Rais Samia kuongoza uzinduzi wa filamu ya Royal Tour
Jifunze kukubali kutokukubali. Kupinga jambo sio kupotosha bali ni haki ya kuwa na mtazamo tofauti.
Lakini ni wazi umeshupalia kupinga haki ya wengine kuwa tofauti na mtazamo wako.

Uwe na usiku mwema sasa maana inaelekea umekalia kupinga tu hapa. Ukute unalipwa kwa unachofanya hapa, naishia kupoteza muda wangu kumbe mwenzangu upo kazini kupromote movie.
Ukweli umekuuma, vumilia sindano muhimu upone.
 
That means tuko nao vizuri kuliko mabeberu. Kwanini uzinduzi haukufanyika Moscow or Beijing?
Umetumia vigezo gani kusema tuko nao vizuri kuliko mabeberu ?

Watalii wetu wengi hutokea US na nchi za EU kuliko huko China na Urusi, tunaangalia panapolipa zaidi ndio tukazindulia huko
 
🔥NI LEO, KUANZIA SAA 7 USIKU HUU, FILAMU YA ROYAL TOUR KUZINDULIWA RASMI NEW YORK- MAREKANI, KUWAFIKIA WATU BILIONI 1 DUNIANI KOTE.

Na Bwanku M Bwanku.

Historia inaandikwa rasmi kuanzia Saa 7 usiku wa leo Jumatatu Aprili 18, 2022 kwenye Anga za Kimataifa ambapo Royal Tour, Filamu Maalum ya Kutangaza Utalii na Uwekezaji wa Tanzania itazinduliwa rasmi kule New York, Marekani.

Dunia nzima itasimama wakati Filamu hii Maalum ya kutangaza Utalii wetu wa Tanzania ikizinduliwa pale New York ambapo Mkuu wa Nchi, Rais Samia Suluhu Hassan ni Mhusika Mkuu (Tour Guider) kwenye Filamu hii inayokwenda kueleza kila Vivutio vya Utalii na Uwekezaji vilivyopo nchini ili kuwavuta Watalii na Wawekezaji wengi zaidi Ulimwenguni kuja nchini ili tupate fedha nyingi zaidi kupitia Utalii na Uwekezaji ili tuzipeleke kwenye Uchumi na Maendeleo yetu.

Kwa Mujibu wa Dkt. Hassan Abbasi (Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo) ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Rais Samia ya Kuratibu Mpango wa Kuitangaza Tanzania Kimataifa amesema Filamu hii ya Royal Tour inatarajia kuwafikia watu Bilioni 1 katika mwaka mmoja wa kusambaza kwake.

Pia, Dkt. Hassan Abbasi amesema kuwa mikakati mbalimbali imewekwa ya kusambaza Filamu hiyo itakayozinduliwa kwa mara ya kwanza leo Jijini New York na Aprili 21 Los Angeles, Marekani kisha Dar es Salaaam Aprili 28 na Zanzibar Mei 07, 2022.

Amesema pia kuwa Filamu itaoneshwa kwenye kumbi za sinema, kwenye ndege, mitandao ya kijamii na yote hayo ikilenga kuwafikia watu wa makundi mbalimbali na kuongeza kwamba, akiwa ziarani nchini Marekani, Rais Samia Suluhu Hassan atakutana na makundi mbalimbali ya wasanii na wafanyabiashara ambao watapata wasaa wa kutazama Filamu hiyo inayoonesha fursa za uwekezaji na utalii nchini.

Kwa upande wake Waziri wa Maliasili na Utalii, Pindi Chana amesema vivutio vingi vya utalii nchini havijulikani, lakini kupitia filamu hiyo vitajulikana na watalii wengi zaidi watafika Tanzania.

Mhe. Rais Samia kwasasa ni Mwanamke anayetajwa kuwa na ushawishi mkubwa zaidi Barani Afrika na Duniani kwa Mujibu wa Majarida ya Avance Media la Ghana na Jarida la Ulimwengu la Forbes, hivyo uamuzi huu wa Rais Samia kurekodi Filamu hii ya Kutangaza Utalii wetu kama Mhusika Mkuu ni turufu ya Kimkakati sana na itafanya Ulimwengu mzima kutazama na kufuatilia Filamu hii na kujionea uzuri wa Tanzania na kumiminika kwa wingi kuja nchini.

Watanzania wote Mabibi na Mabwana tuiunge mkono Filamu hii, inakwenda kutusaidia kupandisha idadi ya Watalii kutoka chini ya Milioni 2 wasasa mpaka kufikia Milioni 5 kufikia mwaka 2025 kama ilivyo Mipango yetu ya Ilani ya CCM, Chama kinachoongoza Taifa letu inayotekelezwa na Taifa na Mipango yetu. Ni wakati wa Tanzania Kimataifa sasa.

Bwanku M Bwanku
bwanku55@gmail.com.

View attachment 2192194

View attachment 2192197

View attachment 2192198

View attachment 2192204

View attachment 2192206
Nonsense, majizi matupu.
 
Umetumia vigezo gani kusema tuko nao vizuri kuliko mabeberu ?

Watalii wetu wengi hutokea US na nchi za EU kuliko huko China na Urusi, tunaangalia panapolipa zaidi ndio tukazindulia huko
... tunawaalika kwenye vikao vya Chama maana yake nini Mkuu? Umewahi kuona mabeberu wakitia pua kwenye mikutano mikuu ya chama chetu? Tafakari.
 
