Rais Samia kusaini EPA huko Brussels?

Rais Samia kusaini EPA huko Brussels?

Status
Not open for further replies.
Ile Trade Agreement EPA iliyokuwa inapingwa kwa kila hali na CCM sasa kusainiwa na Raisi wa Tanzania Samia huko Brussels kwenye EU- Afrika Union summit.

EPA ni free trade Agreement Kati ya EU na Nchi za Afrika Mashariki zikiwemo Tanzania, Kenya, Uganda, Burundi na Rwanda.

Tanzania walipinga EPA kwa maana hawakuona manufaa yoyote kwa nchi yetu kwani hatuna cha kuuza EU wakati EU wana kila kitu cha kuuza kwetu.

Je, Viwanda vyetu juice ya Azam na umeme wa mgao vita compete na EU products? Kama hapo Kenya tu au Uganda ni ngumu kushindana tutaweza EU ?

Ikumbukwe sukari kutoka Brazili ni cheaper kuliko ya Tanzania sasa EU products tax free Tanzania, tutaweza?

Tunategemea kuuza nini EU ? Vipi natural resources zetu ?

Kweli ni Vita ya Kiuchumi RIP Magu …
Ushindani na the best in the industry ndiyo kitu bora kuliko kubakia tunashindana na the weakest. Haijalishi leo tuna vichache vya kuuza huko kama Majani ya chai na Kahawa ila tukiwa na akili ya kuona mbele tunaweza tuka export holticulture products, nyama za mbuzi na kondoo na live animals kama mijusi, vipepeo, vinyonga etc

Kwa mtazamo wangu Mama anaupiga mwingi, tumuunge mkono tu kwa kuzalisha vilivyo bora.

Lakini kama tumeamua kuwa wasindikizaji kwenye uchumi wa Dunia basi tuendelee kubeza juhudi za Rais SSH
 
Tupambane, tuache uvivu watu wafanye Kazi. Kuna mazao mengi Sana ambayo tunaweza kuuza ulaya. Mfano mzuri ni asali yanahitajika sana Ulaya.Tuna mapori mengi Sana lakini tumeshindwa kupambana tunabaki kulaumu kwamba hatuna Cha kuuza ulaya. Ukienda pale Vijibweni watu wanazalisha asali, sisi tunabaki kulaumu.
 
Lakini hatuhitaji EPA ili tuweze kuuza hao mazao na asali Ulaya, sasa hivi bado tunapewa upendeleo kama ldc countries kuuza hayo mazao yote ulioyataja EU, hivyo kwetu EPA hatuihitaji, isitoshe kama mpaka sasa hivi hatujaweza kuuza hiyo asali EU ambapo tunapewa upendeleo maalumu tutawezaje kuuza baada ya EPA ?

Kama mtu haujajipanga siyo dhambi kusubiri kwanza kuliko kuingia kwenye mpambano ambao umeshashindwa tangia mwanzo.
 
Ushindani na the best in the industry ndiyo kitu bora kuliko kubakia tunashindana na the weakest. Haijalishi leo tuna vichache vya kuuza huko kama Majani ya chai na Kahawa ila tukiwa na akili ya kuona mbele tunaweza tuka export holticulture products, nyama za mbuzi na kondoo na live animals kama mijusi, vipepeo, vinyonga etc

Kwa mtazamo wangu Mama anaupiga mwingi, tumuunge mkono tu kwa kuzalisha vilivyo bora.

Lakini kama tumeamua kuwa wasindikizaji kwenye uchumi wa Dunia basi tuendelee kubeza juhudi za Rais SSH

Unajua ni kwa nini Kampuni za Bia Tanzania zinanunua shairi kutoka nje wakati inalimwa hapa hapa pia ingawaje hiyo shairi ya kutoka nje bado inatozwa kodi lkn Kampuni za bia kwao bado ni bora kuagiza nje ? Tanesco tu wanaagiza nguzo za umeme nje miti ipo unajua ni kwa nini ? Sukari ya nje pamoja na kodi bado ni rahisi klk ya hapa hapa kwetu unajua ni kwa nini ? Leo hii ukiondoa kodi hali itakuwaje ?
 
Nimesoma na kusema ilkabidi nicheke tuu! Kusema kweli Rais wetu si mwenye tabia ya kusoma vitu hata kidogo! Sitashangaa yeye akisaini kwakuwa kaambiwa! Rais wetu yeye huwa akikutana na mkataba ni kusaini tuu wala sina hakika kama anao muda wa kusoma hata kidogo.

