Rais Samia, kuna dalili zote za kuwa na mafuta ziwa Tanganyika na Nyasa

Huyu jamaa anachekesha sana kama mafuta yapo upande wa Malawi waache wachimbe ila kama yapo Tanzania ni ya kwetu hatuwezi kugawana rasilimali kwa sababu tu ya kuridhishana
 
Rudi darasani kijana! Huku umerusha upupu mtupu! Nashukuru waelewa wa mambo wamekujibu!
Nadhani unaona aibu kwa kuongea bila ufahamu wa hivi vitu. Kuna wakati ni bora kukaa kimya, sio lazima utoe comments kwenye kila thread. Ukikosa cha kusema nenda kule kwenye thread za Mwajuma kamfumania mumewe na rafiki yake akagoma kupika, huko utakuwa na wigo mpana wa ku-comment, maana hizi thread sio size yako.
 
Huyu jamaa anachekesha sana kama mafuta yapo upande wa Malawi waache wachimbe ila kama yapo Tanzania ni ya kwetu hatuwezi kugawana rasilimali kwa sababu tu ya kuridhishana
Mkuu, unaelewa jiolojia ya mafuta kabla hata ya kusema hivyo? Mafuta yanakuwa ndani ya mwamba, na ukisema kila mtu achimbe upande wake inawezekana kabisa mkawa mnachimba tola reservoir moja. Pili kumbuka context ya thread ziliwekwa kama reference ni kwamba uwezekano wa kukubaliana mpaka uko wapi ni mdogo. Sasa tutachimbaje kila mtu upande wake wakati hautujaelewana kila mtu upande wake ni wapi? Tutaishia kutoelewana juu ya hilo hadi mafuta yapoteze thamani.

Hivi kwa nini watu wengine mnakuwa wagumu sana kusoma na kuelewa maandishi na mnaishia kusema huyu anachekesha?
 
Mimi hoja yangu ni wapi mafuta yanapatika hayo mengine siyo ya msingi, Zanzibar waliondoa maswala ya mafuta na gesi baada ya kuhisi wanaweza kupata mafuta baharini
 
Mimi hoja yangu ni wapi mafuta yanapatika hayo mengine siyo ya msingi, Zanzibar waliondoa maswala ya mafuta na gesi baada ya kuhisi wanaweza kupata mafuta baharini
Nchi za Uingereza, Norway na Denmark waligundua mafuta kule North Sea. Sasa ili wasiingie kwenye huu ubishi wa kijinga kama tulio nao na Malawi, wakaamua kufanya ubia wakijua mwamba wa mafuta utakuwa umesambaa sehemu zote, badala ya kila nchi kujikakamua kuchimba upande wake. Kwa hiyo nimeanzia hapo - shule inasaidia hatuongei tu vitu hivi. Haina maana kugombana na Malawi juu ya mpaka kwa ajili ya mafuta wakati ni wazi mwamba wa mafuta ndani ya ziwa Nyasa utakuwa umesambaa sehemu ya Malawi na Tanzania

 
Na hayo magari ya kutumia mafuta mtatengeneza wenyewe? Na spare zake?

Na kuchimba mafuta kwa ajili ya soko la ndani ya nchi peke yake is not economical
Kwani mafuta tunatumia kwenye magari na bodaboda tu? Vipi Boti na Meli kubwa za mizigo? Vipi ndege za abiria na mizigo na za kivita? vipi magenerator? hata sabuni za kufulia nazo, Lami?

In short mafuta bado yataendelea kutumika tu na hasa Africa. Kama ishu ya kupiga vita mafuta kisa inachafua mazingira, basi ni bora waekeze kwenye Research and Development na kupunguza uchafuzi wa mazingira. Mfano Diesel pekee came a long way, tangu unakuta ki sedan kinatoa moshi hadi sasa unakuta Range Rover diesel haitoi moshi. Sijaona souce of energy ambayo tunaweza kutumia bila kuharibu mazingira. Hizo Batteries nazo ndo ivo ivo. Nuclear power ingekuwa good replacement ila shida ipo kwenye radiation na waste.
 
