Rais Samia kusaini EPA huko Brussels?

Status
Not open for further replies.
Hakuna nchi ya Africa inaweza kushindana na nchi ya ulaya kwenye uzalishaji wa bidhaa za viwandani. China wameua kabisa viwanda vyetu vya ndani kupitia wafanyabiashara wachuuzi kariakoo na wengine kama Vunja bei.
 
Kama tumeshindwa ku compete na hizi bidhaa hafifu kutoka China ndio tutaweza ku compete na za Ulaya. Huo mkataba na Ulaya ni vigumu kuelewa unalenga kufanikisha nini kwa sababu sio rahisi kwa Watanzania wengi kununua bidhaa kutoka Ulaya waache za bei rahisi kutoka China.
 
Shauri wafanyeje sasa? hebu toa mapendekezo yako.
 
Kwa hiyo unaona ni sahihi kwa Nchi kuendelea kuwa chanzo cha mali ghafi kwa viwanda vya Ulaya! Tena wanunue kwa bei watakayo ipanga wao! Halafu wenyewe wakuletee mitumba ununue kwa bei kubwa!

Na sisi tuwauzie malighafi kwa bei tuliyopanga sisi
 
EPA bado sana wananchi wetu hawajui ni nini, tatizo kubwa ni hilo.
 
Na wewe kwa akili zako mbovu unaamini hatuna cha kuuza Ulaya? Parachichi kwa mfano hatuwezi kuuza?
Hivi kwa akili yako ilojaa maparechichi ya uozo..unategemea ulaya una import to kila takataka kama huko Tanganyika..Unijua ISO unaijua CAC..au una ropoka tu.

#MaendeleoHayanaChama
 
Inasikitisha mno hii tabia ya ku undo kila lilofanyika awamu ya tano.

Hata kama hatukumpenda Magufuli basi wakati tukiachana na mambo yake tuangalie kama alifanya kwa maslahi ya Taifa ama la.

Yeye aliheshimu ya wengine waliopita?
 
EPA bado sana wananchi wetu hawajui ni nini, tatizo kubwa ni hilo.

Kwahiyo tatizo la hiyo EPA ni kwakuwa wananchi hawajui ama? Maana hata wakijua ubaya wa huo mkataba, maadam viongozi wanataka wao watafanya nini?
 
EU wenyewe juice anakunywa za mchina

EU watatuuzia nini, karibu kila kitu tunatoa Guangzhou? Au dubai?
Tunao-import from EU tunakuangalia huku tunasema nhiiiiiiii! Anyway kufa kufaana. Kwahio hii EPA inaondoa kodi bidhaa za EU nianze kushangilia?!!
 
Hivi kwa akili yako ilojaa maparechichi ya uozo..unategemea ulaya una import to kila takataka kama huko Tanganyika..Unijua ISO unaijua CAC..au una ropoka tu.

#MaendeleoHayanaChama
Wewe kwa aki yako ya hovyo tunavyo export saizi vinatoka wapi?

EPA itatoa fursa nyingine zaidi on mutual benefits principle, ujinga hautakitoka kwa kukimbia ushindani.
 
Una nini cha ku export kwenda ulaya?
Vingi tuu,tuna exports horticultural products na Mazao mengine mengi tuu ya kilimo kama korosho na mchele.

Msivyo na akili mnadhani wao wakileta industrial products basi ni lazima na nyie mpeleke industria products.

Akili za usiku hizi,una export kile ambacho uta gain competitive advantage

Wewe kama umekaa unauza kashata usidhani wote
 
Akili za chekechea, kwahiyo machinga badala ya kwenda China kununua bidhaa Sasa wataenda nchi za ulaya kuleta bidhaa na kuzimwaga kariakoo?
Wewe ulitaka waende wapi? Ulishawahi sikia bidhaa substandard kutoka Ulaya kama ilivyo china?

With competion you got the so called citizen welfare..

Huelewi hata EPA ime constitute nini ila unaropoka tuu.
 
Reactions: Tui
Hakuna nchi ya Africa inaweza kushindana na nchi ya ulaya kwenye uzalishaji wa bidhaa za viwandani. China wameua kabisa viwanda vyetu vya ndani kupitia wafanyabiashara wachuuzi kariakoo na wengine kama Vunja bei.
Kwani EPA ipo tuu kwa ajili ya kushindana? EPA ipo kwa ajili ya kufungua fursa pia.

Saizi without EPA ndio mnashindana na Ulaya?

Good news ni kwamba tutapata soko kubwa na tutazalisha bidhaa ambazo tuna competitive and comperative advantage over them na hususani bidhaa za horticulture na kilimo kama mchele na korosho nk.

Faida ya pili ni kupata bidhaa shindani na zenye ubora kuliko sasa ambavyo tunapata hasara na mabidhaa feki ya China.
 
Kinachohitajika Sio Free Trade..., Ni Fair Trade..., Hizi Trade their Neither Free nor Fair....
 
Tutauza Tanzanite,Gold ,Vinyago na vitenge
 

Kuna sababu nyingi kwanini TZ isisaini huu mkataba miongoni mwazo ni:
1. Faida ya kusaini tayari tunaipata Sasa kwanini tusaini? Ni hivi tunasaini Ili tuuze bidhaa zetu Ulaya bila kutozwa kodi, mpaka sasa TZ kwa kuwa ipo kwenye orodha ya nchi za chini kimaendeleo yaani Least Developed Countries hatutozwi kodi bidhaa zetu zinapopelekwa Ulaya. Na bado hatujakidhi vigezo vya kutoka kwenye orodha hiyo hata kama tumeongia kwenye lower middle income countries. So hatuna sababu ya kusaini,

2. Japo bidhaa za Ulaya zitaendelea kulipa kodi zinapoingia TZ baada ya muda au taratibu kodi itapunguzwa na baadae itaondolewa kabisa, Sasa serikali itatoa wapi mapato yanayotokana na kodi hiyo? Je serikali imeshaandaa vyanzo mbadala vya kodi?

3. Je bidhaa zetu zinaubora wa kushindana na bidhaa za Ulaya? Hii inamaanisha bidhaa za ndani hazitanunuliwa na hivyo viwanda vtakufa na kuachia bidhaa za nje soko! Mwishowe watauza kwa Bei wanayotaka!

4. Viwanda vya ndani vitaweza kushindana Bei ya Mali ghafi na viwanda vya nje? Hii inamaana viwanda vyetu vitakosa Mali ghafi na hivyo kufa kifo Cha mende.

Kenya wamesaini Ili wasikose soko la Ulaya kwani wao hawako kwenye least developed countries so walilazimika kusaini Ili waendelee kupeleka bidhaa zao haswa maua na majani ya chai bila kutozwa kodi. Tuishauri serikali yetu ilifikirie hili kwa jicho la pili, wataalam serikalini msiogope kumwambia Rais ukweli!
 


 
Unahisi mkapa na kikwete hawakua na vision? Maana waliikataa kabisa hii kitu
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…