Rais Samia, kuna dalili zote za kuwa na mafuta ziwa Tanganyika na Nyasa

Rais Samia, kuna dalili zote za kuwa na mafuta ziwa Tanganyika na Nyasa

Hiyo ndio ilikuwa philosophy ya Magufuli ambayo Samia anajaribu kurekebisha kwa kuwa ilituharibia nchi sana!
Jibu hoja yangu kama ilivyo, usikimbilie kujificha kwenye mzimu wa JPM, kama ilikuwa falsafa yake, so what? Ipinge hoja ya falsafa hiyo kwa hoja. Hoja kwa hoja.
 
Mafuta yatatumika kuendesha Mitambo y kuzalisha umeme, Mfano Generators, kwahiyo usijali msee
Hio Mali haina expire date
Mitambo yote mikubwa na injini zenye ujazo mkubwa tutatumia sana dizeli sio leo sio kesho mafuta kuacha kutumika labda miaka 100 baadae

Bado sioni teknolojia ya kutumia umeme kwenye meli za mizigo,magari makubwa na mitambo hivi karibuni

Halafu watu bado wanatumia mpaka coal ambayo emmisions zake ni mbaya zaidi kuliko mafuta so zutu la muarabu bado lipo lipo sana tu
 
Raisi Samia, nadhani una taarifa kwamba kuna kila dalili za mafuta ndani ya Ziwa Tanganyika na Ziwa Nyasa. Hakuna maendeleo yaliyofanyika kuchimba mafuta katika maeneo haya kutokana na vikwazo viwili;
  1. Upande wa ziwa Tanganyika kuna kikwazo cha waasi wa DRC. Si rahisi kuendeleza mradi wa mafuta ziwani Tanganyika ikiwa waasi hawa wa DRC hawajaondolewa kabisa. Na mafuta haya yataendelezwa kwa ushirikiano kati ya Tanzania na DRC, ndio maana Tanzania ilikuwa tayari kupeleka jeshi DRC kusaidia kuondosha waasi ili tuchimbe haya mafuta kwa ushirikiano na DRC. Inaonekana zoezi la kuondoa waasi limekwama, na hiki kimekuwa kikwazo
  2. Upande wa ziwa Nyasa kuna mafuta. Lakini pindi ilipoonekana Ziwa Nyasa lina mafuta tuliingia katika mgogoro wa mpaka kati yetu na Malawi. Wakijua rasilimali ya mafuta iloiyomo ziwani, Malawi walianza kudai ziwa Nyasa lote liko upande wa Malawi na ndio maana wao wanalitambua kama Ziwa Malawi. Nilipendekeza humu JF kwamba tuachane na suala la mgororo wa mpaka na jirani zetu Malawi tukubaliane nao kwamba rasilimali yoyote ya mafuta ndani ya ziwa tutagawana 50/50 bila kujali iko upande gani. Sijui kama nilisikilizwa.
Sasa kuna tatizo. Kutokana na tatizo la mabadiliko ya mazingira (climate change), mataifa makubwa duniani yameweka mkakati wa kuacha kutumia mafuta kwa ajili ya magari na mitambo. Norway kwa mfano, wanasema kufikia 2050 wataacha kabisa shughuli za kuchimba mafuta. Uingereza wanasema watapiga marufuku magari ya kutumia diesel kufikia 2025 nadhani. Japan, Germany na hata China, wote wanasema ndani ya miaka 15 ijayo wanataka kutoka kwenye kutumia mafuta kwenye magari na kuingia kwenye magari ya umeme (from internal combustion engines to electric vehicles)

Sasa hii inamaanisha nini kwa nchi kama Tanzania ambazo hadi sasa zimekalia tu uchumi wa mafuta bila kuuendeleza? Ina maana ndani ya miaka 20 ijayo, mafuta yatakuwa si mali kitu. Hata ukigundua una mafuta mengi kama bahari ya Hindi, hayatakusaidia tena kwa kuwa dunia imeanza kuondoka toka tekinolojia ya mafuta kwenda teknolojia ya umeme!

Hivyo basi, kama kweli tunataka kufaidika na rasilimali ya mafuta tuliyonayo, ni lazima iendelezwe ndani ya kipindi cha miaka kumi ijayo. La sivyo haya mafuta yatakuwa na rasilimali isiyohitajika tena duniani, na ndani ya kipindi cha miaka kumi ijayo tutaanza kushuhudia kuporomoka kwa bei ya mafuta kadiri magari ya umeme yanavyoingia sokoni. Leo hii hata Lamborghini wamesema wataacha kutengeneza gari za mafuta!

Kwa hiyo kaza mwendo tuweke mkakati wa kuchimba mafuta Lake Tanganyika na Nyasa. Tatua changamoto zinazokabili maeneo haya. Waambie TPDC waache ku-weka areas with the highest oil potential for last. Ikiwezekana, wafanye mkupuo mmoja wa kugawa vitalu vya kufanya oil and gas exploration kwa nchi nzima, time is of essence, waache mwendo wa bata.