Haya ni mahusiano binafsi ya vyama hata vyama vingine vina vyama rafiki huko dunia ya kwanza

Kuna muda viongozi wa vyama vyetu (pinzani na tawala) hukutana na mabalozi kutoka nchi za mabeberu.....hakuna jipya hapo
 
... What does it mean by mahusiano binafsi ya vyama?
 
Na vile vichapio vya mama yetu .lugha gongana mviondoe maana nilisikia sehemu moja akimwambia peter .we are safety here .mweeeee

IMG_0754.jpg
 
Waisalam wote hatuikubali Marekani maana inatuhusisha na Ugaidi, Hivyo hatukabalini na kitu kiachohusiana na USA
 
Yanalenga zaidi itikadi baina yao, kubadilishana uzoefu wa uendeshaji na uongozaji wa vyama.
... itikadi huzaa sera, sera huzaa ilani, ilani huzaa sheria. In that sense, hatuna itikadi inayoeleweka; neither east nor west au sio?
 
Yap!... tupo vuguvugu tu
 
[emoji91]NI LEO, KUANZIA SAA 7 USIKU HUU, FILAMU YA ROYAL TOUR KUZINDULIWA RASMI NEW YORK- MAREKANI, KUWAFIKIA WATU BILIONI 1 DUNIANI KOTE.

Na Bwanku M Bwanku.

Historia inaandikwa rasmi kuanzia Saa 7 usiku wa leo Jumatatu Aprili 18, 2022 kwenye Anga za Kimataifa ambapo Royal Tour, Filamu Maalum ya Kutangaza Utalii na Uwekezaji wa Tanzania itazinduliwa rasmi kule New York, Marekani.

Dunia nzima itasimama wakati Filamu hii Maalum ya kutangaza Utalii wetu wa Tanzania ikizinduliwa pale New York ambapo Mkuu wa Nchi, Rais Samia Suluhu Hassan ni Mhusika Mkuu (Tour Guider) kwenye Filamu hii inayokwenda kueleza kila Vivutio vya Utalii na Uwekezaji vilivyopo nchini ili kuwavuta Watalii na Wawekezaji wengi zaidi Ulimwenguni kuja nchini ili tupate fedha nyingi zaidi kupitia Utalii na Uwekezaji ili tuzipeleke kwenye Uchumi na Maendeleo yetu.

Kwa Mujibu wa Dkt. Hassan Abbasi (Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo) ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Rais Samia ya Kuratibu Mpango wa Kuitangaza Tanzania Kimataifa amesema Filamu hii ya Royal Tour inatarajia kuwafikia watu Bilioni 1 katika mwaka mmoja wa kusambaza kwake.

Pia, Dkt. Hassan Abbasi amesema kuwa mikakati mbalimbali imewekwa ya kusambaza Filamu hiyo itakayozinduliwa kwa mara ya kwanza leo Jijini New York na Aprili 21 Los Angeles, Marekani kisha Dar es Salaaam Aprili 28 na Zanzibar Mei 07, 2022.

Amesema pia kuwa Filamu itaoneshwa kwenye kumbi za sinema, kwenye ndege, mitandao ya kijamii na yote hayo ikilenga kuwafikia watu wa makundi mbalimbali na kuongeza kwamba, akiwa ziarani nchini Marekani, Rais Samia Suluhu Hassan atakutana na makundi mbalimbali ya wasanii na wafanyabiashara ambao watapata wasaa wa kutazama Filamu hiyo inayoonesha fursa za uwekezaji na utalii nchini.

Kwa upande wake Waziri wa Maliasili na Utalii, Pindi Chana amesema vivutio vingi vya utalii nchini havijulikani, lakini kupitia filamu hiyo vitajulikana na watalii wengi zaidi watafika Tanzania.

Mhe. Rais Samia kwasasa ni Mwanamke anayetajwa kuwa na ushawishi mkubwa zaidi Barani Afrika na Duniani kwa Mujibu wa Majarida ya Avance Media la Ghana na Jarida la Ulimwengu la Forbes, hivyo uamuzi huu wa Rais Samia kurekodi Filamu hii ya Kutangaza Utalii wetu kama Mhusika Mkuu ni turufu ya Kimkakati sana na itafanya Ulimwengu mzima kutazama na kufuatilia Filamu hii na kujionea uzuri wa Tanzania na kumiminika kwa wingi kuja nchini.

Watanzania wote Mabibi na Mabwana tuiunge mkono Filamu hii, inakwenda kutusaidia kupandisha idadi ya Watalii kutoka chini ya Milioni 2 wasasa mpaka kufikia Milioni 5 kufikia mwaka 2025 kama ilivyo Mipango yetu ya Ilani ya CCM, Chama kinachoongoza Taifa letu inayotekelezwa na Taifa na Mipango yetu. Ni wakati wa Tanzania Kimataifa sasa.

Bwanku M Bwanku
bwanku55@gmail.com.

View attachment 2192194

View attachment 2192197

View attachment 2192198

View attachment 2192204

View attachment 2192206
ITAPENDEZA WaTz tukajulishwa, kupitia Bunge, gharama za kutengeneza hiyo FILAMU na lini inategemewa gharama hizo zitarudishwa ikiwa ni pamoja na za kuitangaza km gharama za safari hiyo ya Rais na wapambe wake (nauli, malazi nk)
 
Asante mama tunakuombea mafanikio mema ili nasi tupate maendeleo
 
ITAPENDEZA WaTz tukajulishwa, kupitia Bunge, gharama za kutengeneza hiyo FILAMU na lini inategemewa gharama hizo zitarudishwa ikiwa ni pamoja na za kuitangaza km gharama za safari hiyo ya Rais na wapambe wake (nauli, malazi nk)
...
 
Back
Top Bottom