Rais Samia: Kuna biashara za mtandao nyingi zinafanyika hazilipi Kodi na hatuzijui. Mfumo wa Anwani utakapoingia, tutawajua

Rais Samia: Kuna biashara za mtandao nyingi zinafanyika hazilipi Kodi na hatuzijui. Mfumo wa Anwani utakapoingia, tutawajua

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema kukosekana Mfumo wa uhakika wa utambuzi wa Wakazi na Makazi umepelekea athari nyingi kiuchumi, kiusalama na kijamii.

Amesema manufaa ya Mifumo hiyo ya utambuzi ni mengi ikiwemo kuwezesha kufanyika Biashara Mtandao na kuimarisha usalama.

Ameeleza hayo leo akishiriki Kikao Kazi cha Wakuu wa Mikoa kuhusu Mfumo wa Anwani za Makazi na kusema, "Hata wanaofanya Biashara Mtandao tutawajua. Sasa hivi kuna biashara za mtandao nyingi zinafanyika hazilipi Kodi na hatuzijui. Utakapoingia Mfumo huu tutawajua"
 
I do not know how they can handle that! Watafakari sana kuwekeza Sana kwenye hayo and at the end of they day wasipate kitu!
 
Kuna siku nilisema watatimba hadi huko pishi limeanza kuiva
 
Apeleke elimu ya Tehama hadi kwenye shule za kata na elimu ya Tehama kwa watu wazima. Atavuna zaidi akiwekeza huko.
Wanasiasa kama Magufuli wanae wanasoma au walisoma super santas ,wa Nyerere wakisoma za umma.
Mzalendo alikuwa Nyerere lakini hao wanaohubiri communication skills ziwe kiswahili tu waogope kama ukoma ni wapuuzi na wanafiki.

Hivi English si somo kama jingine?kwanini mnakuwa na kigugumizi cha unafiki.
Mbona mtu usoma masomo mengine hadi kuwa bingwa kwa vitu vikubwa tu.Lakini ili tufike hapo communication skills mara nyingi ni lugha ya mama yaani English.

Sijui kwanini watu wanatumia nguvu kubwa kuuwa nchi wakijinadi na substandard issues after all swahili genuine copy right siyo ya wabantu ni Dr Krapf na Lehmann nadhani Wajerumani .OPEN YOUR EYES.
 
Hela zinaliwa tuuuuuuuuuuu,
Sasa unadhani zitatosha?
Matumizi mengi hayana ulazima
 
Mbona tunaponunua vitu kutoka Amazon huwa tunalipia na VAT ,Hii Vat huwa inaenda wapi wadau🤔🧐
 
Huu ni mfumo utakaowanufaisha madalali wa MABEBERU kuiuza nchi kwa urahisi zaidi bila kulazimika kuwaleta nchini kwanza.

Sasa una google aerial code ya eneo husika na inakuletea kila kitu kama ni Earth, Street map, google map kama kawa.
 
Hahaaaaaa, watakata kwenye kila miamala inayotoka nje ya bongo
We ukienda kuchange sh to dolar unakatwa kodi? Sasa fx sio kutumiwa pesa bali ni kufanya exchange kutoka Usd ambayo ipo ktk mt4 yako kuwa sh ambapo hukatwi kodi
 
Kwa sisi tunaocheza na bitcoins na NFT msahau kutupata na kodi zenu🐒
IllSimilarCavy-max-1mb.gif
 
Back
Top Bottom