Rais Samia kufanya ziara ya kikazi nchini Korea Kusini kuanzia Mei 31 - Juni 6

Rais Samia kufanya ziara ya kikazi nchini Korea Kusini kuanzia Mei 31 - Juni 6

Hivi kwanini kiongozi wa China Urusi au Marekani na hata Brazil hawana ziara nyingi hivi kama hawa wa huku kwetu?
Au ndio huwa wanakwenda kuomba?
Tuliza kichwa na anza kufikiri kwa kutumia ubongo usitumie makalio kufikiri.Hizo nchi ukilinganisha na bongo ni sawa na kulinganisha mlima na kichuguu. Budget ya kwenu inategemea misaada kwa 99.9%, hizo nchi ulizozitaja hapo ndio zinazowapa hio misaada. Jitafakari kabla hujaandika pumba zako hapa.
 
Utakufa na wivu wako.
Wivu gani wewe!! Tanzania imejaariwa raslimali za kila aina! Ila kila siku viongozi wako wanahangaika tu kukopa hovyo, na pia kuwabebesha wananchi kodi na tozo zisizo na kichwa, wala miguu!!

Unafikiri wangekuwa wanabana matumizi na pia kudhibiti rushwa na upigaji! tungeendelea kuwa omba omba hata baada ya miaka zaidi ya 60 tangu tulipopata Uhuru?
 
Ndugu zangu Watanzania,

Taarifa inayoendelea kusambaa Duniani kwote na kugonga vichwa vya habari ,ni kuwa Rais wetu na Jemadari Wetu Daktari Samia Suluhu Hasssan anatarajia kufanya ziara nzito sana ya kikazi Nchini Korea ya Kusini. Ambapo huko anatarajiwa kufanya mazungumzo mazito sana na Rais wa nchi hiyo.

Ambapo ni katika ziara hiyo nzito Tanzania inatarajia kupata mkopo wa masharti nafuu wa kiasi cha Dola za kimarekani Billion 2.5 kwa ajili ya kuwekeza katika miradi ya maendeleo. Narudia kusisitiza hapa mkopo huo ni wa mashariti NAFUU na ambao utawekezwa katika miradi ya maendeleo.ikumbukwe kukopa siyo dhambi bali inategemea unakopa kwa ajili ya nini na mashariti ya mkopo yapoje .ndio maana nimesisitiza hapa kuwa mkopo huo ni wa masharti nafuu kabisa.

Lakini vilevile Rais wetu mpendwa atashiriki mkutano utakaowakutanisha viongozi wa nchi na serikali kati ya Korea na wale kutoka Afrika kuanzia Tarehe 4 June hadi Tarehe 6 June. Ambapo katika mkutano huo Rais wetu mpendwa atapata fursa ya kuhutubia mkutano huo na kushiriki mjadala mzito juu ya kuimarisha masuala ya usalama wa chakula na madini.

Mambo mengi na makubaliano mbalimbali yatashuhudiwa yakifanyika na kusainiwa katika ziara hiyo ya kihistoria kwa Rais wetu kipenzi kuanzia kilimo,madini ya kimkakati,masuala ya sanaa na utamaduni na mengine mengi sana. Ni ziara ambayo tunakwenda kupata na kufaidika na mambo mengi sana.

Lakini pia ziara hiyo itashuhudiwa na Dunia nzima Rais wetu mpendwa akipewa na kutunukiwa Udaktari wa Heshima,kwa kutambua mchango Chanya wa uongozi wake ulioleta mabadiliko chanya katika maeneo mbalimbali.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa,Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Duh!! Tulikuwa tunamkumbuka Magufuli nadhani sasa tutalazimika kumkumbuka hata Kikwete!
 
Balozi wetu huko Korea asingeweza kutoa hizo shukrani kwa Korea kwa msaada wa ujenzi wa hilo daraja?!.
 
Balozi wetu huko Korea asingeweza kutoa hizo shukrani kwa Korea kwa msaada wa ujenzi wa hilo daraja?!.
Toa ujinga wako hapa,Balozi ndio atakuwa na itifaki za Rais?

Balozi Huwa anaalikwa Kwa Niaba ya Rais kufanya state Visit?
 
Back
Top Bottom