Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,681
- 8,887
Rais Samia Suluhu akiwa mkoani Mara kuweka jiwe la msingi kwenye mradi wa maji ameongelea suala la miradi ya Serikali. Ameuongelea mradi huo ulioanzishwa na Serikali ya awamu ya tano lakini ukakwamishwa na mkandarasi na kuamua kumbadilisha ili kumalizia mradi. Pia Rais Samia ameongelea spidi ya maendeleo ya miradi kwenye Serikali ya awamu sita.
========
Rais Samia: Serikali yenu tulisema kazi iendelee na kazi inaendelea, najua ndugu zangu kulikuwa na vinenoneno kadhaa, elimu haitaendelea, miradi haitaendelea na mambo mengine kadhaa, lakini nadhani mnajionea wenyewe kwa macho yenu kwamba miradi inaendelea na inaendelezwa kuliko ilivyokuwa ikiendelea, kwahiyo kazi iendelee.
Mwisho Rais ameongelea miradi ya mkoa wa Mara kusuasua na kusema leo mchana atalisemea wakati akizindua hospitali ambapo watatafuta sababu ya kusuasua na pengine kuitafutia dawa na wakiona wanachukua hatua wananchi wajue wanatafutiwa dawa.