Lord denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 15,819
- 33,255
- Thread starter
- #61
Kuna kazi kubwa sana Mama Samia anatakiwa kuifanya. Nayo ni kufanya uwekezaji wa kimaendeleo kulingana na faida za kiuchumi na sio Kwa sababu ya nani anatoka wapi. Kati ya Mambo ambayo yanatakiwa kufanyiwa kazi Kwa kiwango kikubwa hapa Tanzania ni hili.
Ebu fikiria Lami inayoishia Kibaoni kwao Pinda unaweza kukaa bale barabarani masaa zaidi ya matatu bila kuona gari wala pikipiki ikipita kwenye hiyo barabara...unajiukiza ilijengwa kwasababu Pinda ni Waziri mkuu?
Je barabara na daraja lililokua linaunganisha Tabora na Katavi imelaza watu njiani miaka mingi sana. Sehemu ya masaa matano watu wanakaa siku mbili barabarani na ni njia ya kufungua uchumi wa nchi na nchi achilia mbali mkoa kwa mkoa.
Ukibahatika kutembea ndani ya nchi hii unaweza kushangaa mengi sana.
Chukulia ile boarder ya kuunganisha Kenya na Tanzania upande wa Rorya - Shirati. Upande wa Kenya wamejenga majengo yao vizuri na wanakusanya mapato ila upande wa Tanzania shida kwelikweli. Licha ya ushauri uliokwisha tolea na ofisi ya CAG kuhusu ujenzi wa hizi boarde