulani.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, amesema kuwa kutokujitokeza kujiandikisha au kuhuisha taarifa katika Daftari la Kudumu la Mpiga Kura ni sawa na mtu kukataa haki yake ya kikatiba kwa hiari, jambo ambalo siyo uzalendo.

Rais Samia ameyasema hayo leo Jumamosi Mei 17, 2025 mara baada ya kuhuisha taarifa zake kwenye daftari hilo katika Kata ya Chamwino, Jijini Dodoma, ambapo pia amezungumza na wananchi waliokusanyika kwenye kituo cha uandikishaji.

"Kutokujitokeza kujiandikisha ni kukataa mwenyewe haki yako ya kikatiba na unapokataa haki ya Kikatiba jiulize je wewe ni mzalendo? Mzalendo wa aina gani ambaye Katiba imekupa fursa nenda kajiandikishe, piga kura, weka kiongozi unayehisi atakuja kukuhudumia, wewe unaikataa, ukiikataa wenzio wataenda kuweka wanayemtaka na utakosa fursa ya kushawishi wengine kuweka yule mnayemtaka kwahiyo unakuwa wewe wa kubabaisha tu na kulalamika. Hii ni fursa kubwa inatokea kila baada ya miaka mitano, haiji kila siku kwahiyo ni vyema kila Mtanzania ajitokeze atumie fursa hii." Amesema Rais Samia.

Amesema kuwa ameamua kuungana na wananchi wa Chamwino katika mchakato huo kwa kuwa yeye ni mkazi wa eneo hilo, na mwaka huu atapiga kura katika kata hiyo. Aidha, ameongeza kuwa amerekebisha taarifa zake ili kuhakikisha kuwa yuko tayari kushiriki katika uchaguzi ujao.

Rais Samia amewakumbusha wananchi kuwa huu ni mzunguko wa pili wa uandikishaji na uhuishaji, na baada ya awamu hii hakutakuwa na nafasi nyingine ya kujiandikisha, hivyo ni muhimu kutumia fursa hii kikamilifu.

Ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi na pia kuwahamasisha wengine kushiriki katika zoezi hilo muhimu. “Tuonyeshe uzalendo, tujitokeze kwa wingi, na pia tuwe wavumilivu pale changamoto zinapojitokeza,” amesema Rais Samia.

Amebainisha kuwa Serikali imeweka mipango mizuri kuhakikisha kila anayefika kituoni anaandikishwa, na hivyo hakuna sababu ya mtu kubaki nyuma.

Zoezi la kujiandikisha na kuhuisha taarifa linaendelea katika maeneo mbalimbali nchini, likiwa ni hatua muhimu kuelekea uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu.

Pia Raia waambiwe na Haki nyengine isiwe Haki ya kupiga kura Tu!!
 
Nafikiri mama kuna kitu anakifanyia masihara kwa makusudi....
Hakuna mtu ambaye hapendi kwenda kupiga kura...ila hili limeanza baada ya wananchi kuona kura zao hazihwshimiwi....so wananchi wana wajibu na serikal.ina wajbu kulinda haki za raia....kama serikali haitekelezi wajbu wake basi hana haki ya kusema haya kwa maana yy pia ni sehemu ya kukwamisha watu kuwa wazalendo
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, amesema kuwa kutokujitokeza kujiandikisha au kuhuisha taarifa katika Daftari la Kudumu la Mpiga Kura ni sawa na mtu kukataa haki yake ya kikatiba kwa hiari, jambo ambalo siyo uzalendo.

Rais Samia ameyasema hayo leo Jumamosi Mei 17, 2025 mara baada ya kuhuisha taarifa zake kwenye daftari hilo katika Kata ya Chamwino, Jijini Dodoma, ambapo pia amezungumza na wananchi waliokusanyika kwenye kituo cha uandikishaji.

"Kutokujitokeza kujiandikisha ni kukataa mwenyewe haki yako ya kikatiba na unapokataa haki ya Kikatiba jiulize je wewe ni mzalendo? Mzalendo wa aina gani ambaye Katiba imekupa fursa nenda kajiandikishe, piga kura, weka kiongozi unayehisi atakuja kukuhudumia, wewe unaikataa, ukiikataa wenzio wataenda kuweka wanayemtaka na utakosa fursa ya kushawishi wengine kuweka yule mnayemtaka kwahiyo unakuwa wewe wa kubabaisha tu na kulalamika. Hii ni fursa kubwa inatokea kila baada ya miaka mitano, haiji kila siku kwahiyo ni vyema kila Mtanzania ajitokeze atumie fursa hii." Amesema Rais Samia.

Amesema kuwa ameamua kuungana na wananchi wa Chamwino katika mchakato huo kwa kuwa yeye ni mkazi wa eneo hilo, na mwaka huu atapiga kura katika kata hiyo. Aidha, ameongeza kuwa amerekebisha taarifa zake ili kuhakikisha kuwa yuko tayari kushiriki katika uchaguzi ujao.

Rais Samia amewakumbusha wananchi kuwa huu ni mzunguko wa pili wa uandikishaji na uhuishaji, na baada ya awamu hii hakutakuwa na nafasi nyingine ya kujiandikisha, hivyo ni muhimu kutumia fursa hii kikamilifu.

Ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi na pia kuwahamasisha wengine kushiriki katika zoezi hilo muhimu. “Tuonyeshe uzalendo, tujitokeze kwa wingi, na pia tuwe wavumilivu pale changamoto zinapojitokeza,” amesema Rais Samia.

Amebainisha kuwa Serikali imeweka mipango mizuri kuhakikisha kila anayefika kituoni anaandikishwa, na hivyo hakuna sababu ya mtu kubaki nyuma.

Zoezi la kujiandikisha na kuhuisha taarifa linaendelea katika maeneo mbalimbali nchini, likiwa ni hatua muhimu kuelekea uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu.

Hivi ataenda na Zanzbar kumpigia kura Rais wao?
 
Back
Top Bottom