PreGE2025 Rais Samia kugawa bahasha kwa watumbuizaji ni sawa na kununua watu, anatuonesha hakubaliki bila 'zawadi'?

PreGE2025 Rais Samia kugawa bahasha kwa watumbuizaji ni sawa na kununua watu, anatuonesha hakubaliki bila 'zawadi'?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Wakuu,

Karibu wenye kila mkutano wa ndani ambao Rais Samia huwa mgeni rasmi, huwa kunakuwa na vikundi vywa kutumbuiza yaani wasanii wakubwa wa muziki, wa mashaiemri, kuna ngoma nk.

Sasa wasanii hawa wakimaliza kufanya shughuli zao huenda moja kwa moja kwa Rais Samia kupokea bahasha zao na kuondoka.

View attachment 3274495

Kuna ulazima gani wa yeye kama Rais kukabidhi ujira huo kwa wanaotumbuiza? Kamati inakuwa na shughuli gani? Ni kwasababu anafanya hivi makusudi. Kuonesha nguvu, kwamba mimi ndio 'mfuga mbwa', usipofata mluzi wangu jua haupo na mimi.

View attachment 3274493

Kitendo hiki kwanza ni RUSHWA bila kupepesa macho. TAKUKURU hapa huwa hawaoni kabisa wala hawasikii. Watu wananunuliwa mchana kweupe ili uaminifu wao ubaki kwa Rais! Hatuwezi kutarajia uwajibikaji wakati msingi umejengwa kwa kuta za biskuti zinazotafunywa na kumegwa na panya kila iitwapo leo.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Kupitia kitendo hicho anatuma ujumbe pia. Kwamba mambo yako yatakunyookea endapo tu utamfurahisha, na yeye ndio mtoaji hela mkuu. Ukimzingua na mrija wako umekatwa, hivyo unatakiwa kuwa 'mbwa' mwaminifu kwake wakati wote.

View attachment 3274494

Kwa upande mwingine hii inaonesha Rais Samia bila pesa hakuna wa kumsikiliza, bila pesa hakuna anayeoona anafaa, bila pesa hakuna "Mama anatosha", bila pesa hata kina Lucas Mwashambwa ChoiceVariable Tlaatlaah akili zinawarudi, mama wa taifa anakuwa hatoshi hata kuwa wa nyumba kumi.

Yote kwa yote kitendo hiki kinatakiwa kukemewa mapema kabla mizizi haijakomaa mwisho kila mtu akawa anaenda kwa Samia kupata ujira kwa 'kazi nzuri' aliyofanya kuhakikisha anaendelea kufanya 'kazi nzuri'.

View attachment 3274496

#MamaUsirudiTena

Ila hako ka hashtag kama kamenoga hivi, au vipi Tlaatlaah?:BearLaugh::BearLaugh::BearLaugh:
Hizo stori hazitaksaidia kama unagombea toa bahasha.

Nikukubli wewe ni Mke/mume au mzazi wangu?
 
Tia neno Tlaatlaah na wenzake wapone Mkuu :BearLaugh: :BearLaugh: :BearLaugh:
maelezo na ufafanuzi wangu wa kina kuhusu mambo hayo, nadhani umeeleweka na kukubalika na wadau wote JF,

kwenye hilo nimefurahi sana,
asanti kwa kunielewa Cute Wife, inapendeza sana kua pamoja kama familia moja na taifa kwa ujumla tukiongozwa na Dr.Samia Suluhu Hassan:KasugaYeah: :pedroP:
 
Back
Top Bottom