..Nakumbuka baada ya vita vya Kagera / Uganda Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere aliomba Watz " wafunge mikanda " kwa miezi 18 ili arekebishe uchumi.
..tangazo hilo lilifuatiwa na hatua mbalimbali za kubana matumizi haswa ya fedha za kigeni.
..moja ya eneo ambalo serikali ililenga ni uagizaji wa mafuta. Serikali ilikuwa haina fedha za kutosha kuagiza mafuta.
..kutokana na hali hiyo kukawa na marufuku ya kuendesha gari binafsi Jumapili baada ya saa 8 mchana. Yaani polisi akikukuta unaendesha gari binafsi Jumapili baada ya saa 8 utaipeleka gari hiyo kituoni.
..SAMAHANI kama nimechepuka nje ya mada.
Cc
Kiranga,
Nguruvi3