Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 28,722
- 20,610
Ndugu zangu Watanzania,
Habari ni kuwa Rais wetu mpendwa na Jemedari wetu kipenzi cha watanzania Mheshimiwa Mama Samia Suluhu Hasssan anatarajia kufanya ziara ya kikazi nchini Uturuki kwa mualiko maalum wa Rais wa nchi hiyo Mheshimiwa Erdogan. Hii imeelezwa na waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa Mheshimiwa Januari Makamba.
Inaelezwa kuwa ziara hii inalenga kuimarisha mahusiano ya kidiplomasia,biashara,uchumi,siasa na masuala mengine mbalimbali.inaeleza ya kuwa akiwa nchini humo Mheshimiwa Rais atapata fursa ya kuhudhuria kongamano kubwa la biashara na uwekezaji litakalofanyika mji wa Instanmbul ,ambapo hapo Mheshimiwa Rais atakutana na wafanyabiashara na wawekezaji mbalimbali wakubwa.
Lakini pia Mheshimiwa Rais atakutana na makampuni makubwa 15,ambapo atatumia nafasi kuweza kuwashawishi kuja kuwekeza hapa nchini.imeelezwa pia ya kuwa imepita miaka 14 tangia Rais kutoka Tanzania kuitembelea nchi hiyo,lakini pia imepita miaka 7 tangia Rais wa nchi hiyo aje aitembelee Tanzania,ambapo mara ya mwisho ilikuwa ni 2017 wakati wa utawala wa hayati dkt John Pombe Magufuli.
Imeelezwa pia kuwa uturuki ni miongoni mwa nchi 20 zenye uchumi mkubwa hapa Duniani,na hivyo kuwa nchi muhimu katika kushirikiana nayo na kuweza kufaidika kwa fursa mbalimbali.lakini pia imeelezwa pia kuwa biashara na maingiliano ya nchi hizi mbili yameongezeka sana kwa sasa jambo linalochochea umuhimu wa kukaa pamoja kwa viongozi wetu katika kuimarisha ushirikiano zaidi kwa maslahi ya pande zote mbili.
Kazi iendelee,Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.