wa R4Samuya ni Dr wa nn, tuanzie hapo kwanza!
Huyu Hakainde Hichilema ni mtu muhimu sana kwetu, tuna kazi ya kuijenga upya reli ya TAZARA ifike hadi Angola ili kupambana na reli pinzani ya Lobito inayojengwa na wazungu ili kupunguza wanaotumia bandari zetu.
TAARIFA KWA UMMA
RAIS SAMIA KUSHIRIKI SHEREHE ZA UAPISHO WA RAIS HICHILEMA WA ZAMBIA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo tarehe 01 Septemba, 2026, anaondoka nchini kuelekea Lusaka, Zambia kuhudhuria sherehe za Uapisho wa Rais Mteule wa Jamhuri ya Zambia, Mheshimiwa Hakainde Hichilema.
Katika Uchaguzi Mkuu wa Zambia uliofanyika tarehe 13 Agosti, 2026, Rais Hichilema alichaguliwa kuiongoza nchi hiyo kwa muhula mwingine wa miaka mitano.
Ziara ya Rais Dkt. Samia inaendeleza uhusiano wa kindugu na kihistoria kati ya Tanzania na Zambia, unaojengwa katika misingi ya umoja, mshikamano, ujirani mwema na ushirikiano wa kikanda.
Bakari S. MachumuMkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu
Pia soma: Rais Samia Suluhu Hassan ampongeza Rais Mteule wa Zambia Haikande Hichilema kwa kushinda muhula wa pili
Dr wa hapa na pale.Samuya ni Dr wa nn, tuanzie hapo kwanza!
Hata ule wa Marekani wanautilia shaka vilevile. Survival of the fittest.Uchaguzi Huo Ulijaa Ukakasi Mwingi
Dr wa kuchapa na kuhamasisha uchapaji wa mikwaju kwa wanaharakati kutoka mataifa jirani Kenya na UgandaSamuya ni Dr wa nn, tuanzie hapo kwanza!
Ndege wafananao huruka pamoja, so usishangae mkuu...hata mbinu za wizi wa kura zilitajwa kutokea Tz kwa wana ccm!Uchaguzi Huo Ulijaa Ukakasi Mwingi
Hivi hua hana mshipa wa aibu?Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiagana na Viongozi mbalimbali kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar kabla ya kuondoka nchini, kuelekea Lusaka Zambia kuhudhuria Sherehe za Uapisho wa Rais Mteule wa Jamhuri ya Zambia Mheshimiwa Hakainde Hichilema kufuatia ushindi alioupata katika Uchaguzi Mkuu wa Zambia Uliofanyika tarehe 13 Agosti, 2026 ambapo Rais Hichilema alichaguliwa kwa Muhula mwengine wa Miaka mitano. Tarehe 01 Sept, 2026.View attachment 3661125