Rais Samia Kuingia Katika vitabu Vya historia yaDunia. Ni Baada ya Kualikwa na Mataifa mawili Tofauti kuwa Mgeni Rasmi katika maadhimisho ya uhuru wao

Rais Samia Kuingia Katika vitabu Vya historia yaDunia. Ni Baada ya Kualikwa na Mataifa mawili Tofauti kuwa Mgeni Rasmi katika maadhimisho ya uhuru wao

Acha uongo, sa100 hana akili wala maarifa yoyote...mtu alipata zero form 4 anatoa wapi hizo skills?!.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Ukisikia kupendwa basi huku ni zaidi ya kupendwa ,ni zaidi ya kuheshimika ,ni zaidi ya kuthaminiwa,ni zaidi ya ushawishi ,ni zaidi ya kukubalika na Dunia.

Kwa hakika Rais Samia anapendwa hapa Duniani sijapata kuona ,.anakubalika haijapata kutokea. Ana ushawishi haijapata kushuhudiwa. Mama amekuwa kama ndio Nembo ya Afrika. Amekuwa kama Nabii na Mtume Wa Mungu kuleta amani Ulimwenguni wote.

Anang'ang'aniwa kila kona,. Kila mtu sasa anatamani kuona Rais Samia anatua na kukanyaga ardhi yake ili walau apate baraka na maneno ya hekima ,busara ,maarifa na maono ya namna ya kujenga nchi zao. Kila mmoja anatamani kuona Rais Samia akizungumza na Taifa lake kwa kutoa hotuba .kila mmoja anatamani apate muda hata wa dakika moja wa walau kuchota maarifa kutoka kwa Rais wetu Mpendwa na Jemedari wetu kipenzi cha watanzania aliyeinuliwa kwa Mkono wa Mungu Mwenyewe.

Sasa Afrika wanapigana vikumbo kumpatia mialiko ya kuwa mgeni Rasmi katika matukio muhimu kwa nchi zao. Kila mmoja anajaribu kukimbizana na ratiba ya Rais Samia ili walau kupata upenyo wa kumualika na kuchota maarifa kutoka kwake.

Kwanini imekuwa hivyo? Hii inatokea baada ya viongozi mbalimbali barani Afrika na Duniani kwote wote kwa ujumla wake kutambua uwezo mkubwa wa kiakili alionao Rais Samia. Watu wamejua Mama ni akili kubwa ,kichwa kwelikweli, watu wamegundua Mama anaishi mbele ya wakati na anaona vitu vya mbele kama Twiga mbugani au rubani angani. Sasa wanatamani waweze kufikishwa kimawazo mahali ambapo wao pekee yao hawawezi kufika.

Ndio sababu ya kuona mialiko mizito mizito ikitua mezani pa Rais wetu kumuomba kwa unyenyekevu mkubwa kuhudhuria kama mgeni Rasmi katika matukio muhimu katika Nchi zao. Ndio sababu tuliona akipata mualiko wa kipekee katika mkutano wa Nchi 20 matajiri zaidi Duniani Kwote. Ndio maana tuliona akipata mualiko mzito na heshima ya kipekee kule nchini Namibia katika Uapisho wa Rais wa Taifa hilo.

Sasa Msumbiji na Comoro nao katika kupigana vikumbo na kukimbizana na ratiba ya Mheshimiwa Rais wamepata upenyo na kumuomba Mheshimiwa Rais wetu kipenzi kubwa mgeni Rasmi katika maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru wa Nchi zao . Ambapo mualiko wa kwanza ni wa june 25 kwa Msumbiji na mwingine ni Julai 6 kwa upande wa Comoro.

Jambo kama hili kwa kiongozi wa Nchi kualikwa katika mataifa mawili tofauti kama mgeni Rasmi katika maadhimisho ya heshima kama haya haijawahi kutokea popote pale . Na hivyo Rais Samia anaingia katika vitabu vya historia ya Dunia ambayo vizazi kwa vizazi vitajifunza historia hii juu ya Mama huyu shupavu,madhubuti ,imara na hodari kuwahi kutokea hapa Nchini na pengine katika uso wa Dunia.

Kwa hakika Rais Samia ni zawadi kwetu watanzania tunayopaswa kuitunza na kuilinda kwa wivu mkubwa sana. Mama ni Hazina ya Tanzania, Afrika na Dunia nzima kwa ujumla wake.View attachment 3364840View attachment 3364846

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
No reform no election
 
Back
Top Bottom