Rais Samia, kuna dalili zote za kuwa na mafuta ziwa Tanganyika na Nyasa

Hiyo ndio ilikuwa philosophy ya Magufuli ambayo Samia anajaribu kurekebisha kwa kuwa ilituharibia nchi sana!
Jibu hoja yangu kama ilivyo, usikimbilie kujificha kwenye mzimu wa JPM, kama ilikuwa falsafa yake, so what? Ipinge hoja ya falsafa hiyo kwa hoja. Hoja kwa hoja.
 
Huo mpango wa magari ya umeme muarabu hawezi kubali
 
Mafuta yatatumika kuendesha Mitambo y kuzalisha umeme, Mfano Generators, kwahiyo usijali msee
Hio Mali haina expire date
Mitambo yote mikubwa na injini zenye ujazo mkubwa tutatumia sana dizeli sio leo sio kesho mafuta kuacha kutumika labda miaka 100 baadae

Bado sioni teknolojia ya kutumia umeme kwenye meli za mizigo,magari makubwa na mitambo hivi karibuni

Halafu watu bado wanatumia mpaka coal ambayo emmisions zake ni mbaya zaidi kuliko mafuta so zutu la muarabu bado lipo lipo sana tu
 
hawa TPDC bonde la mandawa huko lindi bonde la ruvuma huko mtwara na bonde la tanga hawajamaliza kufanya utafiti ingawa viashiria vya uwepo wa mafuta vinaonekana wazi pamoja na sababu za kijiolojia zinazo sadifu uwepo wa mafuta.
 
Kuna uharaka gani wa kuchimba mafuta? Tuna resources nyingi ambazo bado hatuja utilize potential yake ikiwamo Gesi. Kama mafuta yatashuka bei itakuwa vyema kwa uchumi wa nchi. Wanaojenga petrol stations waweke option ya umeme na gas. Mabadiliko hayakawii kuja. Jirani zetu uganda washaanza mradi wa magari ya umeme ya abiria.
 
Nishati ya mafuta haiwezi kuwa obsolete hata kwa miaka mia mbili ijayo, bado yatatumika sana kwenye kuendesha mitambo mikubwa hata huko kwa wazungu, na kwa nchi za ulimwengu wa tatu itachukua miaka mingi zaidi kuacha kutegemea nishati ya mafuta....
 
Na hayo magari ya kutumia mafuta mtatengeneza wenyewe? Na spare zake?

Na kuchimba mafuta kwa ajili ya soko la ndani ya nchi peke yake is not economical
Tutatengeneza.Mbona hata kenya tu wanatengeneza magari.
South, Ghana, Nigeria kote wanatengeneza gari.
Kuundda magari sio jambo linalowasumbua waafrika kwa sasa labda ndege.
Kumbuka mafuta yanaweza kubadilishwa kuwa umeme.
 
Hizo ni ndoto mafuta bado yapo Sana hadi mwisho wa dunia.Sema labda yashuke bei sababu KILA nchi Ina mafuta wakianza kuchimba
 
Meli,jenerator,mbolea,gas,lami, grease,rangi, mafuta bado Sana yapo
 
Hoja ya waasi wa DRC kuwa sababu ya kutochimba mafuta ziwa Tanganyika haina mashiko, mbona Total wame-exprole gas Ziwa Tanganyika upande wa DRC? Labda ziko sababu nyingine.

Vv
Inategemea TOTAL wamefanya exploration ya gas upande gani. Ziwa Tanganyika ni refu sana. Na pia kama TOTAL wamefanya exploration, haiondoi ukweli kwamba huko nyuma DRC walisema tatizo kubwa la kuendeleza mafuta upande wao au kwa kushirikiana na Tanzania ni waasi Mashariki mwa nchi hiyo na kuiomba Tanzania kusaidia kuwaondoa
 
Hizo ni ndoto mafuta bado yapo Sana hadi mwisho wa dunia.Sema labda yashuke bei sababu KILA nchi Ina mafuta wakianza kuchimba
Watu kama wewe ni wagumu sana kuelewa. Tatizo sio mafuta kutopatikana tena, tatizo ni kubadilika kwa technolojia. Kwani watu waliacha kutumia radio kaseti kwa kuwa ziliisha?
 
Meli,jenerator,mbolea,gas,lami, grease,rangi, mafuta bado Sana yapo
Na vitu hivyo vinachukua asilimia ngapi ya soko la mafuta? Ongea kama mtu aliyeelimika, kwa takwimu. Kwa taarifa yako synthetic grease (lubricants) za sasa no bora kuliko hizo za mafuta.
 
Kwani makampuni ya kuchimba mafuta unadhani yanatoka nchi zipi?
Atafanya nini? Kwanza mataifa ya Magharibi yanaona ni kiboko cha kumtandikia maana mafuta yanampa kiburi. Na huo sio mpango tena, ni jambo linatekelezwa kwa sasa.
 
Jibu hoja yangu kama ilivyo, usikimbilie kujificha kwenye mzimu wa JPM, kama ilikuwa falsafa yake, so what? Ipinge hoja ya falsafa hiyo kwa hoja. Hoja kwa hoja.
Nimeona hakuna kitu cha maana ulichoongea ambacho kinastahili jibu langu. Huo mfoforo wa mpaka kati ya Malawi na TZ umekuwapo kwa muda gani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…