Huihui2
JF-Expert Member
- Jan 5, 2012
- 7,021
- 11,475
Ushindani na the best in the industry ndiyo kitu bora kuliko kubakia tunashindana na the weakest. Haijalishi leo tuna vichache vya kuuza huko kama Majani ya chai na Kahawa ila tukiwa na akili ya kuona mbele tunaweza tuka export holticulture products, nyama za mbuzi na kondoo na live animals kama mijusi, vipepeo, vinyonga etcIle Trade Agreement EPA iliyokuwa inapingwa kwa kila hali na CCM sasa kusainiwa na Raisi wa Tanzania Samia huko Brussels kwenye EU- Afrika Union summit.
EPA ni free trade Agreement Kati ya EU na Nchi za Afrika Mashariki zikiwemo Tanzania, Kenya, Uganda, Burundi na Rwanda.
Tanzania walipinga EPA kwa maana hawakuona manufaa yoyote kwa nchi yetu kwani hatuna cha kuuza EU wakati EU wana kila kitu cha kuuza kwetu.
Je, Viwanda vyetu juice ya Azam na umeme wa mgao vita compete na EU products? Kama hapo Kenya tu au Uganda ni ngumu kushindana tutaweza EU ?
Ikumbukwe sukari kutoka Brazili ni cheaper kuliko ya Tanzania sasa EU products tax free Tanzania, tutaweza?
Tunategemea kuuza nini EU ? Vipi natural resources zetu ?
Kweli ni Vita ya Kiuchumi RIP Magu …
Kwa mtazamo wangu Mama anaupiga mwingi, tumuunge mkono tu kwa kuzalisha vilivyo bora.
Lakini kama tumeamua kuwa wasindikizaji kwenye uchumi wa Dunia basi tuendelee kubeza juhudi za Rais SSH