Tukiweza kuchimba mafuta ndani ya miaka kumi ijayo, yatachangia sana kuinua uchumi wetu, tutakuwa na barabara za rami hadi vijijini! Tukichelewa, haya mafuta hayatatusaidia, yatakuwa obsolete resource!

Angalia pia:

Suluhisho la mgogoro na Malawi ni hili; sio suala la ziwa wala mpaka

Suala la uwepo wa mafuta katika ziwa Nyasa na kusababisha mgogoro wa mpaka kati ya Tanzania na Malawi limeishia wapi?

Katika awamu hii chini ya Rais mpya Malawi, Magufuli atumie fursa hii kutatua mgogoro wa mpaka kati ya Malawi na Tanzania
hawa TPDC bonde la mandawa huko lindi bonde la ruvuma huko mtwara na bonde la tanga hawajamaliza kufanya utafiti ingawa viashiria vya uwepo wa mafuta vinaonekana wazi pamoja na sababu za kijiolojia zinazo sadifu uwepo wa mafuta.
 
Kuna uharaka gani wa kuchimba mafuta? Tuna resources nyingi ambazo bado hatuja utilize potential yake ikiwamo Gesi. Kama mafuta yatashuka bei itakuwa vyema kwa uchumi wa nchi. Wanaojenga petrol stations waweke option ya umeme na gas. Mabadiliko hayakawii kuja. Jirani zetu uganda washaanza mradi wa magari ya umeme ya abiria.
 
Nishati ya mafuta haiwezi kuwa obsolete hata kwa miaka mia mbili ijayo, bado yatatumika sana kwenye kuendesha mitambo mikubwa hata huko kwa wazungu, na kwa nchi za ulimwengu wa tatu itachukua miaka mingi zaidi kuacha kutegemea nishati ya mafuta....
 
Na hayo magari ya kutumia mafuta mtatengeneza wenyewe? Na spare zake?

Na kuchimba mafuta kwa ajili ya soko la ndani ya nchi peke yake is not economical
Tutatengeneza.Mbona hata kenya tu wanatengeneza magari.
South, Ghana, Nigeria kote wanatengeneza gari.
Kuundda magari sio jambo linalowasumbua waafrika kwa sasa labda ndege.
Kumbuka mafuta yanaweza kubadilishwa kuwa umeme.
 
Hizo ni ndoto mafuta bado yapo Sana hadi mwisho wa dunia.Sema labda yashuke bei sababu KILA nchi Ina mafuta wakianza kuchimba
 
Meli,jenerator,mbolea,gas,lami, grease,rangi, mafuta bado Sana yapo
 
Hoja ya waasi wa DRC kuwa sababu ya kutochimba mafuta ziwa Tanganyika haina mashiko, mbona Total wame-exprole gas Ziwa Tanganyika upande wa DRC? Labda ziko sababu nyingine.

Vv
Inategemea TOTAL wamefanya exploration ya gas upande gani. Ziwa Tanganyika ni refu sana. Na pia kama TOTAL wamefanya exploration, haiondoi ukweli kwamba huko nyuma DRC walisema tatizo kubwa la kuendeleza mafuta upande wao au kwa kushirikiana na Tanzania ni waasi Mashariki mwa nchi hiyo na kuiomba Tanzania kusaidia kuwaondoa
 
Hizo ni ndoto mafuta bado yapo Sana hadi mwisho wa dunia.Sema labda yashuke bei sababu KILA nchi Ina mafuta wakianza kuchimba
Watu kama wewe ni wagumu sana kuelewa. Tatizo sio mafuta kutopatikana tena, tatizo ni kubadilika kwa technolojia. Kwani watu waliacha kutumia radio kaseti kwa kuwa ziliisha?
 
Meli,jenerator,mbolea,gas,lami, grease,rangi, mafuta bado Sana yapo
Na vitu hivyo vinachukua asilimia ngapi ya soko la mafuta? Ongea kama mtu aliyeelimika, kwa takwimu. Kwa taarifa yako synthetic grease (lubricants) za sasa no bora kuliko hizo za mafuta.
 
Kwani makampuni ya kuchimba mafuta unadhani yanatoka nchi zipi?
Atafanya nini? Kwanza mataifa ya Magharibi yanaona ni kiboko cha kumtandikia maana mafuta yanampa kiburi. Na huo sio mpango tena, ni jambo linatekelezwa kwa sasa.
 
Jibu hoja yangu kama ilivyo, usikimbilie kujificha kwenye mzimu wa JPM, kama ilikuwa falsafa yake, so what? Ipinge hoja ya falsafa hiyo kwa hoja. Hoja kwa hoja.
Nimeona hakuna kitu cha maana ulichoongea ambacho kinastahili jibu langu. Huo mfoforo wa mpaka kati ya Malawi na TZ umekuwapo kwa muda gani?
 
Back
Top Bottom