Rais Samia kufanya ziara ya kikazi nchini Korea Kusini kuanzia Mei 31 - Juni 6

Rais Samia kufanya ziara ya kikazi nchini Korea Kusini kuanzia Mei 31 - Juni 6

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2022
Posts
28,722
Reaction score
20,610
Ndugu zangu Watanzania,

Taarifa inayoendelea kusambaa Duniani kwote na kugonga vichwa vya habari ,ni kuwa Rais wetu na Jemadari Wetu Daktari Samia Suluhu Hasssan anatarajia kufanya ziara nzito sana ya kikazi Nchini Korea ya Kusini. Ambapo huko anatarajiwa kufanya mazungumzo mazito sana na Rais wa nchi hiyo.

Ambapo ni katika ziara hiyo nzito Tanzania inatarajia kupata mkopo wa masharti nafuu wa kiasi cha Dola za kimarekani Billion 2.5 kwa ajili ya kuwekeza katika miradi ya maendeleo. Narudia kusisitiza hapa mkopo huo ni wa mashariti NAFUU na ambao utawekezwa katika miradi ya maendeleo.ikumbukwe kukopa siyo dhambi bali inategemea unakopa kwa ajili ya nini na mashariti ya mkopo yapoje .ndio maana nimesisitiza hapa kuwa mkopo huo ni wa masharti nafuu kabisa.

Lakini vilevile Rais wetu mpendwa atashiriki mkutano utakaowakutanisha viongozi wa nchi na serikali kati ya Korea na wale kutoka Afrika kuanzia Tarehe 4 June hadi Tarehe 6 June. Ambapo katika mkutano huo Rais wetu mpendwa atapata fursa ya kuhutubia mkutano huo na kushiriki mjadala mzito juu ya kuimarisha masuala ya usalama wa chakula na madini.

Mambo mengi na makubaliano mbalimbali yatashuhudiwa yakifanyika na kusainiwa katika ziara hiyo ya kihistoria kwa Rais wetu kipenzi kuanzia kilimo,madini ya kimkakati,masuala ya sanaa na utamaduni na mengine mengi sana. Ni ziara ambayo tunakwenda kupata na kufaidika na mambo mengi sana.

Lakini pia ziara hiyo itashuhudiwa na Dunia nzima Rais wetu mpendwa akipewa na kutunukiwa Udaktari wa Heshima,kwa kutambua mchango Chanya wa uongozi wake ulioleta mabadiliko chanya katika maeneo mbalimbali.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa,Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Taarifa inayoendelea kusambaa Duniani kwote na kugonga vichwa vya habari ,ni kuwa Rais wetu na Jemadari Wetu ea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Miaka ya 1960's nchi yetu ilikuwa inakaribiana kabisa kiuchumi na hiyo nchi!! Halafu leo hii tunachukua lidege likubwa, ndani likiwa limejaa wasanii! Kwenda kuomba mkopo wenye masharti nafuu!!

Aisee Waafrika bora mngeendelea tu kutawaliwa.
 
Tunamtakia Kila la heri Rais Samia kwenye ziara hiyo ya mdau Wetu muhimu wa Maendeleo Korea Kusini.

Ikiwezeoana Awapatanishe Kim wa North Korea na South Korea.
Mwanadiplomasia namba 1 na Bingwa wa Biashara na Uchumi 👇👇

Nawakumbusha tuu Samia Huwa hafanyi ziara za hasara,hapo anaenda kuvuna Mkopo nafuu wa kujengea SGR zaidi ya Trilioni 4.5👇👇
===
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mh. January Makamba amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuanza ziara ya siku sita nchini Korea Kusini kuanzia Mei 31 kwa mwaliko rasmi wa kiongozi mkuu wa taifa hilo.

Waziri Makamba ameyasema hayo wakati akizungumza na Waandishi wa habari kwenye ofisi za Wizara hiyo zilizopo Jijini Dar, ambapo amesema ziara ya Rais Dkt. Samia itakuwa na sehemu kuu mbili, moja ni ziara rasmi kati ya Serikali ya Tanzania na Korea, lakini la pili ni Rais Samia kuhudhuria mkutano mkuu wa nchi za Afrika na Korea utakaofanyika Juni 3 na Juni 4.

Waziri Makamba amesema katika ziara hiyo ya Rais Samia, Serikali ya Tanzania itaingia mikataba saba ukiwamo wa msaada na mkopo nafuu wa Dola za Marekani 2.5 bilioni kutoka katika Serikali ya Korea Kusini.

'Makubaliano hayo ni mapya ya ushirikiano wa maendeleo ya kati ya Serikali ya Tanzania na Korea na mkataba mkubwa kati ya mikataba saba Serikali itakayoingia na fedha hizi zitakwenda uboreshaji wa sekta ya elimu, afya na miundombinu' - Waziri Makamba.

Waziri Makamba ameitaja mikataba mingine itakayosainiwa ni pamoja na ushirikiano katika maendeleo ya uchumi wa buluu, kutambua vyeti ya mabaharia, tamko la pamoja la uanzishwaji wa majadiliano na mkataba wa ushirikiano wa kiuchumi.

Mingine ni hati ya makubaliano kati ya Taasisi ya Utafiti wa Madini Tanzania (GST) na Taasisi ya Sayansi na Miamba na Madini ya Korea, ushirikiano utakaojikita katika utafiti, uchoraji ramani, rasilimali na shughuli za maabara.

Mbali na hilo, Waziri Makamba amesema kutakuwa na hati ya makubaliano kati ya Wizara ya Madini ya Tanzania na Wizara ya Viwanda na Biashara ya Korea kuhusu ushirikiano wa kuchambua na kufanya utafiti wa madini mkakati.

Halikadhalika kutasainiwa mkataba wa makubaliano kati ya Shirika la Taifa la Madini (Stamico) na Shirika la Ukarabati wa Migodina Rasilimali za Madini la Korea.

Waziri Makamba amesema ziara hiyo, pia itaanzisha ushirikiano kati ya Chuo Kikuu cha Korea cha Usafiri wa Anga na Tanzania ili kuboresha soko la usafiri wa anga na uendeshwaji wa biashara ya sekta hiyo.
 
Back
Top Bottom