Rais Samia kuongoza uzinduzi wa filamu ya Royal Tour

BWANKU M BWANKU

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2019
Posts
377
Reaction score
435
šŸ”„NI LEO, KUANZIA SAA 7 USIKU HUU, FILAMU YA ROYAL TOUR KUZINDULIWA RASMI NEW YORK- MAREKANI, KUWAFIKIA WATU BILIONI 1 DUNIANI KOTE.

Na Bwanku M Bwanku.

Historia inaandikwa rasmi kuanzia Saa 7 usiku wa leo Jumatatu Aprili 18, 2022 kwenye Anga za Kimataifa ambapo Royal Tour, Filamu Maalum ya Kutangaza Utalii na Uwekezaji wa Tanzania itazinduliwa rasmi kule New York, Marekani.

Dunia nzima itasimama wakati Filamu hii Maalum ya kutangaza Utalii wetu wa Tanzania ikizinduliwa pale New York ambapo Mkuu wa Nchi, Rais Samia Suluhu Hassan ni Mhusika Mkuu (Tour Guider) kwenye Filamu hii inayokwenda kueleza kila Vivutio vya Utalii na Uwekezaji vilivyopo nchini ili kuwavuta Watalii na Wawekezaji wengi zaidi Ulimwenguni kuja nchini ili tupate fedha nyingi zaidi kupitia Utalii na Uwekezaji ili tuzipeleke kwenye Uchumi na Maendeleo yetu.

Kwa Mujibu wa Dkt. Hassan Abbasi (Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo) ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Rais Samia ya Kuratibu Mpango wa Kuitangaza Tanzania Kimataifa amesema Filamu hii ya Royal Tour inatarajia kuwafikia watu Bilioni 1 katika mwaka mmoja wa kusambaza kwake.

Pia, Dkt. Hassan Abbasi amesema kuwa mikakati mbalimbali imewekwa ya kusambaza Filamu hiyo itakayozinduliwa kwa mara ya kwanza leo Jijini New York na Aprili 21 Los Angeles, Marekani kisha Dar es Salaaam Aprili 28 na Zanzibar Mei 07, 2022.

Amesema pia kuwa Filamu itaoneshwa kwenye kumbi za sinema, kwenye ndege, mitandao ya kijamii na yote hayo ikilenga kuwafikia watu wa makundi mbalimbali na kuongeza kwamba, akiwa ziarani nchini Marekani, Rais Samia Suluhu Hassan atakutana na makundi mbalimbali ya wasanii na wafanyabiashara ambao watapata wasaa wa kutazama Filamu hiyo inayoonesha fursa za uwekezaji na utalii nchini.

Kwa upande wake Waziri wa Maliasili na Utalii, Pindi Chana amesema vivutio vingi vya utalii nchini havijulikani, lakini kupitia filamu hiyo vitajulikana na watalii wengi zaidi watafika Tanzania.

Mhe. Rais Samia kwasasa ni Mwanamke anayetajwa kuwa na ushawishi mkubwa zaidi Barani Afrika na Duniani kwa Mujibu wa Majarida ya Avance Media la Ghana na Jarida la Ulimwengu la Forbes, hivyo uamuzi huu wa Rais Samia kurekodi Filamu hii ya Kutangaza Utalii wetu kama Mhusika Mkuu ni turufu ya Kimkakati sana na itafanya Ulimwengu mzima kutazama na kufuatilia Filamu hii na kujionea uzuri wa Tanzania na kumiminika kwa wingi kuja nchini.

Watanzania wote Mabibi na Mabwana tuiunge mkono Filamu hii, inakwenda kutusaidia kupandisha idadi ya Watalii kutoka chini ya Milioni 2 wasasa mpaka kufikia Milioni 5 kufikia mwaka 2025 kama ilivyo Mipango yetu ya Ilani ya CCM, Chama kinachoongoza Taifa letu inayotekelezwa na Taifa na Mipango yetu. Ni wakati wa Tanzania Kimataifa sasa.

Bwanku M Bwanku
bwanku55@gmail.com.

IMG-20220418-WA0005.jpg


IMG-20220418-WA0038.jpg


IMG-20220418-WA0040.jpg


Screenshot_20220418-203850.png


Screenshot_20220418-203859.png
 

Attachments

  • VID-20220418-WA0004.mp4
    19.2 MB
... nimeuliza kwanini haikuzinduliwa nchini badala yake uzinduzi unafannyika kwa beberu Mkuu?
 
Labda dunia ya ukoo wenu [emoji706][emoji706][emoji706][emoji706][emoji706][emoji706]
 
Labda dunia ya marekani🤣🤣
 
Sawa, nimeenda Ruaha hivi karibuni. ni hifadhi nzuri sana lakini naona Serikali imeisahau na kuipotezea kabisa.
kutoka Iringa mjini mpaka kwenye hifadhi ni 130km lakini ni kama 30km ndio zinakiwango cha lami, kwasababu hiyo unatumia masaa yasiyopungua 4 kufika kwenye hifadhi.
Hifadhi kubwa lakini wanyama haina. Wanyama niliowaona barabarani Mikumi walikuwa sawa na niliowaona wakati nazunguka hifadhini Ruaha. Nasikia mnyama Nyati (Buffalo) hayupo kabisa.
Mazingira ya huduma za kijamii bado ni duni, hayaendani na unaposikia Jina Ruaha.
Kaskazini tayari kunajiendesha na kujitangaza, serikali hamisheni nguvu Kusini kuanzia miundombinu na ulinzi kwenye hifadhi.
 
Mkuu kitulize,, acha kupiga mayowe,, tuache tutajionea wenyewe
 
Dunia hii ukitaka usifiwe kuwa Rais wa Tanzania. Yaaani utasifiwa hadi basiiiiiiii [emoji1787][emoji1787]
 
Wasiwasi wangu vile jinsi ilivyotengenezwa....

Ngoja tuone ...
Wahusika wakuu,wahusika duara ,wahusika wajenzi,manzali, vinaendana na jina na kilichomo ndani!!?

Wasije kutuletea kitu chaajabu hapa.
 
Bro ni lini uliwahi kuona dunia imesimama.? Nasemea dunia kusimama.
Hiyo ni misemo tu ya kunogesha tukio, acheni kukaza fuvu kwa maneno mepesi tu.

Isitoshe hili tukio litashuhudiwa na mamilioni ya watu ulimwenguni hivyo hakuna tatizo kusema 'dunia itasimama'.
 
Back
Top Bottom