Rais Samia ana udhaifu wa kutopenda kufatilia kujipa muda wa kujitafakari na kupitia mambo yeye huwa ni mtu wa kuanguka tuu sahihi hana muda kabisa.......

Nakumbuka hata ule mkataba pale bandarini alishiriki utiwaji saini baadae akaja kugundua aliingizwa cha kike

Lakini Rais Samia anahitaji kushauriwa zaidi kabla ya kusaini mikataba ni lazima tuangalie mbele na tujiulize je viwanda vyetu na huo uchumi wa viwanda tutafika kweli?

Rais Samia lazima awe makini kwa watu wake wanao mshauri!
Mshauri wake ni tony blair ambaye alikuwa mpiga debe mkubwa wa epa
 
Huko tuendako nadhani nafasi ya u Makamu wa Rais itatiliwa maanani

Hiyo kansa ya kupata viongozi wabovu tayari imeshamea. Kumbuka wakati wa kumtafuta makamu wa rais, vikao vyote rais huyu anakuwepo. Hamuwezi kumchagua makamu wa rais makini kwa kusema kuuepuka tatizo la kuwa na rais kama huyu. Na kwa mifumo yetu viongozi wetu wengi ni watu wenye uwezo mdogo, lakini ni mahodari wa fitina, majungu na hila. Watu wenye uwezo huwa hawataki uongozi, maana huwa wanaogopa changamoto za kuchafuliwa kwenye uga wa siasa.
 
Pia umesababisha wananchi kuwa mazuzu kusubiria kila kitu serikali na kulaumu,hatujui ubunifu na kuchangamkia fursa.

Ndio maana mimi naona turuhusu afu kwa njia hiyo tutajifunza kuwa aggressive badala ya kubaki na kurithishana maujinga yetu.

Naunga mkono Rais kusaini.

Umewaza kama mimi, East Africa tunawaogopa wakenya ooh wakija kwetu watachukua ajira zetu. Kwanini tusiwaze kuwa waje tushindane nao tupate kilicho bora.
Kama tunauziwa majuice famba tukomae nayo badala ya kuwapa ushindani watengeneze nzuri?
 
Kwa gharama ya Viwanda vyetu ? Vipi kuhusu ajira za watu wetu waliojiriwa kwenye hivi viwanda vyetu? Vipi kuhusu mapato ya kodi tunayoyapata sasa hivi kwa kutoza kodi imports ? Nani atafidia hiyo yote ?

Viwanda vitengeneze bidhaa bora
 
Umeongea ukweli! Rais Samia sio mtu ambae anaweza kusoma jambo na akalichambua ye mwenyewe kwa mapana lakini ata akishauliwa bado ni kazi bure maana naamini uo mkataba alishawahi kuusikia enzi za JPM akiusema hauna maslahi kwetu!

Samia anaamini kwenye Ubepari, Samia anaamini ili taifa liendelee lazima mzungu ashirikianenae direct, Samia atakubali masharti mengi ya ovyo kutoka upande wa Magharibi cos anawatetema pia anawanyenyekea pia.

Naamini yule alietuambia Baba wa Mikata hana kazi kule na sitaki kuamini kama kaendanae maana kwahakika yule hawezi kuukubali ule mkataba.

Huyo JPM sio reference ya taifa. Sio kila alichosema tufuate mama anaakili zake acha aongoze kivyake
 
Tunalima korosho,kahawa,pamba nk.

Kwa hiyo unaona ni sahihi kwa Nchi kuendelea kuwa chanzo cha mali ghafi kwa viwanda vya Ulaya! Tena wanunue kwa bei watakayo ipanga wao! Halafu wenyewe wakuletee mitumba ununue kwa bei kubwa!
 
EPA imejadiliwa toka enzi za Mkapa, hatua za mwisho hapa nilisikia tunafanya majadiliano ya mwisho kwa mambo ambayo tulikuwa hatujakubaliana, nadhani sasa tumefikia muafaka ndio maana Rais kasaini.
 
Hiyo kansa ya kupata viongozi wabovu tayari imeshamea. Kumbuka wakati wa kumtafuta makamu wa rais, vikao vyote rais huyu anakuwepo. Hamuwezi kumchagua makamu wa rais makini kwa kusema kuuepuka tatizo la kuwa na rais kama huyu. Na kwa mifumo yetu viongozi wetu wengi ni watu wenye uwezo mdogo, lakini ni mahodari wa fitina, majungu na hila. Watu wenye uwezo huwa hawataki uongozi, maana huwa wanaogopa changamoto za kuchafuliwa kwenye uga wa siasa.
"Those who are too smart to engage in politics are punished by being governed by those who are dumber" - Plato
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom