Kuwa na imani na awamu ya sita isitumiwe kama uchochoro wa watu kuvunja sheria, kujaribu kuvuruga amani iliyopo, na kutafuta huruma kwa mgongo wa matukio ya hovyo yanayopangwa na wanasiasa wachovu ambao wamefilisika kihoja na kimkakati. Wanasiasa ambao wameshindwa kusimamia sera zao kikamilifu nk. Namshauri mama asilegeze kamba hata dakika moja, kila atakaevunja sheria na kuvuruga amani kwa nia ya kuja kutafuta huruma huku mitandaoni, ashughulikiwe kwa mujibu wa sheria. Hakuna muda wa kucheka na nyani shambani. Haya maneno ya kujifanya kumpamba mama ili watu wapate nafasi ya kuiharibu nchi hayana nafasi kwa sasa.