Mafuta yanakaribia kugunduliwa kwenye maeneo karibu ya Ziwa eyasi , tabora na simiyu kwa mujibu wa waziri wa nishati na uzalishaji ukianza watatumia bomba la tanga

Mama alitoa maelekezo wataalamu wa Tanzania washirikiane na wataalamu wa Uganda matokeo yameanza kuonekana

Kuhusu ziwa tanganyika hakuna waasi ni vibaka wa kawaida tu, waasi wapo upande wa kaskazini jimbo la kivu mpaka wa DRC na Rwanda na uganda
 
Sidhani kama umetia shule, ungetumia shule ungeelewa nini kiini cha ugomvi wa Malawi na Tanzania.
Ugomvi wa Malawi na Tanzania unatokana na Malawi kutaka kujimilikisha ziwa lote Nyasa lakini wewe umeleta hoja mfu nyie ndio mkonTanzania mkijifanya watanzania kumbe sio watanzania si ajabu ni ukoo wa kina Karume
 
Sasa wewe, unafikiri hadi wakaamua kukomesha matumizi ya mafuta yote hayo hawajafikiria? Wewe unaingilia field za watu na kutoa point ambazo hazina mshiko. Hiyo neclear power utatumia kwenye magari? Na unajua athari na gharama zinazotokana na nuclear power? Kwa taarifa yako nchi zilianza kuondokana na nuclear power kabla hata hawajaanza kufikiria kuondokana na mafuta.

Ngoja nikueleweshe kidogo; usichanganye kati ya ambient air pollution ya mafuta na greenhouse gas emission ya mafuta. Unaweza ukapunguza sana ambient air pollution lakini greenhouse gas emission zikabaki pale pale. Kwenye ambient air pollution hatua imepigwa katika kupunguza kiwango cha sulfur and particulates, na kukomesha kuweka Lead kwenye mafuta, ndio maana unasikia kuanzia sasa Leaded Petrol hairuhusiwi, au Diesel inayoruhusiwa ni 50ppm au 10ppm. Hiyo ni pollution, lakini hata ukiwa na na unleaded Petrol au Diesel safi ambayo tunaita Ultra-low-sulfur diesel (ULSD), bado haipunguzi greenhouse gas emissions. Unakuwa umepunguza pollutants.

Ndio maana basi, msukumo mkubwa wa kukomesha mafuta uko kwenye kuzuia emissions za greengose gases ambazo zinasababisha climate change, na ndio maana kwa sasa hata mvua za dhoruba zinainyemelea Tanzania ambapo ni jambo la ajabu. Tunaona mvua kubwa za mafuriko na ukame ukiongezeka kwa ajili ya climate change, ambayo kwa kiwango kikubwa inasababishwa na matumizi ya mafuta. Ndio maana dunia imeamua kuachana na mafuta, sasa watu kama nyie acheni kung'ang'ania tekinolojia zilizopitwa na wakati
 
Acha upoyoyo. Sasa kusema ugomvi wa Tanzania na Malawi ni Malawi kutaka kujimilikisha ziwa lote, na kusema kuna mgogoro wa mpaka kati ya Malawi na Tanzania kuna tofauti gani? Wewe unafikiri Malawi wameibuka tu na kusema tunataka Ziwa lote? Kama wangefanya hivyo kungekuwa na haja ya kuwaweka watu kama kina Mbeki wasuluhishe?

Yaani leo Kenya wakiibuka na kusema Mlima Kilimanjaro ni wetu, unadhani dunia itahangaika kuweka tume za kusuluhisha kati ya Tanzania na Kenya? Kinakachotokea ni Kenya kushutumiwa na UN na jumuia za kimataifa na kuambiwa waache kabisa kuleta mgogoro usiokuwapo la sivyo watachukuliwa hatua za kimataifa.

Usuluhishi unakuja pale ambapo nchi inayodai mpaka inakuwa na sababu za msingi, na ukiangalia madai ya Malawi juu ya ziwa Nyasa yana msingi, lakini pia madai ya Tanzania juu ya mpaka kuwa katikati ya ziwa yana msingi. Ndio maana zinaundwa tume za usuluhishi za kina Mbeki na Chisano.

Vitu huvielewi lakini unatanguliza domo lako kubwa kuropoka, eti umeleta hoja mfu.
 
Hi mbona watu wagumu sana kuelewa mambo madogo kama haya? Mbona nimejibu hoja yako hapo juu?

Ni hivi, matumizi ya mafuta kwenye magari ni karibu 70% ya mafuta yanayozalishwa. Sasa ukipunguza hiyo 70% kwenda labda 30%, bei ya mafuta itashuka sana, kwa kuwa unakuwa umepunguza demand ya mafuta. Exploration na production ya mafuta kwa ajili ya matumizi yaliyobaki inakuwa sio economically feasible kwa uzalishaji mdogo mdogo. Watakaoweza kuendelea kuzalisha mafuta ni makampuni makubwa ambayo wao economies of scale zinafanya production cost zao kuwa chini. Hivyo wazalishaji wadogo kama Tanzania, Uganda nk itabidi wafunge production zao kwa kuwa itakuwa hasara wao kuendelea kuzalisha mafuta.

Sasa kama shule yako ni ndogo hapo nitakuwa nimekuchanganya sana!
 
Poyoyo ni wewe unayekuja na hoja zisizo nq mashiko mara ulaya wameacha kutumia mafuta hivi unafahamu ni mwaka wa ngapi nchi za Scandinavia zimeacha.kutumia mabasi yanayotumia mafuta na diesel halafu unakurupuka kurupuka au unatafuta cheo ungeweka na namba yako ya simu kabisa
 
Halafu ulivyo kilaza hujui investment ya uchimbaji wa mafuta na geai return yake inarudi baada ya muda gani
 
Poyoyo twice, hata haieleweki unabisha nini sasa, maana unaunga mkono hoja bila kujitambua
 
Halafu ulivyo kilaza hujui investment ya uchimbaji wa mafuta na geai return yake inarudi baada ya muda gani
Kilaza ni wewe, return za investment haina muda maalum kama unavyofikiria. Inategemea ni development off shore, onshore, na kama offshore ni deep sea nk. Na pia inategemea reservoir pressure, crude type nk. Inategemea pia cost za well development, acquisition agreement na hata vitu kama production sharing agreement, levies nk.

Sasa upo hapo? Domo kubwa masikio madogo, kujifanya unajua kumbe huna kitu. Nani alikuambia kuna fixed time ya return kwenye oil production? Mtafute nimtukane.
 
Uko tushachelewa sana tungwekeza kwenye kilimo both organic and modern farming, na viwanda especially agri business na mining hasahasa refinery mana haiwezekani ndo nchi ya 2 au 3 afrikaans then hatuna refinery kabisa au si za kutosha. Yani hii nchi imechelwa kila kitu na kila siku tunazidi kurudi nyuma. Tuwekeze viwanda na kilimo na sio mimafuta ambayo tumeshachelewa sana.
 
Wewe umechemka kwanza umshauri rais kama nani mtu mwenyewe una mbele wala nyuma
 
Kichwa maji , akili fupi bichwa kubwa ! idiot .Rudi Facebook k wewe
Utumwa wa akili unakusumbua sana, yani unaamini mzungu ndio mungu wako. Huwezi kupanga jambo lako bila kumuwaza mzungu.
Nyie ndio mnauza utu wenu pumbavu sana, kila kitu unawaza wazungu, wazungu wasipofanya hivi.
Hi dunia sio ya wazungu tu.
Ndio maana wazungu wanawaelekeza muoane pumbavu kama wewe unaweza kuwasapoti.
Maisha yanawezekana bila wazungu.
Usitake kunilazimisha niamini unavyoamini, acha kulazimisha mawazo yako yawe kweli kwa watu wote ni upumbavu.
 
Wewe umechemka kwanza umshauri rais kama nani mtu mwenyewe una mbele wala nyuma
Kiwango cha shule yako hata Kiswahili hakikukusaidia kukielewa, itakuwa issue kama hizi za elimu ya juu? Wewe kama kimya watu waliosoma wajadili hili suala.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…