Rais Samia, kuna dalili zote za kuwa na mafuta ziwa Tanganyika na Nyasa

Ulisoma vizuri nilichoandika au ulidandia tu? Rudia tena kusoma kwa utulivu.

Mafuta yataendelea kuchimbwa kwa miaka mingi tu ijayo na yatatumika.
 
Wewe shule yako kubwa 300 acres.

Kwenye hii link inasema 26% ya mafuta duniani inatumika kwenye usafiri. How electric vehicles could take a bite out of the oil market kwaio 74% iko kwenye sekta nyenginezo. Kwa hapa Afrika magari ya mafuta yataendelea kuwepo kwa mda mrefu sana tu. Isitoshe, bei ya mafuta watu wanaamua tu mwezi huu tuzalishe machache, bei inapanda watu wanajilipa, ndio michezo inayochezwa kila kukicha na wazalishaji mafuta au hujui hilo? Unafikiri mafuta bei yanapanda kwa sababu imekuwa shida uchimbaji au watu wameamua tupunguze uzalishaji na tutengeze demand? shuleni umelishwa kwa kijiko.
 
Kwa hii point wala sikubishii. Nimerudi kwenye reference yangu nikakuta inasema non-vehicle consumption ndio 74", kwa hiyo nakiri kufanya makosa hapo. Na you are right, global consumption ya transport ni 26%, hata kulingana na BP Outlook (angalia diagram chini hapa). Hata hivyo, note kwamba hiyo distribution ya matumizi ya mafuta haiko hivyo katika nchi zinazoendelea. Si ajabu nchi kama Tanzania matumizi ya mafuta kwenye transport sector ni zaidi ya 80%, industry 15%, buildings 5%.

Lakini sasa, angalia kwamba objective hapa ni kuondoa matumizi ya fossil fuel kama suluhisho la climate change. Wakati kuna nchi zinasema zitaondoa gari za mafuta, kuna nchi zinasema zitasimamisha uzalishaji wa mafuta, kwa kuwa objective ni kupunguza GHG emissions kutokana na matumizi ya mafuta. Hivyo basi, tutatarajia impact hata kwenye non-transport sectors ambazo zinatumia oil products, kama industry na buildings. Kwenye industry kwa mfano, matumizi ya mafuta kutengeneza plastics yatapungua kwa kuwa kuna kampeni za kuzuia matumizi ya plastics. Hata hapa Tanzania plastic bags sasa marufuku. Europe inaelekea ku-ban single use plastics. Synthetic lubricants pamoja na oil za magari sasa hivi ndio mtoto mpya na bora kuliko zinazotokana na mafuta. So all in all, demand ya oil itapungua, na hoja kwamba tuharakishe ku-develop mafuta yetu inabaki palepale.

Hongera kwa kubisha kisomi kwa hili.

 
Ulisoma vizuri nilichoandika au ulidandia tu? Rudia tena kusoma kwa utulivu.

Mafuta yataendelea kuchimbwa kwa miaka mingi tu ijayo na yatatumika.
Na wewe umesoma vizuri? Sijasema popote mafuta hayatachimbwa tena, nimesema matumizi yake yatapungua na hivyo kusababisha bei ya mafuta duniani kushuka sana, na haitakuwa economically feasible kwa nchi kama Tanzania kuchimba mafuta kutoka visima vyetu ikiwa reservoir ni ndogo na cost ya production na kuyasafirisha say toka Ziwa Nyasa hadi Dar es Salaam for export ni kubwa. Sana sana offshore productions ndio zita survive.

Nikasema watabaki oil producers wachache wenye production kubwa sana na hivyo kuhimili cost of production against world oil market price kwa sababu ya economies of scale au competitive advantages watakazokuwa nao. Ndio maana nikasema kama tunataka kufaidika basi tuharakishe kuendeleza mafuta yetu sasa, ndani ya miaka 10, kabla impact ya kushuka bei ya mafuta haijaikumba dunia kutokana na measures zilizopo za kuondokana na matumizi ya fossil fuels katiaka sector mbalimbali transport sector ikiongoza. Soma uelewe kabla ya kujibu
 
Mnapokua mnaleta hoja mpitia kqanza vyanzo mbalimbali vta taarifa.
Hii hapa ni habari ya Egypt.
 
Hili ni suala jingine natamani sana Mama Samia angelisikiliza. Na labda Prof. Mwandosyaanaweza kusaidia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…